Mke wa Mtikila, Georgia Mtikila ateuliwa Mwenyekiti wa DP

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
pic+mtikila.jpg

Chama cha Democratic Party (DP) kimemteua Georgia Mtikila kuwa mwenyekiti wa chama hicho kitaifa

Dar es Salaam. Chama cha Democratic Party (DP) kimemteua Georgia Mtikila kuwa mwenyekiti wa chama hicho kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba.

Georgia alikaimu nafasi hiyo tangu alipofariki dunia mwasisi wa DP, Christopher Mtikila kwa ajali ya gari Oktoba 2015 maeneo ya Chalinze Mkoa wa Pwani.

Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari leo Juni 20, Georgia amewataka wajumbe wa chama hicho mikoani kufanya kazi kwa kufungua matawi ili kukiimarisha chama hicho katika ngazi zote.

“Mkaimairishe chama kwa kufungua matawi katika ngazi zote za mkoa, wilaya, kata, tawi, kitongoji na shina ili kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,” amesema Georgia katika taarifa hiyo.

Georgia ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, amewataka viongozi wa chama hicho waliochaguliwa kuwa na mshikamano wa pamoja wa kukijenga chama na kuachana na majungu na masengenyo.

Amewasihi viongozi hao kusoma katiba na kuielewa ili kusaidia katika shughuli zao, kujiepusha na migogoro ya chama.

Alisema migogoro ikitokea wanatakiwa kufuata katiba ya chama au itakapozidi wahusika wakatafute suluhu nje ya chama.

Georgia amewataka viongozi wa Serikali hasa ofisi ya Msajili kuheshimu yaliyomo ndani ya katiba za vyama vya siasa na kama kuna mapungufu ya vipengele awape ushauri.

“Ofisi ya msajili inatakiwa kuheshimu yaliyomo katika baadhi ya vipengele ndani ya katiba zao, kama kuna kasoro basi msajili anaweza kushauri kuvibadili au kuvifuta vipengele husika,” amesema Georgia.

Viongozi wengine 19 waliochaguliwa katika mkutano wa chama ni pamoja na Dastan Malle ambaye amekuwa Makamu Mwenyekiti na Haji Ally Makamu ambaye ni Mwenyekiti wa DP Zanzibar.

Chanzo: Mwananchi
 
View attachment 529417

Mwenyekiti anateuliwa?
Mwenyekiti anachaguliwa
 
Mkuu naomba unielimishe kidogo kivipi hiyo statement yako!?
CHADEMA iliundwa na mzee mmoja alikua waziri wa fedha wa wakati wa Nyerere anaitwa Edwin Mtei kwa kuwazidi kete kina Marando Prince Bagenda na kutumia jasho lao kuanzisha CHADEMA sasa kakikabidhi kwa mkwewe anaitwa Freeman Mbowe. DP kilianzishwa na Mchungaji Mtikila kwa kumzidi kete rafiki yake kwa kubadilisha jina kutoka Kiswahili kwenda kimombo na kukiita Demcratic Party na kukiongoza kama mali ya familia mpaka hapo umauti ulipomfika na sasa waliobaki wanakirudisha kwenye familia na mke wa Mtikila atapokea kijiti. CHADEMA pesa nyingi inatoka serikalini lakini nusu inaenda kwa familia maana ndiyo inayokikopesha chama vitu vingi kwakua mbowe ni bepari usidhani kama anawapa bure, huko DP Kina Mtikila wanatumia pesa zao wenyewe na michango ya watu wema kwa njia mbalimbali iwe ya kitapeli kisiasa ama la
 
Ha haaa! Baada ya kuona uenyekiti dili eeh! Safi mama, kuna mkoa mpya wa Korogwe unaanzishwa, fursa hiyo...
 
CHADEMA iliundwa na mzee mmoja alikua waziri wa fedha wa wakati wa Nyerere anaitwa Edwin Mtei kwa kuwazidi kete kina Marando Prince Bagenda na kutumia jasho lao kuanzisha CHADEMA sasa kakikabidhi kwa mkwewe anaitwa Freeman Mbowe. DP kilianzishwa na Mchungaji Mtikila kwa kumzidi kete rafiki yake kwa kubadilisha jina kutoka Kiswahili kwenda kimombo na kukiita Demcratic Party na kukiongoza kama mali ya familia mpaka hapo umauti ulipomfika na sasa waliobaki wanakirudisha kwenye familia na mke wa Mtikila atapokea kijiti. CHADEMA pesa nyingi inatoka serikalini lakini nusu inaenda kwa familia maana ndiyo inayokikopesha chama vitu vingi kwakua mbowe ni bepari usidhani kama anawapa bure, huko DP Kina Mtikila wanatumia pesa zao wenyewe na michango ya watu wema kwa njia mbalimbali iwe ya kitapeli kisiasa ama la

Mkuu mtikila alimzidi kete nani?

Na alibadilisha jina gani la kiswahili kuwa hilo DP la leo???

Nataka nikajiunge. Nilikua namkubali sana na misimamo yake kuhusu uTanganyika wetu
 
Mkuu naomba unielimishe kidogo kivipi hiyo statement yako!?
Ze chadema was founded by mzee mtei who is ze Baba mkwe of freeman mbowe. Who is now ze ze chaiman Of ze ze chadema so ze congulusheni is ze ze That when mbowe gets ze ze ruzuku he gives ze ruzuku to his ze ze babamkwe. Zeafor chadema is ze family property
 
Hivi chadema bado ni cha familia ya Mtei? Mbona nilisikia Lowasa alitosha bei au alikodi kwa muda kama yanga ilivyotaka kukodishwa kwa Manji?
 
Ze chadema was founded by mzee mtei who is ze Baba mkwe of freeman mbowe. Who is now ze ze chaiman Of ze ze chadema so ze congulusheni is ze ze That when mbowe gets ze ze ruzuku he gives ze ruzuku to his ze ze babamkwe. Zeafor chadema is ze family property

Utaacha lini kutumia masaburi kufikiri?
 
Ze chadema was founded by mzee mtei who is ze Baba mkwe of freeman mbowe. Who is now ze ze chaiman Of ze ze chadema so ze congulusheni is ze ze That when mbowe gets ze ze ruzuku he gives ze ruzuku to his ze ze babamkwe. Zeafor chadema is ze family property
Childish!
 
Back
Top Bottom