Mke wa marehemu Mengi atoa onyo kali kwa wanaonyemelea mali za marehemu

Kama nakuelewa hivi... hao watoto wa mengi wameshindwa kuendeleza ukoo.. nahisi hii ilimtisha mengi.. hata akiwaachia mali itapotea tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa unaanza kuelewa sio kama ulivyobwabwaja hapo juu, wale watoto wamezaliwa kimkakati baada ya uzao wa kwanza kuonekana hakuna kitu.... mzee alifanya vile ili kupata warithi wa kuendeleza mali.

Fikiria hao Regina na kaka yake ni wazee sasa na hakuna dalili za kupata watoto, naamini hili limemtesa sana mzee Mengi na huenda ndio sababu kubwa kuamua kuoa upya na uzee ule.... hao watoto wadogo ilikuwa furaha yake ya kweli.

Kuhusu urithi mali zilishapigwa mgao alipoachana na mkewe mkubwa na alipofariki ile sehemu ya mama yote ilienda kwa watoto wake.... huo urithi ulioandikwa kwenye wosia ni katika lile tu fungu lake ambalo ni sahihi kabisa kulielekeza kwa watoto wake hawa wadogo chini ya mama yao.

Kinachowaumiza hao ‘first generation’ ni ile wivu kwa bi mdogo ni kama alijiingiza kimkakati, na pia wanamtuhumu kuhusika na RIP ya Mzee..... wanasahau kuna watoto kule ambao ni ndugu zao na ni warithi halali.
 
Tafuta hela za kukutosha wewe tu, kufariki na kuacha ziada ni dhulma hivyo hupelekea ugomvi na kutoelewana.... Mengi hakurithi mali.
Ni sisi tu black people ndo tuna tatizo la kugombea Mali...The first world walishatoka huku..Unawezaje kutafuta pesa inayokutosha tuu wewe!! Muhimu ni kuweka mambo yetu clear wakati tupo hai na kuwandaa waendelezaji siyo warithi...
 
Vipi mrithi asipoupinga mahakamani, lakini mtu mwingine akaupinga mahakamani kwa niaba ya mrithi, halafu mrithi akashinda?

Is that a loophole?
nadhani kwakuwa huyu mtu mwingine nae yupo upande wa mrithi jibu litakua lile lile haki yao ni BUKU tu (1000) kwasababu kaupinga kwa niaba ya mrithi means mpingaji ni mrithi hivyo bado wosia umeshasema haki ya hawa watu ni jero mbili tu yani sh mia tano mbili

picha kwa msisitizo 👇👇

images.jpg
 
nadhani kwakuwa huyu mtu mwingine nae yupo upande wa mrithi jibu litakua lile lile haki yao ni BUKU tu (1000) kwasababu kaupinga kwa niaba ya mrithi means mpingaji ni mrithi hivyo bado wosia umeshasema haki ya hawa watu ni jero mbili tu yani sh mia tano mbili

picha kwa msisitizo

View attachment 1343026
aroo hii kama comedy walai yaani mtu anaipiginia buku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utalipwa pesa taslimu kiasi cha shilingi elfu moja za kitanzania.

Safi sana hii ni fundisho kwa wale ndugu wanaonyemeleaga mali za marehem

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ni wosia ,na wosia ukishakuwa batili ni batili, hivyo kifungu kitakuwa hakina nguvu tena.

Itakayotumika kugawa mali ni sheria sasa sio wosia tena.

Kifungu hakina maana, kama wosia ni batili.
 
Back
Top Bottom