Mke wa balozi Daraja auawa; Mfanyakazi wa nyumbani atafutwa

Kuna namna ambayo mjadala huu ulitakiwa uwe umeenda,lakini naona bado hatujafikia hapo.

Ninaweza kuwa na baadhi ya assumptions kuhusiana na ni kwanini bado hatujafika "Huko"

Nimegundua kuwa tamaduni zetu nyingi haziendani na the so called ethics...Mifano ni mingi lakini kwa haraka haraka ni mambo kama longevity ya breaks,utamaduni wa rushwa,wa kufanya mambo mengine yasiyohusu kazi wakati wa kazi nk.

Nimetoa mfano huo hapo juu ili kuelezea ni kwanini hatujafika "Huko" kwenye mjadala....Sasa naona nielezee kwa ufupi where is "Huko"

Moja tuna ule utamaduni wa kuwa jadili baadhi ya members wa society ambao ni watumishi wa umma ama wana madaraka kwa namna ya tofauti na wananchi wa kawaida pale inapokuja kwenye issue zinazowakabili,kwa mfano kuwaita wezi wa pesa wa wananchi "Mafisadi" na wananchi wanaokamatwa kwa wizi wa pesa za wananchi wenzao tunawaita just wezi ama viibaka ama majambazi,na kwa upande wa mafisadi due process yao certainly ni tofauti na ya wezi wengineo wa pesa za wananchi ie vibaka na majambazi, kwa kifupi wale wasiokuwa na wadhifa ama nafasi ya utumishi wa jamii ama wale wasiokuwa na madaraka wako treated tofauti hata kwenye mijadala na due process etc,na hivyo ufisadi ni kinga dhidi ya kuwa mwizi wa kawaida.

Back to the point hapa,kaa nilivyosema hapo awali,nilichelea kusema haya kwasababu nilijiuliza kama nifuate utamaduni wetu wa kutokuzungumzia mambo flani flani hadi hapo matanga yatakapokuwa yameanuliwa.

Hata hivyo kutokana na heading,habari hii imekaa kwa namna ambayo maswali ya nini hasa kilichotokea kupelekea msiba huo yanajitokeza kwa namna ambayo ni vigumu kuyafumbia macho.

Kwenye kesi kama hii,mtuhumiwa wa kwanza ni Mh Balozi Daraja,kwanza kabisa samahani kama kuna watakaokuwa wamekwazika kwa kusema haya kutokana na ukweli kwamba msiba huu umemgusa yeye kama mtu wa karibu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kwa victim...Hivyo hatua ya kwanza kwa wapelelezi ni kumwondoa mh Balozi kwenye utata wa aina yeyote kuhusiana na mauwaji hayo,then baada ya kumclear wana move kuangalia ni nani mwingine anayeweza kufanya mauaji hayo.

Wakati wanaangalia namna ya kum clear mume,wakati huo huo pia ni lazima waangalie motives zinazoweza kupelekea mauwaji hayo,kwamba ni nani atakayetaka victim huyo afe na ni kwanini ie atanufaika vipi na kifo hicho.

Mara nyingi kwa wenzetu wa west huwa wanaangalia kama kulikuwa na mahitaji ya pesa nk,halafu kama hitaji la pesa lilikuwepo,say this time kwa familia ama hata Balozi Daraja mwenyewe,then wanaangalia insurance policy waliyonayo ilikuwa ni ya kiasi gani,je amount ya insurance ni kubwa kiasi ambacho kinaweza kupelekea ushawishi wa mauwaji?Je alikuwa akihitaji pesa hizo?nk.

Hivyo basi long story short,kama ni kweli wana JF tunatakiwa tuende na upelelezi inavyotakiwa kwenye analysis hapa,tunagalie kwanza namna ya kum clear Mh Balozi Daraja kabla hata ya huyo msaidizi/house boy wtever!

Kwa hiyo sasa badala ya kusema ooh Balozi Daraja alitakiwa afanye hili ama lile,tunaangalia ni kwanini inawezekana alifanya/hakufanya hivi ama vile
 
siamini jambo hili limeweza kutokea mchana kweupe na kusiwe na mashahidi... tusubiri tu vitu vitakapoanza kufunuliwa..
 
Pole sana kwa wafiwa na mwenyezi mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.

d. The story:

Wacha we... .... MM Mwanakijiji mimi naona nisiseme maana kama wale walio ughaibuni wanaangalia FBI Files documentaries hapo iko kazi.

Bandugu angalieni hizo programmes ni muhimu sana kwa wale wanaoweza hasa walio USA, UK na popote pale ambako zinatolewa na hata askari polisi wetu ili kujua mbinu na mienendo ya uhalifu na jinsi ya kupata evidence etc.
Angalieni crimelibrary.com.....zipo story nyingi sana kama hii!
RIP in peace Hanna.
 
kama wengi walivyo ongea , hii hadithi ina matundu mengi, kwanza kwa siku hizi msaidizi wa kazi na mama wengi wana simu ukitilia maanani hiyo nyumba wana kaaa watu watatu, tena Kimara ambako viwanja/shamba ni kubwa , je mzee hakumpigia simu huyo msaidizi kuulizia mbona simpati Mama?
Pili Yeye akiwa Mstaafu na anakaa huko Shambani kimara na nyumba za huko na wadhifa wake etc kwa kweli itakuwa kubwa na hiyo nyumba ya Msaidizi awe wa nje au wa ndani , je kulikuwa hakuna ndugu/mtu yoyote zaidi anaye kaa hapo? angalau kumpa kampani Mama Mzee akitoka?
au Walikuwa hawana Mlinzi? na alipo rudi hakuwa na Funguo za Geti mpaka dereva aruke ukuta? na kama kulikuwa na struggle katika tukio hawakuweza kuona michirizi ya damu toka nyumba kubwa kwenda Garage, au tuseme mama alikuwa attack Garage, labda akirudi toka matembezini etc kwa hiyo mtuhumiwa alimfungulia mama Main Gate na Garage Gate, then akamchoma kisu then , kwenye mlango wa garage kumngekuwa na damu, na inawezekana mtuhumiwa akawa na damu kwenye nyao na mikono hivyo alivyo ingia ndani kupekua fedha nk damu zingeonekana au dalili za tukio la mauuaji lingeonekana.
Jingine Balozi kaajiri msaidizi wa shamba/wa ndani Bila kumjua vizuri au kupewa reference??/
 
siamini jambo hili limeweza kutokea mchana kweupe na kusiwe na mashahidi... tusubiri tu vitu vitakapoanza kufunuliwa..
swala mda hapa nimuhimu sana mkuu.ndio maana nikasema pale mwanzo hii "late evening" ni vizuri angetaja mda wenyewe kamili hili wapelelezi waangalie kuanzia mda ule wa mchana aliongea nae mpaka mda huo ambao hakupatikana (yani hio simu ya pili aliopiga "late evening").
 
Jasusi.. that is the story we have been told; but in a situation like this there is a story behind the story. Ngoja nioneshe matundu machache kwenye stori ilivyo sasa.

a. The Story:

Kwa hiyo.. timeline yetu ni kuwa lolote lililotokea lilitokea siku ya Jumamosi kati ya mchana na jioni. Halikutokea usiku. Kama lilikuwa ni tukio la ujambazi na matumizi ya nguvu kiasi hicho hao majambazi watakuwa ni watu wa karibu sana kiasi cha kutokusababisha shuku toka kwa majirani mchana kweupe; na hiyo ina maana wapo mashahidi walioona kilichotokea, gari, watu n.k

Balozi alilala salama usiku ule bila kutoa taarifa polisi, kwa ndugu, jamaa na marafiki huku akiwa hana mawasiliano na mke wake na hajasema kama alijaribu kuwasiliana na msaidizi huyo wa nyumbani. (this is important to keep in mind)

b. The Story:

Sasa tunajua kuwa Balozi alilala salama usiku wote ule na hakufanya juhudi ya kupiga simu nyumbani siku ya pili wala kutoa taarifa kwa mtu mwingine yeyote. Muda huo unatoa nafasi ya mtu yeyote kutoweka na kuchelewesha uchunguzi.

Lakini pia tunaona jambo jingine muhimu kwa upelelezi. Malango ya nyumba ya Balozi yalikuwa yamefungwa kwa ndani. Sasa hapa hatuna budi kujiuliza huyo msaidizi wa nyumbani alitokaje na vitu vya kuiba halafu akafunga mlango kwa ndani kiasi kwamba mtu aliye nje anashindwa kuufungua?

La pili ni kuwa Balozi hana ufunguo wa mlango wa nyumba yake akiwa nje?

c. The Story:

Hapa kuna tatizo kidogo. Kwenye upelelezi tunaweza kusema ni kutokubaliana kwa eneo la tukio (inconsinstence of crime area). Viatu vya mhanga na mabegi yake yamekutwa karibu na geti. Vilifikaje hapo? Je mhanga aliuawa nje, aliwafukuza wahusika, hapa ni clue nzuri.. kulikuwa na damu karibu na geti?

d. The story:

So far.. tunachosikia hapa ni kwamba ndani ya nyumba na eneo zima hakukuwa na ushahidi wa foul play! Ina maana huyo mama hakuuawa ndani ya nyumba au nje ya nyumba kwani kama kungekuwa na damu au aina yoyote ya ushahidi kuwa amedhurika wangeita polisi mara moja. Kama walikuta ushahidi wa kitendo kibaya walipoingia ndani (hasa baada ya kukuta viatu vyake nje na mabegi) walitakiwa kutoa taarifa polisi mara moja, itakuwaje kama wabaya walikuwa bado wako ndani wanasubiri? especially baada ya kujua kuwa geti lilifungwa kwa ndani?

d. The story:
[Just when he was about to give up, he remembered to look inside his garage and…there she was, laying on the floor with a knife sticking out on her chest.

“We unlocked the garage which was padlocked from outside but she was already dead. We reported the matter to the police and they are investigating,” he whispered, tears streaming down his face. /QUOTE]

Hapa kuna mambo ya kutugusa fikra zetu kidogo. Baada ya kumkosa huko kwingine kote akaamua kuangalia kwenye gereji na wakaona mwili wa marehemu ukiwa na kisu kifuani. Wakafungua hilo lango la gereji (na hivyo kupoteza kwa kiasi kikubwa ushahidi wa nani aliufunga!) na siwezi kushangaa walipofika ndani mmoja wao akakichomoa kile kisu, na hivyo kufuta ushahidi wa nani alikichomeka (I hope thats not the case).

e. The story:

Tunaambiwa kuwa hili halikuwa tukio la ujambazi kwani hakuna kitu cha thamani kilichoibiwa, kuna kitu hawa watu walikuwa wanatafuta au kulikuwa na sababu binafsi ya kufanya tukio hilo zaidi ya kuiba. kama hao jamaa walikuwa wanatafuta fedha na ndani ya nyumba kuna vitu vya thamani why not take the valuables and liquidate them later?

So.. in short ni kuwa it is not what it seems..

Huyu kajamaa kanachambua hii mada kama FBI agent!
 
Mkjj, nasikia FBI wanakutafuta sana. Fanya hima ukawaone :)
 
Inasikitisha sana,neways back to the point on motives,tunajua balozi Daraja anahitaji pesa za kampeni kama ni kweli habari za kugombea ubunge zipo,ila ambalo hatuwezi kujua ni kuhusiana na life insurance,bottomline ni muhimu kupata taarifa kama yuko cleared ama la,nadhani hayo yote labda ni baada ya kipindi cha maombolezo.
 
BaK.. umenichekesha.. ndio tatizo la kukesha everyweekend to watch CSI Miami na Law and Order!!

Teh teh teh...Kweli MKJJ,hata FBI Files pia,especially kama maelezo yangu hapo juu,story huwa zikiingiza matundu kama hivi foul play huwa iko,ila mazingira all the time money is the motive.
Mara ya kwanza kutoka na utamaduni wangu,nilikuwa nikijiuliza hawa wazungu wana kichaa kweli,yani suspect wa kwanza ni mume ambaye kwetu kiutamaduni na yeye ni kama victim?Yalipokuja mambo ya insurance ndiyo nikagundua kuwa life insurance pia si utamaduni wetu,ila in this case kwa mtu ambaye ana previledges hizo, na nyakati hizi za maendeleo,plus more knwoledgable and civil society anything is possible....I am really looking forward for the clearance of Mh Balozi Daraja.
 
Poleni sana fammilia ya Daraja , tulikua wote DC.

Jamani kumbukeni hii ni posh fammily na muda mrefu imishi nje ya TZ , ina wezekana hawana mambo ya kiswahili ya kujuana na majirani na kujazana na ndugu toka vijijini kwenye nyumba moja , ambapo sio jambo la ajabu, so sulala la kutaarifu majirani au kupigia simu ndugu linaweza kuwa sio kitu cha kwanza kufikiria kukifanya.
R.I.P Mama Daraja.
 
kama hilo unalosema ni kweli basi yawezekana hilo linaweza kuwa limewagharimu.. wakati mwingine "uswahili swahili" unaweza kusave watu..
 
Poleni sana fammilia ya Daraja , tulikua wote DC.

Jamani kumbukeni hii ni posh fammily na muda mrefu imishi nje ya TZ , ina wezekana hawana mambo ya kiswahili ya kujuana na majirani na kujazana na ndugu toka vijijini kwenye nyumba moja , ambapo sio jambo la ajabu, so sulala la kutaarifu majirani au kupigia simu ndugu linaweza kuwa sio kitu cha kwanza kufikiria kukifanya.
R.I.P Mama Daraja.

Baalozi Daraja mbona ni mtu approachable sana tu, tena yeye mwenyewe ni mswahili swahili tu.

Tanzania haijawa na class system kiasi cha kusema huyu ni wa posh family, posh families wachache wenyewe kina Mwapachu na Rupia ambao walikuwa influential tangu kabla ya uhuru wanajua kujichanganya na watu.

Hao kina Daraja ndiyo generation ya kanza kwenda shule and all, wameenda shule kwa miguu, bila viatu wengine, huu u posh utoke wapi?

Tusitake kuleta negative assumptions bila ya kuwa na fact. Mimi nilivyomjua balozi Daraja balozi mzima unamsimamisha kwenye corridor mnapiga naye story kama mnajuana, mtu balozi halafu mshua, yule mzee wala si mtu wa kumchunia mtu/ kutojimix eti kwa sababu yeye ni Balozi Daraja.
 
Ni dhana potofu kudhani kujuana na majirani ni uswahili. Mimi na majirani zangu wazungu mbona tunajuana na huwaga tunaalikana kwenye bbq....au hawa wazungu majirani zangu ni waswahili?
 
- I am down balozi Daraja ni mtu wa kujichanganya sana wala hana nyodo mtu clean hana noma, sawa sawa mkuu.

Respect.

FMEs!
 
Mwanakijiji inawezekana story unayoitumia kum-quote Balozi imeandikwa na "kanjanja". Amejikalia ofisini tu na kuweka maneno yake kwenye story nzima. Hata uandishi wenyewe si umeuona? Ni wa ajabu kweli.

Inasikitisha kwa kuwa ndio media house zetu zilivyo. Kwa hiyo kwa maoni yangu matundu mengi ya hii stori yapo kwa mwandishi na wala sio kwa Balozi mwenyewe.
 
Ni dhana potofu kudhani kujuana na majirani ni uswahili. Mimi na majirani zangu wazungu mbona tunajuana na huwaga tunaalikana kwenye bbq....au hawa wazungu majirani zangu ni waswahili?
Mijirani yako ndivyo ilivyo....lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom