Mke wa mganga wa kienyeji ananitaka, Nifanyeje?

secretary POMPEO

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,895
2,000
habari zenu wadau

Leo nikiwa nipo free sina ishu ya kufanya nilienda zangu maeneo ya Kisiju Pwani kuangalia shamba langu la hekari takribani 40, pembeni ya shamba hilo anaishi mzee mmoja makamo yake kama miaka 65 hivi lakini ameoa Mwanamke mwenye umri wa miaka 30.

Nikiwa niko zangu shamba naangalia mipaka akaja huyo mke wa mganga " Habali yako leo umekuja tena kuangalia minakwambiaga unipe namba yako niwe nakujulisha maendeleo ya huku weutakiii! "

Ikabidi nimwambie ukweli kua sitaki mazoea na wake za watu! Lakini cha kushangaza mwanamke yule alishindwa kuzuia hisia zake na kunishika mkono huku akiniangalia machoni na kuniambia ananipenda sana, daaah! Kiukweli sikuamini mwanaume mzima niko natongozwa katikati ya mikorosho.

Ikabidi nimtoe mkono wake alionishika niondoke zangu nikamwacha kasimama pale na namba sikumpa wala nini.

Kiukweli huyu mwanamke ni mzuri sana mweupeeee, kiukweli yule mzee mganga anajua sana kuchagua lakini ndio naogopa kulogwa.

Nijilipue?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kinderu

Member
Feb 20, 2020
74
150
Budaa mke wa mtu sio poa,Ukijafanya mwamba ipo siku utakuja kujua why kifo cha mende n maarufu kuliko wadudu wengine.

Barnes
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,148
2,000
Kuna habari zinavuma kwenye mitandao ya kijamii kuwa wewe ni pandikizi kutoka Lumumba ambae umepewa kazi ya kuvuruga attentions za watu juu ya udikteta wa serekali kwa kuanzisha nyuzi nyingi za uongo per day!Kuna ukweli wowote ndugu?
 

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,877
2,000
Kama shida ni kurogwa ondoa shaka kabisa.. hakuna kitu kama hicho duniani.

Lakini.kumbuka mke wa mtu ni sumu.. antidote yake ni kutembea na mafuta tu incase ukifumwa usichubuliwe sana.
 

Lugumgya

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
631
1,000
1. Kama amekushika mkono, atakuwa tayari ashakuambukiza Corona, nenda nae karantini siku 14. Mkitoka huko, uje na mrejesho wa sehemu zingine atakazo kuwa amekushika.

2. Naona unataka kujilipua, rudi shambani ukajilipulie huko huko, hapo nafikir utakuwa umesafisha shamba, na wew utakuwa umebahatika kufia shambani kwako.

Kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 

secretary POMPEO

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,895
2,000
1. Kama amekushika mkono, atakuwa tayari ashakuambukiza Corona, nenda nae karantini siku 14. Mkitoka huko, uje na mrejesho wa sehemu zingine atakazo kuwa amekushika.

2. Naona unataka kujilipua, rudi shambani ukajilipulie huko huko, hapo nafikir utakuwa umesafisha shamba, na wew utakuwa umebahatika kufia shambani kwako.

Kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
Najilipua

Sent using Jamii Forums mobile app
 

MR. IBU

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,318
2,000
Pitanaye tu achauoga....yaani huwezi kuwa baharia wewe kitu kidogo tu hicho.mimi mwenzako nilimtapeli mganga tena anaogopwa na kila mtu kwa balaa lake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom