Mke wa Mbunge Lema ashtakiwa kwa kumtumia ujumbe Mkuu wa Mkoa wenye neno 'Shoga'

olevaroya

JF-Expert Member
May 6, 2012
1,224
512
Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini, Neema Tarimo amefikishwa mahakamani jijini Arusha na kusomewa shtaka la kumtukana Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo baada ya kumtumia ujumbe kwenye simu yake wenye neno 'shoga'.

Mke wa Mbunge huyo amekana kumtusi Mkuu huyo wa Mkoa baada ya kudai kuwa neno shoga sio tusi bali ni neno ambalo hulitumia kuwaita marafiki zake.

Amesema neno shoga kwenye mazingira ya Tanzania humaanisha rafiki.



=========

Lema atamani mkewe alale magereza kwa siku 14

MKE wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema, Neema Lema (33), mkazi wa Njiro, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kuunganishwa katika kesi ya mume wake ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuwa ni shoga.
2f662ca8-bd67-4aba-8059-651a2c0a9a5a.jpg

Godbless Lema akiwa na Mkewe, Neema Lema

Akimsomea mashitaka hayo kwa mara ya kwanza, Wakili wa serikali Blandina Msawa, mbele ya hakimu Agustino Rwezile, alidai kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha alimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani Mkuu huyo wenye lugha ya matusi Mkuu huyo, huku akijua ni kosa kisheria.

Alidai mtuhumiwa huyo alituma ujumbe kutoka 0764150747 namba 0756551918 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”
Gambo.JPG

Mrisho Gambo - Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Mshitakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena kesi hiyo.

Hata hivyo baada ya kuachiwa huru nje ya Mahakama, Neema alisema anashanga kuunganishwa katika kesi hiyo, lakini yeye hajamtukana Mkuu wa Mkoa, japo simu ni yake ilitumika kama wanavyodai kutuma ujumbe huo.

“Mimi wanadai nimemtumia meseji za matusi katika simu ya Gambo na sijamtukana Mrisho Gambo, ila kwa kuwa simu ni mali yangu, hivyo niko tayari kupambana na Mrisho Gambo na mimi nawasiliana na Mrisho Gambo na sio kwa mara ya kwanza, ila tunawasiliana sielewi kwa nini hii achukulie matusi,”alisema.

Godbless-Lema-Arusha.jpg

Mbunge Godbless Lema

Mbunge Godbless Lema, alisema anashukuru mke wake anapita kwenye mambo anayopitia na itamfundisha ujasiri wa kuomba vizuri na tangu awe na matatizo mke wake hajawahifikishwa amahakamani na yeye siku hiyo ni Baraka kubwa kwake.

“Ila nilitamani aende akajue magereza ipoje kwa kukaa siku 14 magereza ila madiwani wamenishauri sana nikaona tumdhamini tu, ila ushoga sio jambo baya, ila tutamshinda na tutamdhibiti gambo na tunaamini haki yetu tutaipata mahakamani,”alisema.

Chanzo: EATV
 
Kwani anaogopa kusema kweli, jamani huyo ni mke wa kamanda si aseme tu ukweli kuwa alidhamiria kumuita huyo RC shoga liwalo naliwe! anaogopa nini kuanza kupindisha pindisha maneno? ooooops nimekumbuka na yule mheshimiwa aliyegoma kula halafu akasingizia eti alikuwa amefunga, waache woga wajiamini waseme wazi walichodhamiria huo ndio "UKAMANDA"
 
Haki ya mtu haiwezi kupotea.
Japo kwa sasa mahakama zetu zina dalili zote za kuingiliwa na watawala kimaamuzi lakini mtashinda Lema.
 
Amekamatwa kwa sababu gani au alikataa kudhalilishwa na mkuu kama alivyofanya kule korogwe?
 
Kwani anaogopa kusema kweli, jamani huyo ni mke wa kamanda si aseme tu ukweli kuwa alidhamiria kumuita huyo RC shoga liwalo naliwe! anaogopa nini kuanza kupindisha pindisha maneno? ooooops nimekumbuka na yule mheshimiwa aliyegoma kula halafu akasingizia eti alikuwa amefunga, waache woga wajiamini waseme wazi walichodhamiria huo ndio "UKAMANDA"

Ninyi mliohusishwa kitabia na Mwenyekiti Wenu( Sio Mwingine au kujitungia mfanyavyo ninyi, hili limetoka kwenye kinywa chake) kuwa ndani ya chama kuna wenye tabia hizi:-

upload_2016-11-1_13-19-41.png
mna tabu kweli kweli, na mtahangaika mpaka :D:D:D:D:D:D:D:D
 
Back
Top Bottom