Je, ni sahihi mpenzi wako kufahamu kipato chako unachokipata?

Vipato vijulikane kwa wote ili muweze kufanya maendeleo, hata kama pia hafanyi kazi mkeo mwambie kila kitu
 
Vipato vijulikane kwa wote ili muweze kufanya maendeleo, hata kama pia hafanyi kazi mkeo mwambie kila kitu

Shantel,ili suala tushalijadili sana humu mmu, siku zote kuhusu suala hili mimi huwa natoa tahadhari sana,ndoa ndoana mnapokuwa kwenye lindi la mapenzi sawa mnaweza peana siri zote hata za hela lakini penzi likichacha mmoja anaweza kulipa kisasi kwa kuvujisha siri za mwenza na mwenza akaishia lupango,ni tahadhari tu tokana na uzoefu wangu wa maisha maana nimeyaona na wala sio kusimuliwa.
 
bora niambiwe ntakuwa sipress plafoma nyingi ila NIKIFICHWA ahh ntajua zipo tu so ntasend plafoma mpk atajiuliza i nini

bt nkiambiwa/nikiusishwa ntahisi m part of t so ntatunza na statapanya...nikifichwa ntakomoa daily chumzi hakuna ,faigio limeisha,.... chup IMETATUKA..
 
bora niambiwe ntakuwa sipress plafoma nyingi ila NIKIFICHWA ahh ntajua zipo tu so ntasend plafoma mpk atajiuliza i nini

bt nkiambiwa/nikiusishwa ntahisi m part of t so ntatunza na statapanya...nikifichwa ntakomoa daily chumzi hakuna ,faigio limeisha,.... chup IMETATUKA..

Rose bana.......halafu utundu wako huu nshakwambia ntakuchapa!
 
Sio vipato vyote vya kushea. Ni vyema mkashea vipato vile vya msingi kama mashahara na fedha ya miradi mbalimbali lakini zinazopatikana kwenye kona zisizo rasmi ni hatari kumshirikisha mwenzi wako. Kaa na fedha yako itakusaidieni kwenye dharura fulani fulani. Hujawahi sikia kauli kama hizi " Mama nanii hebu angaliangali kwenye akiba zao labda utapat hata buku" au "Baba nanii nenda wewe ni mwanaume Bwan hebu jitahidi, au onyesha uwezi wako bwana" Sasa hapo ndo pa kutumia hako ka fedha ambako yeye hakajui.
 
sidhani kama salary slip ukawa unampa kabisa ila ndugu pesa ya mishe mishe hatakiwi kujua
 
Maisha yanabadilika na binadamu wanakuwa na roho mbaya sana ya kutaka kutawala Mali na umiliki pia huwa nafika mahali naogopa sana mwanamke yaani kumwamini kwenye suala la Mali hivi Kuna umuhimu mke au girlfriend kujua mshahara wako au kipato unachoingiza au miradi unayomiliki? daa huwa naogopa sana navyoona wanawake wanaua waume zao afu wamiliki Mali au mwanaume unahangaika ala izo izo ela mwanamke anaenda mhonga mwanaume mwenzio tena unakuta fala tuu daa....
 
maisha yanabadilika na binadam wanakua na roho mbaya sana ya kutaka kutawala Mali na umiliki pia huwa nafika mahali naogopa sana mwanamke yaani kumwamin kwenye suala la Mali hivi Kuna umuhimu mke au girlfriend kujua mshahara wako au kipato unachoingiza au miradi unayomiliki? daa huwa naogopa sana navyoona wanawake wanaua waume zao afu wamiliki Mali au mwanaume unahangaika ala izo izo ela mwanamke anaenda mhonga mwanaume mwenzio tena unakuta fala tuu daa....


Mimi ni mwanamke, binafsi sitaona ulazima wa kufahamu mshara wako ama kipato chako ikiwa unajitambua na kujiongeza kuhuduma na badala yake nitakuwa na kazi ya ziada ya kukuombea mungu ufanikiwe zaidi ili tuneemeke. Lakini pia somehow kuna umuhimu maana kuna kuugua,umauti ni vyema mwenzi wako akajua mali zako (hapa namuongelea mke wa ndoa ikiwa hujahususha ndg wala wazazi wako,kwani ikiwa ndg na jamaa zako wanajua basi na mara nyingi ukiona mtu mali zake zinajulikana kwao kuliko kwa mkewe ujue huyo mwanamke ana walakini. Nadhani mara nyingi umsome mwenzi wako kwanza umjue ndio umshirikishe sio kwa nyie wanaume tu hata sisi wanawake maana wapo wanawake wenye uwezo kifedha na wanaishi na wenzi wao wasio na uwezo kifedha nao pia ni wa kuwaangalia wasije kuwageuka na mara nyingi ili yasikufike hayo madhara ni vyema ukajiongeza mwenyewe kwa kila wajibu unaokuhusu ili kuleta amani ndani na kuepusha tamaa ambazo hazikupangwa, Huu ni mtazamo wangu mimi lkn inategemea maana nafsi zinatofautiana sana na imani imekuwa haba.
 
Katika vitu nilivyo wahi kuambiwa na mzee wang icho kilikua chakwanza kabisa ni mwiko mwanamke kujua michakato yako ya ela kikubwa mtimizie maitaji yake muhim yote then unaweza mfungulia biashara ambae anaimiliki yy mwenyewe si kuajiliwa MARUFUKU!!
Tawile mkuu,habari za masiku,wewe ni mume bora baba wajibika sihitaji kujua kupato chako hudumia familia.
 
Hamna formula maalumu kwa kila mtu na inategemea mmekutana wapi, kwa mazingira gani, mnaaminiana kiasi gani, imani yenu kwa Mungu ipoje na malengo yenu ya pamoja yakoje. Mimi ni muumini wa ndoa iliyo na uwazi , mnapanga, mnajua vipato vyenu, matumizi, malengo, miradi , nk nk
Binafsi sioni shida wanandoa kuambiana vipato vyao na wapange pamoja mipango yao. Unaficha ili iweje? Unalalaje na mtu na kuishi naye ukijua kila moja ana siri nzito ?
Kama ndoa i thabiti basi mume na mke wote wanahitajika kupanga pamoja na kila mtu kukubali kuwa mwenzake ana private needs (ndugu, salon, nk , nk). Ni maelewano tu, mimi nipo kwenye ndoa over 10 years tumekuwa tukipanga pamoja na Mungu ametubariki kwa njia hii. Kila mtu anajua kipato cha mwenzake . Hakuna mmoja wetu anayewaza mimi bora kuliko mwingine na kwakuwa mwenzangu ana hela nyingi basi madai yasiyokuwa na msingi yaanze . Ila ni maoni tu, wengine kwa experience zao wanaweza ona huu ni ushamba.
 
Back
Top Bottom