Mke wa Mrema azikwa aliliwa kila Kona, mchango wake kuenziwa

Kilimanjaro

BAADHI ya viongozi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini wamesema kuwa wataendelea kumkumbuka aliyekuwa mdhamini na mjumbe wa halimashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Tanzania Labour(TLP)Marehemu Rose Mrema kwa kwa ushauri wake na busara zake wakati wa kampeni na harakati za kisiasa katika kipindi cha uhai wake.

Marehemu Rose Mrema aliyekuwa mke wa Mwenyekiti wa Taifa wa TLP,Augustino Mrema alifariki tarehe 16 mwezi huu katika hospitali ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na tatizo la shinikizo la damu alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa jana tarehe 21 nyumbani kwake Kiraracha Wilaya ya Moshi vijijini Mkoani hapa

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere,alisema kuwa atamkumbuka sana marehemu Rose katika harakati zake za kisiasa katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini mwaka 1995,wakati mume wake akigombea Urais kupitia Chama Cha NCCR-Mageuzi .

“Nakumbuka kipindi hicho nilipata fursa ya kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kampeni nikiwa na mgombea urais pamoja na marehemu ambapo ndipo nilipoanza kujifunza siasa kwa undani zaidi kwani marehemu alikuwa akiendesha siasa za ustarahabu zisizokuwa na chuki na uhasama”alisema

Nyerere aliongeza kuwa Taifa limepata pigo kubwa sana kwani tangu Augustino Mrema kushika madaraka ya kuwa Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa mambo ya ndani ya mbunge katika majimbo mbalimbali hapa nchini kwa vipindi tofauti hakukuwahi kutokea na malumbano wala majibizano kati ya serikali na wananchi na hiyo yote ni kutokana na busara zake marehemu.

Akitoa salamu za pole kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Vunjo, Mbunge wa Jimbo hilo Dkt.Charles Kimei(CCM), alisema kuwa marehemu atakumbukwa kwa jitihada zake katika kuhakikisha kuwa kina mama
,vijana na wasiojiweza wakiwemo walemavu ndani ya jimbo hilo wanajikwamua kiuchumi.

“Marehemu alikuwa anawapa mikopo nafuu ambayo ilikuwa aikiwasaidia kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi pamoja na kuondokana na umasikini,ambapo pia aliwasaidia vijana kupata elimu pamoja na misaada mbalimbali kwa makundi ya wasiojiweza.”alisema Mbunge huyo

Dkt.Kimei alisema kuwa jamii inatakiwa kumkumbuka marehemu kwa kutambua mchango wake alioutoa jimboni hapo na kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wa marehemu Rose mrema kwani mbali na Siasa pamoja na michango yake ya kimaendeleo jimboni hapo alikuwa akimkumbuka Mungu wakati wote kwani alishiriki katika shuguli mbalimbali ya kidini ikiwemo ujenzi wa nyumba za ibada pasipo kujali itikadi ya kidini.

Kwa upande wake mume wa marehemu,Augustino Mrema alisema kuwa akilia atakuwa anamkufuru Mungu kwani ameishi naye katika ndoa kwa miaka 48, hiyo hata akilia aitomsaidia chochote kwani hata angepewa miaka zaidi ya hiyo ni lazima angekufa kama maandiko yasemavyo kila nafsi lazima itaonya mauti.

“Mke wangu Rose ni kama aliona kifo chake kwani hivi karibuni aliikutanisha familia yake yote na kuipa nasaa ambapo alisisitiza waishi kwa amani na upendo huku wakijikita zaidi akatika kusaidia makundi yenye uhitaji katika jamii na kumtanguliza Mungu. Hivyo wanangu wasiponiangalia kama alivyokuwa akiniangalia mama yao watakuwa
wamekiuka wosia wa marehemu mke wangu”alisema Mrema

Akiongoza sala ya mazishi Paroko wa Parokia ya Uomboni Marangu,jimbo Katoliki la Moshi,Padri Adelard Imani alisema kuwa wamempoteza msharika wa muhimu sana kwani alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wakisaidia Kanisa na jamii kwa ujumla hivyo watamkumbuka na wao kama parokia watazidi kumuombea apumzike kwa amani.

Marehemu Rose Mrema alizaliwa mwaka tarehe 5 mwezi 1 mwaka 1954 huko Marangu mkoani hapa ambapo ameacha mume, watoto sita na wajukuu kumi na tatu

Mwisho

View attachment 1948213View attachment 1948214View attachment 1948215
Mbona alishindwa kumshauri mmewe amuunge mkono mgombea wake wa TLP badala ya kumuunga mkono mgombea wa CCM Magufuli!
 
Wewe bila kumtaja Mbowe husikii raha ese?
Uwe unajadili kilichopo mezani. Sawa?
Kila saa Mbowe, Mboweee au ndio ile 'mti wenye matunda kuurushia mawee', anyway its Up to you!
Mbowe akifungwa nitafanya sherehe kubwa ,kubwa sana

USSR
 
Mbowe akifungwa nitafanya sherehe kubwa ,kubwa sana

USSR
Sisi ni binadamu na sio nyani. Unachosema utafanya ni tabia za kinyani, wewe ni binadamu?
Usifurahie mateso ya mwenzio sababu tu ya tofauti ya kimtazamo.

Orodhesha hapa sababu zako za msingi zitakazokufanya ufurahie.
 
Sisi ni binadamu na sio nyani. Unachosema utafanya ni tabia za kinyani, wewe ni binadamu?
Usifurahie mateso ya mwenzio sababu tu ya tofauti ya kimtazamo.

Orodhesha hapa sababu zako za msingi zitakazokufanya ufurahie.
Nyani nyie wakati tunamzika JPM hamkufanya sherehe ,ni zamu yenu sasa

USSR
 
Nyani nyie wakati tunamzika JPM hamkufanya sherehe ,ni zamu yenu sasa

USSR
1.Weka picha tuone hiyo sherehe unayoisema.

2. Orodhesha sababu zako zinazofanya usherekee Mbowe akifungwa.
1.
2.
3.
4.
5.
Vinginevyo itakuwa uatakuwa na tabia za kinyani nyani.
Kuwa binadabu, ishu, weka virungu chini shindanisha hoja, basiii.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom