Mke wa aliyekuwa Kamanda wa polisi [RPC] Mwanza ashitakiwa kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa aliyekuwa Kamanda wa polisi [RPC] Mwanza ashitakiwa kwa rushwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Jun 9, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hakimu wa mahakama ya mwanzo Ukonga Ndevera Kihengu na wenzake Karani wa mahakama ya Ukonga Evelyne Mowo na karani wa mahesabu Victoria Mtasiwa wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kuomba rushwa ya Tsh 100,000.Bi Ndevera Kihengu ni mke wa aliyekuwa RPC mkoa wa Mwanza Kamanda Eliah Kihengu.

  Bibi Ndevera Kihengu,Evelyne Mowo na Victoria Mtasiwa wote kwa pamoja walimshawishi Joyce Msaki awape rushwa ya Tsh 100,000/= iliwaweze kumpatia dhamana katika kesi inayomkabili mahakamani hapo [Ukonga].tayari hakimu Kihengu alishalamba kiasi cha tsh 40,000/= toka kwa Joyce Msaki.

  Washitakiwa Hakimu kihengu na Victoria wako nje baada ya kukamilisha taratibu za dhamana,Karani Mowo yuko rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Juhudi kubwa zinatakiwa kufanywa hakuna sehemu ambako rushwa imetamalaki kama Mahakamani,Polisi,Magereza,Uhamiaji na huduma za afya.Ukijaribukutia pua huku utashangaa jinsi Tanzania ilivyozama kwenye rushwa hakuna TAKUKURU wala mjomba wa kusaidia kuondoa mdudu rushwa.

  Ni vyema rushwa ikatangazwa kama "JANGA LA KITAIFA" huduma ndani ya maofisi ya serekali hakuna bila kutoa kitu kidogo.
  Nina wasiwasi kesi inayomkabilia Hakimu N Kihengu na wenzake itamalizwa kiutu uzima.
   
 3. l

  lebadudumizi Senior Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama Kihengu aliwahifanyakazi mahakama ya mwanzo Buguruni kabla hajahamishiwa Ukonga kuepusha malalamiko ya wanachi waliodaiwa rushwa bila kificho.Hakimu Kihengu akiringia cheo cha mumewe kabla hajastaafu kwa mujibu wa sheria ukamanda wa polisi Mwanza.TAKUKURU waliwahi kumkamata lakini kesi haikupelekwa mahakamani ikamalizwa nje ya utaratibu rasmi ili kulinda heshima ya Mume wake Kamanda Kihengu.

  Kweli kila jambo na wakati wake niliposikia habari za kukamatwa kwake sikuamini.nimejifunza jambo moja kubwa ukiondoka kwenye system unaondoka na ulinzi.Ndio maana Chenge,Rostam na Lowassa hawataki kuondoka.
   
 4. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hadi TAKUKURU wamo kah!!!!
   
 5. M

  Mwera JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwahakika nchi yetu imefikia pabaya,kwamtindo huu hupati haki mpaka uinunue.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu mama ni dagaa rushwa ya Laki moja tu wanampeleka mahakamani wanao kula mabilioni wanapeta mitaani
   
 7. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ngongo umesema!
  Yaani mimi ninapokumbuka kuwa nina ndugu zangu Polisi na mahakama napta mfadhaiko wa ajabu! Idara hizi kwa Tz zimelaaniwa. I fear for them kwa sababu ipo siku patatokea mabadiliko ya kiutawala na watu watawashukia hawa kama mzigo wa matofali! Ni wachafu, waovu kuliko Yuda Iskariota na ni watumishi wa ibilisi na sio serikali wala umma!
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Baba polisi , mama hakimu .. Rushwa mbele kwa mbele.
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana na hoja yako Mama ni dagaa.Mkuu kumbuka Hakimu alitakiwa kutoa dhamana ikiwa mtuhumiwa alikidhi vigezo vya kupata dhamana hapakuwa na sababu za kumdai rushwa.Mtuhumiwa hakuwa na kesi ya mauaji au uhani ambayo haina dhamani yamkini ni kesi ni hivi vikesi vya dagaa ingekuwa kesi ya vigogo asingepelekwa mahakama ya mwanzo hatujui kukaa kwake rumande aliathirika kiasi gani pengine ana mtoto mdogo anahitaji malezi ya mama,au pengine kukaa kwake rumande kumesababisha kibarua kuota nyasi.

  Mkuu nashukuru Mungu sjawahi kukaa rumande katika maisha yangu lakini nina marafiki,ndugu na jamaa wananipa hadithi na vituko vya magerezani hakika usiombee yakakukuta kuna msongamano wa kufa mtu,chakula,maji na usafi ni baadhi ya mambo utakayokumbana nayo ndani ya magereza ya Tanzania.Magereza mengi yamejengwa enzi za mkoloni wakati huo Tanganyika ilikuwa na idadi ya watu wasiozidi milioni 8 leo tuko milioni 44 sijui unapata picha gani ?.Usiangalie kiasi cha fedha jaribu kutazama athari za watuhumiwa wanazokumbana nazo magerezani.
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Duh huo mchanganyiko utanoga zaidi kama mtoto akiwa mwendesha mashtaka,mjomba afisa uhamiaji,shangazi TAKUKURU,Baba ndogo TRA,Baba mkubwa TISS.
   
 11. M

  Mzee wa Wasa Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kila ninapoona tuhuma za rushwa "ndogo ndogo" nabaki tu kushangaa. Mabilioni ya fedha yanapotea kupitia misamaha ya kodi na wahusika wanaendelea kupeta kila uchao. Serikali hii ya sasa imekumbatia rushwa na wala rushwa kwa kiwango cha kutisha. Mabadiliko yasipotokea haraka nchi yetu itaangamia kabisa. Mungu ibariki Tanzania!
   
 12. l

  lebadudumizi Senior Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga jijini Dar es Salaam, Ndevera Kihangu na wenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kushawishi na kupokea rushwa ya sh 100,000.
  Mbali na Hakimu Kihangu, washitakiwa wengine ni karani wa hakimu huyo, Eveline Mowo na mhasibu wa mahakama hiyo, Victoria Mtasiwa.
  Wakili wa Serikali, Salha Abdallah, mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo, alidai washitakiwa wanakabiliwa na makosa matatu ya kushawishi na kuomba rushwa ya kiasi hicho cha fedha.
  Alidai kosa la kwanza ambalo linamkabili mshitakiwa wa kwanza na wa pili ni kuwa Aprili 24 mwaka huu, katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga washitakiwa hao walimshawishi Joyce Msaki awapatie kiasi hicho cha fedha ili wampatie dhamana katika kesi inayomkabili iliyopo katika mahakama hiyo.
  Wakili Abdallah alidai kuwa kosa la pili ni la kupokea rushwa ya sh 40,000, ambalo linamkabili mshitakiwa wa kwanza na wa pili. Siku hiyo walipokea kiasi hicho cha fedha kama kianzio cha kumpatia dhamana.
  Alidai kosa la tatu ambalo linawakabili washitakiwa wote ni kuwa Mei 27 mwaka huu katika mahakama hiyo, washitakiwa hao walipokea tena sh 60,000 kutoka kwa Msaki.
  Washitakiwa wote walikana mashitaka na washitakiwa wawili ambao ni Hakimu Kihengu na Mhasibu Victoria walipata dhamana baada ya kutimiza masharti huku mshitakiwa Mowo alipelekwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti na kesi hiyo imeharishwa hadi Juni 22, mwaka huu.

  Source: Tanzania daima.

  Kumbe vyomba vya habari vilishainasa.
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2013
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Taarifa za ndani zinadai TAKUKURU wameiondoa kesi dhidi ya Mama Kihengu kwa shinikizo toka kwa kigogo wizara ya utawala bora.
   
 14. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  mkuu hii habari ndio naskia leo huyu mama alikuwa muumini mwenzangu kanisa moja! alikuwa kinara kweli wa kutoa michango kanisani mpaka nilikuwa najiuliza why hakimu wa mwanzo mwenye certificate anafanya hivi au ndio kubarikiwa?
  last time nilikutana nae atown mwaka jana akaniambia amestaafu but mtu mwingine aliniambia kuwa ameshafukuzwa ananificha tu!

   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2013
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu wangu kabla hajakutwa na hii kadhia ya aibu alikuwa kabakiza mwaka mmoja atimize miaka 60 ya kustaafu kwa lazima.

   
 16. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2013
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,288
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Sijui ni kesi gani ya maana hawa PCCB wamewahi kuisimamia kwa ufanisi!
   
 17. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2013
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,156
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Kwa mtazamo wako unaona ameonewa au?
   
 18. Deo Corleone

  Deo Corleone JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2013
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 14,651
  Likes Received: 2,509
  Trophy Points: 280
  WaTZ tushazoea kuibiwa sana kwahyo hyo watu wanaona ndogo. lakini kwa mama aliyetoa hyo laki kwake ni nyng na kinyume cha sheria
   
Loading...