Elections 2010 Mke wa Dr.Slaa ajitoa CCM, Ajiunga na Chadema

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
MKE wa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Rose Kamili aliyekuwa akigombea ubunge Jimbo la Hanang kwa tiketi ya CCM, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho tayari kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
 
Anataka kugombea ubunge kupitia chadema huko karatu nini? au tayari wameshampata mtu.

This woman seems to be a fighter and an independent minded.
 
Si anaweza nae akatangaza NIA tena hapo hapo Hanang?
Hongera mama kwa maamuzi magumu
 
Sasa mama unaona mzee anagombea urais na wewe unaenda kugombea ubunge CCM, unatakiwa kumsupport mzee, sasa mzee akienda Ikulu na wewe unawakilisha chama pinzani itakuwaje, kutakuwa hakuna surbotage kweli?

Samahani wengine mnaweza kuni-quote wrong, lakini nafikiri ndo ilivo, nchi zote hata kama mama ana independent mind lakini mzee anapowania oval office mama lazima amsuport no matter what, so nashukuru mama kwa kulitambua hilo mapema, mzee yupo serious and sio kwamba CHADEMA inajaribu but tunashinda mwaka huu, so jiandae uwa first lady
 
MKE wa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Rose Kamili aliyekuwa akigombea ubunge Jimbo la Hanang kwa tiketi ya CCM, ametangaza kujitoa kwenye chama hicho tayari kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

amechanganyikiwa huyo naye si alikuwa diwani ccm? kwanza kamponza mwenzio akatoka upadri
 
amechanganyikiwa huyo naye si alikuwa diwani ccm? kwanza kamponza mwenzio akatoka upadri
Wewe utafikiri hivyo hata Dr. Slaa watu walimwona kachanganyikiwa wakati anajitoa CCM.
 
Anataka kugombea ubunge kupitia chadema huko karatu nini? au tayari wameshampata mtu.

This woman seems to be a fighter and an independent minded.
Inawezekana ikawa Karatu au Hanang alikokuwa anagombea. Namsahuri agombee Karatu jimbo lililokuwa chini ya mme wake na akatangazie nia kwenye kampeni ya Slaa inayoendelea ya kutafuta wadhamini aungane nao huko litakuwa boost la nguvu.
 
wito wangu kwenu wana chadema. kusanya watu kumi na zaidi hakikisha wanapiga kura kwa chadema. udiwani, ubunge na urais.
 
Inawezekana ikawa Karatu au Hanang alikokuwa anagombea. Namsahuri agombee Karatu jimbo lililokuwa chini ya mme wake na akatangazie nia kwenye kampeni ya Slaa inayoendelea ya kutafuta wadhamini aungane nao huko litakuwa boost la nguvu.
hapana alikuwa na nia ya Hanang na pia Karatu kuna mtu anayekubalika zaidi, ni bora aende Hanang
 
Ingependeza sana Raisi akiwa anatoka Chadema Na mkewe anatoka CCM.
Hapo tungekuwa kioo cha demokrasia duniani.
 
amechanganyikiwa huyo naye si alikuwa diwani ccm? Kwanza kamponza mwenzio akatoka upadri

una uhakika unacho .....kinena..........upadri ni wito kama ujaitwa hata uje jf utaishia kwenye ndoa...alikuwa na uamuzi wake binafsi....nafikiri haya ni maisha ya mtu si vyema tukayaingilia nyie ndio tunawaalaani mnatuletea udini oooh padri katumwa na waroma wee.....tema mate chini
 
Back
Top Bottom