Mke wa Bilionea Msuya na Mwenzake wakamatwa tena baada ya kuachiwa huru

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Jeshi la Polisi limewakamata mke wa bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake R. Muyela muda mfupi baada ya Mahakama ya Kisutu kuwaachia huru.

Mwanamama huyo aliwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji ya wifi yake (Mdogo wa mume wake), marehemu Anathe Msuya aliyechinjwa kinyama Mei 25, 2016 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni.

Rejea:

Annate ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya auawa kinyama Dar

Mjane wa Erasto Msuya apandishwa Kizimbani Kisutu

Mahakama kutoa uamuzi malalamiko kesi mauaji ya dadake Msuya

Wakili aitaka mahakama imuachie huru mke wa bilionea Msuya
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyela wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Aneth Msuya.

Hata hivyo muda mfupi baada ya kuachiwa huru, askari polisi wamewakamata tena na kuwapandisha kwenye gari polisi na kuondoka nao.

Awali, Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ya mauaji ya kukusudia iliyokuwa ikiwakabili mahakamani hapo.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya jalada la kesi hiyo lililokuwa limeitwa Mahakama Kuu kurejeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Februari 20, 2017 Hakimu Mwambapa aliupa upande wa mashtaka muda wa siku tatu kurekebisha hati ya mashtaka.


Chanzo: Mwananchi
 
2..5..5 HIYO,HUYO MAMA HAKUJIANDAA KUCHOMOKAA MAHAKAMANI FASTAAA

OVA
ili ufanikiwe kuchomoka huwa inafanyika mipango kwa Askari B4 siku ya kutolewa huo Uamuzi wakati wakuachiwa Askari anajifanya kapata Bumbuwazi wewe ushatoka Getini.....lkn bila Mipango huna ujanja wa kukwepa kukamatwa tena!
 
ili ufanikiwe kuchomoka huwa inafanyika mipango kwa Askari B4 siku ya kutolewa huo Uamuzi wakati wakuachiwa Askari anajifanya kapata Bumbuwazi wewe ushatoka Getini.....lkn bila Mipango huna ujanja wa kukwepa kukamatwa tena!
Mama msuya hakujipanga naona au hakulifahamu hilo

Ova
 
Mama msuya hakujipanga naona au hakulifahamu hilo

Ova
Yote yanawezekana....ukiwa na KESI haijalishi uko Mahabusu au una Dhamana hutakiwi Kulala muda wote unatakiwa uwaze kesi....Mahakamani kuna michezo mingi...ndio maana utakuta kuna Hukumu zinatolewa hadi watu mnashangaa....
 
Kuna mtu humu ndani aliulizaga et kwanin watu wakiachiwaga mahakamani wengine hutoka nduki hili ndio jibu sasa ina onekana mama ajui nduki au wakili wake akumpanga vizuri
 
Back
Top Bottom