Mke ni nani kwa sheria ya ndoa ya tanzania


Gamaha

Gamaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2008
Messages
2,842
Likes
1,023
Points
280
Gamaha

Gamaha

JF-Expert Member
Joined Jul 17, 2008
2,842 1,023 280
Helo ndugu Great Thinkers naomba mnijuze unaposema mke katika sheria ya ndoa tanzania ni yupi anayetambulikana, je ukizaa na mtu na ukakaa naye bila kufunga ndoa sheria itamtambua kuwa ni mke wako, na je unapotaka kudai talaka kwa huyu ambaye hukufunga naye ndoa inakubalika kwenda mahakamani.
 
M-bongotz

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
1,734
Likes
44
Points
145
M-bongotz

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
1,734 44 145
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania..Act No. 5 of 1971 [CAP 29 RE:2002]

Kifungu cha 9 cha sheria hii kimeifafanua ndoa kama ifuatavyo.
Meaning of marriage
(1) Marriage means the voluntary union of a man and a woman, intended to last for their joint lives.
(2) A monogamous marriage is a union between one man and one woman to the exclusion of all others.
(3) A polygamous marriage is a union in which the husband may, during the subsistence of the marriage, be married to or marry another woman or women.
Unapozungumzia mke katika ndoa ni yule ambaye mmefunga naye ndoa halali kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania.

Mtu ambaye umezaa naye tu bila kufunga ndoa huyo si mkeo bali ni hawara (concubine), kuzaa nae hakufanyi uhusiano wenu kuwa na hadhi ya ndoa, hivyo ukitaka mtambulike kama wanandoa ni lazima mfuate taratibu za kufunga ndoa kama sheria inavyotaka.

Talaka inatolewa na mahakama kwa wale ambao ni wanandoa halali tu (wenye cheti cha ndoa) lakini hata hivyo kifungu cha 160(1) cha sheria hii kinasema hivi;

Presumption of marriage
(1) Where it is proved that a man and woman have lived together for two years or more, in such circumstances as to have acquired the reputation of being husband and wife, there shall be a rebuttable presumption that they were duly married.
Kwa kutumia kifungu hiki basi, kama mmeishi chini ya paa moja kwa muda wa miaka miwili au zaidi na jamii inayowazunguka imekuwa ikiwatambua nyie kama wanandoa mahakama inaweza kuleta dhana ya ndoa kati yenu, lakini hii haitosaidia kupata talaka isipokuwa tu kama kuna chochote unachostahili kutokana na kuishi kwenu pamoja muda wote huo dhana hii inaweza kukusaidia kupata haki yako.
 
Gamaha

Gamaha

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2008
Messages
2,842
Likes
1,023
Points
280
Gamaha

Gamaha

JF-Expert Member
Joined Jul 17, 2008
2,842 1,023 280
Thanks mkuu umenifafanulia vizuri sana na nimeelewa
 
bht

bht

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
10,335
Likes
212
Points
160
bht

bht

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
10,335 212 160
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania..Act No. 5 of 1971 [CAP 29 RE:2002]

Kifungu cha 9 cha sheria hii kimeifafanua ndoa kama ifuatavyo.


Unapozungumzia mke katika ndoa ni yule ambaye mmefunga naye ndoa halali kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania.

Mtu ambaye umezaa naye tu bila kufunga ndoa huyo si mkeo bali ni hawara (concubine), kuzaa nae hakufanyi uhusiano wenu kuwa na hadhi ya ndoa, hivyo ukitaka mtambulike kama wanandoa ni lazima mfuate taratibu za kufunga ndoa kama sheria inavyotaka.

Talaka inatolewa na mahakama kwa wale ambao ni wanandoa halali tu (wenye cheti cha ndoa) lakini hata hivyo kifungu cha 160(1) cha sheria hii kinasema hivi;Kwa kutumia kifungu hiki basi, kama mmeishi chini ya paa moja kwa muda wa miaka miwili au zaidi na jamii inayowazunguka imekuwa ikiwatambua nyie kama wanandoa mahakama inaweza kuleta dhana ya ndoa kati yenu, lakini hii haitosaidia kupata talaka isipokuwa tu kama kuna chochote unachostahili kutokana na kuishi kwenu pamoja muda wote huo dhana hii inaweza kukusaidia kupata haki yako.
well said learned bro/sis
 

Forum statistics

Threads 1,237,163
Members 475,462
Posts 29,279,931