Mke niliyemlipia mahari anataka kuolewa na jamaa mwingine

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,125
1,467
Habari na poleni kwa swaumu kwa wale wenzangu na mimi,Allaah aendelee kutupa nguvu.

Sifa zote njema anastahiki Allaah aliyetukuka Mola mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka siku ya mwisho.

Kama ni kuisoma number nahisi kwangu si number hii ya Tanzania bali ni kwa dunia nyingine

Naomba niende direct kwenye tatizo langu,kuna binti nimezaa naye mtoto mmoja,nimetoa mahari toka mwaka juzi,kwa imani yangu naamini nikishalipa mahari huyo ni mke wangu kisheria, sasa nashaanga binti ananambia anataka kuolewa na mtu mwingine,hivi inawezekana kweli? Vipi mahari yangu?

Wanajukwaa naomba ushauri nifanyeje nipate haki yangu,je naweza kwenda kupinga ndoa yao kanisani kwa kigezo nimemlipia mahari pia nimezaa naye mtoto hivyo ni mke wangu kisheria?
 
Mwache aolewe iyo mahar kama siyo pesa nyingi potezea.Miaka mitatu ni mingi mkuu ulikuwaa unasubiri nini!mimi siku nalipa mahar sitakubali wiki mbili ziishe kabla sijabeba mke.Kwenda kuzuia unaweza zuia ila ukishazuia utamwoa?bado utamwamini? Kifupi uyo anayetaka kumwoa lazima mtashea nae uyo mke.
 
Sheria inatambua cheti cha ndoa either cha kimila, cha dini au cha serekali.
Hamna mahali wanapotambua mahari, mahari inaweza kurudishwa.

Pamoja kuzaa nae na kumlipia mahari ila kwa sasa kubaliana na ukweli tuu hakupendi tena, achana nae, keshapenda mwingine. Hata ukifosi kuharibu ndoa ukaishi nae wewe hatokuwa na mapenzi ya dhat

Kosa ulilofanya ni kuchelewa kufunga nae ndoa kwa muda muafaka
 
Habari na poleni kwa swaumu kwa wale wenzangu na mimi,Allaah aendelee kutupa nguvu.

Sifa zote njema anastahiki Allaah aliyetukuka Mola mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka siku ya mwisho.

Kama ni kuisoma number nahisi kwangu si number hii ya Tanzania bali ni kwa dunia nyingine

Naomba niende direct kwenye tatizo langu,kuna binti nimezaa naye mtoto mmoja,nimetoa mahari toka mwaka juzi,kwa imani yangu naamini nikishalipa mahari huyo ni mke wangu kisheria, sasa nashaanga binti ananambia anataka kuolewa na mtu mwingine,hivi inawezekana kweli? Vipi mahari yangu?

Wanajukwaa naomba ushauri nifanyeje nipate haki yangu,je naweza kwenda kupinga ndoa yao kanisani kwa kigezo nimemlipia mahari pia nimezaa naye mtoto hivyo ni mke wangu kisheria?
Kutokana na jinsi ulivyoanza uzi wako, ni wazi wewe ni Muislamu.

Na katika Uislam, mwanamke huitwa mke baada ya ndoa na wala si baada ya kulipa mahari.

Kwa minajili hiyo, ulipaswa kusema kuwa "nimekataliwa na mchumba". Na si kosa kwa mchumba kubatilisha uamuzi.

Na kwa mujibu wa Uislam, huyo mtoto mliyemzaa nje ya ndoa, kisheria si mwanao bali ni mtoto wa huyo mwanamke.
 
kama kaamua hivo let her go
usihangaike sana kama haikua ridhiki yako ,itakuja ya kwako
kuwazuia na kupinga ni kujiongezea stress tu!

mwache akaolewe,akajifunze maisha ,dizaini kama anaenda mafunzoni
akishajifunza maisha akirudi mpokee
na wewe pia utakua likizo haijalishi miaka mingapi..
akirudi mpokee ,atakua na adabu njema kabisa..

waache waoane kwa amani na wewe ishi kwa amani..
akirudi mpokee kwa amani
mweke ndani kwa amani!!!
Mwenyezi Mungu atakuzidishia.
 
Habari na poleni kwa swaumu kwa wale wenzangu na mimi,Allaah aendelee kutupa nguvu.

Sifa zote njema anastahiki Allaah aliyetukuka Mola mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka siku ya mwisho.

Kama ni kuisoma number nahisi kwangu si number hii ya Tanzania bali ni kwa dunia nyingine

Naomba niende direct kwenye tatizo langu,kuna binti nimezaa naye mtoto mmoja,nimetoa mahari toka mwaka juzi,kwa imani yangu naamini nikishalipa mahari huyo ni mke wangu kisheria, sasa nashaanga binti ananambia anataka kuolewa na mtu mwingine,hivi inawezekana kweli? Vipi mahari yangu?

Wanajukwaa naomba ushauri nifanyeje nipate haki yangu,je naweza kwenda kupinga ndoa yao kanisani kwa kigezo nimemlipia mahari pia nimezaa naye mtoto hivyo ni mke wangu kisheria?

kupinga ndoa haitakuwa solution ya yeye kuyalejesha mapenzi yake kwako,cha msingi angalia ustaarabu mpya,kuhusu mahali usijari achana nayo ilimradi umezaa naye,watu wanapoteza vingapi ndngu yangu
 
Hakua Wako mwache aende..usiforce mapenzi utaishi maisha ya majuto milele
 
kama kaamua hivo let her go
usihangaike sana kama haikua ridhiki yako ,itakuja ya kwako
kuwazuia na kupinga ni kujiongezea stress tu!

mwache akaolewe,akajifunze maisha ,dizaini kama anaenda mafunzoni
akishajifunza maisha akirudi mpokee
na wewe pia utakua likizo haijalishi miaka mingapi..
akirudi mpokee ,atakua na adabu njema kabisa..

waache waoane kwa amani na wewe ishi kwa amani..
akirudi mpokee kwa amani
mweke ndani kwa amani!!!
Mwenyezi Mungu atakuzidishia.
Ora bwana, kwa hio amuache aolewe na ndoa ikimshinda arudi kwa jamaa sio?
 
Sasa hapo ww unajitafutia matatizo bure maana utamforce huyo mwanamke ubaki naye na wakati ukweli ni hakupendi tena tayari ameshampenda mwanaume mwingine so mahari isikufanye uje kosa amani ndani yanyumba yako.
 
Kuna jamaa alikua afunge ndoa mwezi uliopita, walishavalishana na pete ya uchumba mwaka huu tena kanisani ila kabla ya ndoa jamaa kashtuka binti ni mjamzito na hawakuwahi kushirikiana kimwili.

Haya mambo yapo mkuu.
 
kama kaamua hivo let her go
usihangaike sana kama haikua ridhiki yako ,itakuja ya kwako
kuwazuia na kupinga ni kujiongezea stress tu!

mwache akaolewe,akajifunze maisha ,dizaini kama anaenda mafunzoni
akishajifunza maisha akirudi mpokee
na wewe pia utakua likizo haijalishi miaka mingapi..
akirudi mpokee ,atakua na adabu njema kabisa..

waache waoane kwa amani na wewe ishi kwa amani..
akirudi mpokee kwa amani
mweke ndani kwa amani!!!
Mwenyezi Mungu atakuzidishia.
Mungu hawezi kumzidishia kwa kumpokea Huyo .....naamini hvyo.
 
ndio maana unashauriwa wakati unafanya taratibu za ndoa lazima uwe na super sub tena ya maana ngoma ikipindua unaamia upande wa pili.....na katika uhalisia mke mmoja hatoshi 100%
 
Kama ulilipa mahari bila kupewa risiti imekula kwako...tafuta mwingine na uhakikishe umedai risiti!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom