Mke wa Kanali Muammar Gaddafi wa Libya akimbilia nje ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa Kanali Muammar Gaddafi wa Libya akimbilia nje ya nchi

Discussion in 'International Forum' started by mdau wetu, May 19, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mke wa Kanali Muammar Gaddafi wa Libya akimbilia nje ya nchi [​IMG]Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imekanusha habari kwamba mke wa dikteta wa Libya Kanali Muammar Gaddafi Safia amekimbilia nchini humo akiwa pamoja na binti yake Aisha Gaddafi. Ripoti ya awali ya vyombo vya usalama vya Tunisia ilisema kuwa Safia Gaddafi amefikia katika hoteli moja katika kisiwa cha Jarba nchini Tunisia. Ripoti hiyo imesema Safia na Aisha Gaddafi waliwasili nchini Tunisia jioni ya Jumamosi iliyopita.
  Awali vyombo rasmi vya Tunisia viliripoti kuwa mwana mkubwa wa kiume wa kiongozi wa Libya Muhammad Gaddafi amewasili nchini humo kwa kile kilichotajwa kuwa ni kwa ajili ya kupata matibabu. Baadhi ya duru za kuaminika zimesema familia ya Gaddafi imeondoka Tunisia na kuelekea Poland.
  Maafisa wengi wa ngazi za juu wa serikali ya Libya wameendelea kujitenga na utawala wa Gaddafi na kukimbia nchi baada ya kushadidi mashambulizi ya wanamapinduzi wanaosaidiwa na vikosi vya majeshi ya NATO dhidi ya ngome za Kanali Muammar Gaddafi.  Kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran, Iran
   
 2. zinginary

  zinginary JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2016
  Joined: Dec 18, 2015
  Messages: 1,795
  Likes Received: 1,085
  Trophy Points: 280
  Yupo hai.huyu mama.mpk sasa??
   
 3. Hussein Melkiory

  Hussein Melkiory JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2016
  Joined: Jan 25, 2016
  Messages: 4,675
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  Ndio yupo hai nadhani atakuwa NIGER
   
 4. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2016
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,897
  Likes Received: 24,232
  Trophy Points: 280
  Kama mimi niliumia hadi kutoa machozi kwa kifo cha Gaddafi sipati picha mkewe.
  Dah
   
 5. radika

  radika JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2016
  Joined: Jul 15, 2014
  Messages: 10,546
  Likes Received: 12,333
  Trophy Points: 280
  kweli maisha hayana formular muda wowote unaweza kuanza kuishi kwa wasiwasi.
   
 6. Amon Mtekateka

  Amon Mtekateka JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2016
  Joined: Jun 4, 2014
  Messages: 1,234
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Na libya sasa wanajutia hil kwan walidanganywa wakadanganyika
   
 7. dasenior

  dasenior Senior Member

  #7
  Aug 3, 2016
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Bado wanazidi kumpaka matope na kumuita dikteta?
   
 8. D

  Dina JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2016
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kwani yupo kwenye wanted list? Kama ndiyo ya nani, walibya? Anaunganishwa na makosa ya Gadaffi ? (kama kweli yapo).
   
 9. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2016
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 25,897
  Likes Received: 24,232
  Trophy Points: 280
  Thubutuuuuu!Wanalia na kusaga meno sasa.
   
 10. thesym

  thesym JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2016
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 2,442
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Hayupo walimuomba arudi kwenye mji wa baida ili serikali ipate support ya Yale makabila ambayo yapo loyal kwa Gaddafi kwa sababu eneo ambalo amezaliwa gadafi ISIS wanatawala. Mwezi pili mwaka huu mtoto wa kike wa Gaddafi ambaye sasa yupo Oman aliaema ataunda serikali ya siri na kuna makabila ambayo yapo loyal kwa Gaddafi wapo tayari kumuunga mkono. Kiufupi Libya si salama tena watu wao kila siku wanazama na maji baharini kukimbilia ulaya.
   
 11. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2016
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Wabongo tusikubali kudanganywa kama walivyodanganywa wenzetu wa Libya.
  Nalog off
   
Loading...