Mke wa hayati karume mama fatma karume afunguka kuhusu muungano.

KengeWaKijani

Hebu fanya editing hayo maandishi yako usomeke vizuri, format ya utenzi, lugha ina makosa ya spelling kibao, hebu kuwa makini kidogo unajishushia hadhi ya Uzanzibari wako.
 
Last edited by a moderator:
*Mke wa Rais wa kwanza
Zanzbar jana alifunguka na
kutoa dukuduku zake kuhusu
Kupitia mahojiano ya Live katka
kpind cha KUTOKA ZENJ
Kirushwacho kila jumapil na
ktuo cha Television cha Chanel
10


*Mama huyo alisema
MUUNGANO umepoteza dira,
hata kama marehemu MMEWE
Angekuwepo leo asingekubali
tena uwepo


*Asema Mmewe
hakuiunganisha ZANZBAQ ili
imezwe Tanganyika ila ilataka
mataifa haya mawili
yashirikiane.


*Asema Zanzibar inanyanyaswa
na haitendewi haki kitu
ambacho kmefanya muungano
kuwa mzigo na adhabu kwa
wazanzibara, muungano
Umeleta umaskin mkubwa
Zenj.


*Asema mambo ya hela/cash/
noti si ya muungano kila taifa
kivyake, atoa ushahd kuwa hata
enz za uhai wa waasis wa
Muungano, Nyerere alituma
mtu zanzibar kuuata Noti,
mmewe AKAMTOLEA
NJE...............Alipomuulza
mmewe kwanini amekataza
noti zsiende bara?
.........Karume akasema Mambo
ya hela cyo ya muungano,
zanzibar nchi ndogo haiwez
kuhudumia taifa kubwa kama
tanganyika.


*Asema Nafasi zote za juu na
nyeti Wabara wametwaa zote,
Asema Tanzania ina MABALOZI
33 wanaoiwakilisha katka kona
mbalimbali za dunia, lakini
Wazanzibara ni watatu(3) Tu!


*BOAT tangu ianzishwe miaka
ile hajawah kuwepo Gavana
kutoka Zanzibara, Majuzi ndo
wakapgwa changa la macho
wakapewa naibu gavana ambae
nae hayuko huru Amewekewa
Watanganyika wawil(2)
kumsimamia


*Asema yeye kama mke wa
Mwasisi wa MUUNGANO
Hakuna anachofaidi na
anatamani mme wake
angekuwepo


*Huku akitoa chozi, alisema
yeye AMETELEKEZWA na
serkali ya Kikwete(Tanganyika)
Wake wa Marais wengne
wanahudumiwa na serikali
ikiwepo kwenda kutibiwa India.



*Aishukuru serkal ya Zanzibar
kwa kumhudumia licha ya
kutelekezwa na serkal ya
KIKWETE


*Asema katib mpya
icporekebsha hili bora
wanzibara wadai uhuru wao.

Cortsey of Mwananchi

Hahah wanapenda kwenda India hawa
 
Huyu mama maneno yake kama kweli
Mh kwa kweli wa Zenji wanatia huruma bora waachwe kivyao.
Cjui sasa wapemba walioko huku wote tutawapa uraia!

Wapewe uraia kwa kipi kizuri wanachotufanyia? Nao wanasepa tu hatuwataki.
 
KengeWaKijani

Hebu fanya editing hayo maandishi yako usomeke vizuri, format ya utenzi, lugha ina makosa ya spelling kibao, hebu kuwa makini kidogo unajishushia hadhi ya Uzanzibari wako.

Kweli kabisa Mkuu Zomba.
 
Last edited by a moderator:
Huyu Bibi nae anazeeka vibaya, anasema anashukuru Serikali ya Zanzibar inamkumbuka but serikali ya Kikwete imemtosa..sasa Alitaka avutemshiko huku na huku, au anataka aishi kama Malkia..Mwanae Balozi,Mwingine alikuwa Rais ...wajipange wampeleke mama yao India

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
anataka awe anabebwa na gari kushikana mikono na watu, pia gari na maafisa wa serikali ya muungano wawe wanamfutia vumbi viatu vyetu kila akinyanyia mguu wake. HUYU MAMA HAZIJUI SHIDA, HALAFU ANALALAMIKA KUPATA SHIDA
Mama huyu nadhani amesahau fadhila mbona wakati mtoto wake yupo madarakani hakuyasema hayo? Ammesahau kuwa wabara ndiyo waliomuweka mtoto wake madarakani na kuwa kama sio hao isingekuwa rahisi kupata mbele ya Dk Bilali wakati ule ambapo ndiye aliyekuwa anaungwa mkono?

Mnyonge mnyongeni lakini kwa hili la kumlaumu Rais kikwete nadhani mama karume alitafakari kwa makini
 
Ukiangalia sana utaona huyo mama kikubwa anachopigia kelele ni kutaka yeye na familia yake wapewe upendeleo... Sio familia hiyo iliyo pora ardhi za masikini huko unguja?

aende zake kule.....
 
*Mke wa Rais wa kwanza
Zanzbar jana alifunguka na
kutoa dukuduku zake kuhusu
Kupitia mahojiano ya Live katka
kpind cha KUTOKA ZENJ
Kirushwacho kila jumapil na
ktuo cha Television cha Chanel
10


*Mama huyo alisema
MUUNGANO umepoteza dira,
hata kama marehemu MMEWE
Angekuwepo leo asingekubali
tena uwepo


*Asema Mmewe
hakuiunganisha ZANZBAQ ili
imezwe Tanganyika ila ilataka
mataifa haya mawili
yashirikiane.


*Asema Zanzibar inanyanyaswa
na haitendewi haki kitu
ambacho kmefanya muungano
kuwa mzigo na adhabu kwa
wazanzibara, muungano
Umeleta umaskin mkubwa
Zenj.


*Asema mambo ya hela/cash/
noti si ya muungano kila taifa
kivyake, atoa ushahd kuwa hata
enz za uhai wa waasis wa
Muungano, Nyerere alituma
mtu zanzibar kuuata Noti,
mmewe AKAMTOLEA
NJE...............Alipomuulza
mmewe kwanini amekataza
noti zsiende bara?
.........Karume akasema Mambo
ya hela cyo ya muungano,
zanzibar nchi ndogo haiwez
kuhudumia taifa kubwa kama
tanganyika.


*Asema Nafasi zote za juu na
nyeti Wabara wametwaa zote,
Asema Tanzania ina MABALOZI
33 wanaoiwakilisha katka kona
mbalimbali za dunia, lakini
Wazanzibara ni watatu(3) Tu!


*BOAT tangu ianzishwe miaka
ile hajawah kuwepo Gavana
kutoka Zanzibara, Majuzi ndo
wakapgwa changa la macho
wakapewa naibu gavana ambae
nae hayuko huru Amewekewa
Watanganyika wawil(2)
kumsimamia


*Asema yeye kama mke wa
Mwasisi wa MUUNGANO
Hakuna anachofaidi na
anatamani mme wake
angekuwepo


*Huku akitoa chozi, alisema
yeye AMETELEKEZWA na
serkali ya Kikwete(Tanganyika)
Wake wa Marais wengne
wanahudumiwa na serikali
ikiwepo kwenda kutibiwa India.



*Aishukuru serkal ya Zanzibar
kwa kumhudumia licha ya
kutelekezwa na serkal ya
KIKWETE


*Asema katib mpya
icporekebsha hili bora
wanzibara wadai uhuru wao.

Cortsey of Mwananchi

TUJADILI.

Yaani KUTIBIWA INDIA ndiyo kumemliza?? Kama ugonjwa wake ulikuwa unaweza kutibiwa hapohapo UNGUJA bado angependa tuu kwenda INDIA ili awe sawa na WAKE WA MARAIS WENZIE???

Nadhani hawa WALIOZOEA KULA KWA VIJIKO VYA DHAHABU wanazidi kulewa madaraka na kuzidi kusahau UKWELI WA MAISHA YA NCHI HII TUNAYOISHI WANANCHI!!!!
 
Kwanza huyu mama si ndio waarabu hawa waliolazimishwa kuolewa na watu weusi kule Zanzibar katika kampeni ya Karume kuondoa ubaguzi wa waarabu na wabantu? Hivi aliolewa na Karume kwa mapenzi yake kweli? Mtu wa namna hiyo lazima atasema mume wangu angekuwapo asingekubali tena muungano.

Hapo umemzulia kabisa. Aliolewa na Karume way before Mapinduzi, na watoto wake kina Ali na Amani wamezaliwa kabla ya mapinduzi. Mapinduzi yametokea kina Ali na Amani tayari wanasoma shule Malawi.
 
Pamoja na mabaya yote ya Karume ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Zanzibar lakini alikuwa muumini mkubwa wa muungano alikuwa radhi tuungane na kuwa nchi moja na yeye kuwa makamu wa rais lakini huyu mama kwanza hana shukrani chini ya muungano watoto wake wameweza kujipatia nyazifa za urais na ubalozi na pia wamedhulumu ardhi kubwa ya wananchi wa Zanzibar pia kama amesahau kura za wanaccm wa bara ndizo zilimuingiza mwanae ikulu pamoja na kwamba hakuwa na sifa na pia hakuwa anakubalika na ccm zanzibar.Naombea muungano uvunjike hata leo hili wanafiki wote wanaoona wanamezwa chini ya muungano waumbuke kumbuka chini ya muungano wao wameweza kujitwalia arhi bara ingawa wabara hawaruhusiwi kufanya hivyo ,wametapakaa nchi nzima wakifanya shuguri zao bila bugudha,sasa hivi wanashindana kujenga na kununua nyumba ilala,magomeni,kariakoo,kigamboni,kibaha badala ya kwenda kujenga kwao ,nafasi za elimu ya juu wanazopata kiupendeleo na umeme ambao hawaulipii
 
Huyu bibi wa ajabu sana.......

Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayochunguza ubadhirifu wa mali za Serikali ya Zanzibar imeitaka serikali kurejesha kiwanja alichopewa kinyume na sheria, mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume.


Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi kiwanja hicho namba 186 chenye mita za mraba 750 kipo katika mtaa wa Kinazini, mkabla na Jemgo la historia la Dk. David Livingstone, mjini Unguja.


Ripoti imeeleza kwamba kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kabla ya kupewa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) kujenga makao makuu yake. Uchunguzi wa kamati umebaini kuwa ZRB baada ya kupewa uwanja huo walishindwa kuuendeleza baada ya kupata uwanja mwingine katika eneo la Mazizini na kujenga makao makuu yake na uwanja ulirejeshwa Wizara ya Ardhi.


Ripoti imesema Wizara ya Kilimo ilitoa kiwanja hicho kwa ZRB kupitia barua ya Agosti 28, 2002 yenye kumbukumbu WKMMU/29/5/41/72 kwenda Wizara ya Ardhi ya kuwapa ZRB. Uamuzi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili ulikubaliwa na Wizara ya Ardhi na kukabidhi uwanja kwa ZRB Septemba 9, 2002 kupitia barua yenye kumbukumbu namba MUNA/34/14/378/ VOl.1 na kutoa shahada ya haki ya matumizi ya ardhi ya Aprili 4, 2003.


Hata hivyo, ripoti imesema baada ya ZRB kupata sehemu nyingine ya kuendelea na ujenzi waliamua kukirejesha kiwanja hicho serikalini ambapo aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Makazi,Maji na Nishati, Mansour Yussuf Himid, aliamua kiwanja hicho kumpatia mama yake Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, mwaka 2010.


Akihojiwa na kamati hiyo Desemba 7, mwaka jana, Waziri Mansour, ambaye sasa ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum alikiri kiwanja hicho kumpa mama Fatma Karume baada ya kumuomba ili aweze kukitumia kwa shughuli zake za biashara ambazo hazijaelezwa.


Ripoti imeeleza kwamba baada ya mama Fatma kupewa uwanja huo ndani ya mwezi mmoja aliuuza kwa Kampuni ya F & K Enterprises Limited, ambapo anamiliki na hisa.


Uchunguzi umebaini kuwa baada ya mama Fatma na wenzake kupitia kampuni hiyo kukabidhiwa uwanja huo waliuuza kwa Sh. milioni 150 kwa mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Ali Shahib Khamis, na Waziri kumpatia hati miliki namba L.O.NO Z-53/S.178/2010/186 na R.O.NO Z-150/2010 ikiwa ni shahada ya matumizi ya ardhi iliyotolewa kwa mujibu wa sheria namba 12 ya ya ardhi ya mwaka 1992.


Akihojiwa na kamati juu ya kuuza ardhi hiyo ndani ya mwezi mmoja tangu kupewa mama Fatma, Mansour alisema hii ilitokana na kampuni yao kushindwa kufikia malengo waliojiwekea na hivyo kumua kukiuza kiwanja.


Kamati imesema haikuridhishwa na utaratibu wa kisheria uliotumika kutoa kiwanja cha serikali baada ya mama Fatma Karume na wenzake kushindwa kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha maombi yao kwa wizara kabla ya kutolewa kiwanja hicho.


“Mpaka tunatoa taarifa hii hakuna ushahidi wowote ambao mama Fatma aliuwasilisha pamoja na kuahidi angefanya hivyo kama alivyotakiwa kufanyaharaka iwezekanovyo,” ripoti imesisistiza. Ripoti imeeleza kwamba kamati ilichukua hatua mbali mbali za kufuatilia suala hilo ikiwa pamoja na kuwahoji watendaji wakuu wa wizara, lakini imeshindwa kupata ushahidi wa maombi ya barua ya mama Fatma Karume au kampuni hiyo.


“Kamati kwa kauli moja inathibitisha kwamba hakuna ushahidi wa kuombwa kiwanja hicho na hivyo, ina wasiwasi waziri ametumia vibaya madarakan yake, ameamua kukimilikisha kiwanja cha serikali kwa mtu bila ya maombi yoyote kinyume na taratibu na sheria,” ripoti inasema.


Hata hivyo, kamati imesema baada ya Waziri Mansour kuhojiwa juu ya kukosekana kwa maombi ya wahusika, alisema yalikuwepo maombi ya kampuni ya F&K Enterpreses LTD katika faili maalum na alishangazwa na taarifa za kutoweka kwa nyaraka hizo.




SOURCE: NIPASHE
 
Kwenda kutibiwa India imekuwa fashen siku hizi.

..... Naumwa mafua wacha nikimbie hapo India mara moja nikatibiwe..!!!!!
 
Back
Top Bottom