Mke Wa Koplo Hamisi

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,619
1,799
Kamanda wa majeshi ya ulinzi na uslama Tanzania, alikuwa anakaguwa wanajeshi wake katika gwaride lililofanyika kule Makutupora, akasimama kwa mwanajeshi wa kwanza na kumuuliza:

jina lako nani kijana...?

Koplo Hamisi Afandiii... (akajibu mwanajeshi),

Kamanda akamuuliza Koplo Hamisi:

Na hii ni nini umelibeba?

Koplo akajibu: hili ni bunduki langu-mheshimiwa Afandii.

Kaamanda: Hapana!! nataka kuanzia leo hili musiliite bunduki, unaliita mke wangu-umesikia?,

Ndio mheshimiwa akajibu Kpl.Hamisi.

Kamanda akasimama kwa mwanajeshi wa pili na kumuuliza:

Jina lako nani?

Koplo Daudi: Koplo Daudi mheshimiwa Afandii...! akajibu.

Kamanda akamuuliza na hii ni nini? (akimaanisha ile bunduki alobeba)

Koplo Daudi akajibu: Huyu ni mke wa Koplo Hamisi - mheshimiwaaa Afandiii...!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom