Prodigal Son
JF-Expert Member
- Dec 9, 2009
- 1,067
- 696
Mussa Juma, Arusha
MKE wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Rose Kamili, ambaye Diwani wa CCM wa Kata ya Bassotu, wilayani Hanang, amelituhumu jeshi la polisi wilayani Hanang kutumika kisiasa kutokana na kutekeleza maagizo ya kigogo mmoja kutaka yeye akamatwe pamoja na viongozi wa wafugaji.
Diwani huyo, ambaye ametangaza kugombea ubunge jimbo hilo la Hanang katika uchaguzi mkuu ujao kupitia CCM, alisema kukamatwa kwake juzi pamoja na wananchi wengine 13 ni shinikizo la kigogo huyo.
"Polisi wamenikata na kunipa dhamana mimi na Ally Kaoga jana na wamegoma kutoa dhamana kwa wananchi wengine 12 hili ni shinikizo la kigogo huyo tumepata taarifa amewaahidi baadhi ya wakulima kuwapa mashamba na wanataka kuzuwia dhamana ili walazimishe ugawaji wa mashamba," alisema Rose Kamili.
Kamili ambaye ni Diwani wa CCM tangu mwaka 1994 na amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya CCM ikiwepo ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, alisema mgogoro wa mashamba ya Hanang hivi sasa umefanywa wa kisiasa ili kuficha ukweli.
"Mimi nasema ugawaji wa mashamba Hanang uwe wa haki na wafugaji wapewe haki yao kwani kihistoria wao ndio walipokonywa na serikali maeneo yao na kuwafanya watawanyike karibu nchi nzima ili kuanzisha shirika la chakula la NAFCO," alisema Kamili.
Diwani huyo alisema kitendo cha kigogo huyo, kutembelea eneo la mgogoro kufanya mkutano wa hadhara juzi na kuahidi kuwashughulikia watu aliowaita wachochezi ni ishara kuwa suala hilo limekuwa la kisiasa.
"Mimi wanasema ni mchochezi nawachochea wafugaji wasikubali mgawanyo wa shamba eti nafanya mikutano usiku....huu ni uongo kwani wafugaji kama watanzania wengine lazima haki yao ijulikane na ndicho nimekuwa nikitetea,"alisema Kamili.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani Permena Sumari alikanusha tuhuma kuwa polisi inatumika kisiasa katika kutatua mgogoro wa ugawaji wa mashamba ya Hanang.
"Sisi hatufuati siasa tunaowakamata tutawafikisha mahakamani kwa tuhuma za kufanya uvamizi kwa viongozi wasigawe ardhi na kuwashambulia wananchi wengine kwa silaha,"alisema Sumari.
Kamanda huyo alifafanua kuwa,operesheni ya kuwakamata wananchi wote waliohusika na vurugu itaendelea hadi wote wawe wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
"Ambao tumewakamata tumewanyima dhamana kwa sababu za kiusalama na sio kisiasa kwani hakuna shaka kuwa vurugu zilitokea na watu kujeruhiwa,"alisema Sumari.
Februari 11 mwaka huu, viongozi wa serikali ya kijiji cha Mulbadaw pamoja na wananchi wengine walishambuliwa na kundi la wafugaji ambao walikuwa wanapinga eneo lao kugawanywa kwa wakulima.
Katika vurugu hizo watu zaidi ya 10 walijeruhiwa vibaya kwa silaha za jadi na hadi jana watu wanne walikuwa bado wamelazwa katika hospitali ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) ya Haydom.
Chanzo: Mwananchi