Mke/mume uliyenaye ndiye wa ndoto zako?

Kwani hizi kazi tunazofanya ndio kazi za ndoto zetu?kiukweli ni watu wachache sana wanaishi kwenye ndoto zao humu duniani,life is just living and worshiping God my friend,hivyo vingine ni ziada tu
Tunapata grade ambazo hatutaki,tunaenda college ambazo hatutaki,kwa sababu ya ambazo hatutakia unakuja kupata kazi ambayo utaki unaoa mke ambae utaki alfu unazaa watoto ambao hamtaki alfu uku unaishi nyumba ambayo utaki mbaya zaidi unakuja kuzeeka vile wee utaki an case closed

 
Hahaha mimi kuna binti 1 anaitwa peary Daahh kitambo enzi za ujana alifanikiwaga sana kuzinyanyasa kuta za moyo wangu bwana weeee nilikuwa sili silali mindset yangu yote ikawa ameiteka yeye " Daahh mpaka leo huwa ninakiri kwamba sijawahi kupenda mwanamke kama jinsi ambavyo nimewahi kumpenda Yule binti
Pearl Chelelute huyu huyu wa JAMBO FORUMS? Nakuja inbwobwuongo nikupe simulizi ya mwenzie Suzie yaani Ni noma
 
Kumpata wa ndoto hakuna hata kidgo
Sema tunawapata wale tulioamua kuwavumilia na wao kutuvumilia basi ili maisha yaende

Maana wa ndoto wako ni yule ambae hana kasoro wala pungufu kila sector yupo sawa jee ukimpata na yeye je wandoto wake unamjua!!?

Swali la kujiuliza
Unaweza jua ndoto ya mwenzako!?
Mimi nashukuru Mungu mwanamke niliyenaye niwandoto yangu nimetumia muda mrefu kumsaka mpaka nikamtia mikononi na ndoa tumefunga na kunizalia watoto wawili nampenda sana mke wangu na ninajisikia raha sana ninapomwona kwa kuwa tumetoka mbali Mimi na yeye mpaka sasa ninaye na ni furaha ya moyo wangu.
 
Hebu sema ukweli wa moyoni mwako. Hayo mahusiano ulionayo ndiyo ulikuwa ukitamani kuwa nayo ama unasogeza siku?

Juzi kati tulikuwa watu watatu. Wanaume wawili na mwanamke mmoja. Baada ya kuongea sana mwisho wa siku tukaja kuulizana swali hili.

Ikaja kugundulika kuwa wote hatujapata watu sahihi wa ndoto zetu.

Swali kwako.

Je, umebahatika kumpata wa ndoto yako ama unasubiri subiri...
Halafu na wewe unauliza maswali kama ya KIPIMA JOTO ITV.

Jibu hapo si lipo wazi kabisa.......
 
Mawazo yako ni mawazo yangu, nilichokipata kimekuwa zaidi hata ya kile cha ndoto yangu, namshukuru Mungu sana alichonipatia pia tulipotoka na tulipo sasa ana mchango mkubwa sanaaaaaaa kimwili, kiuchumi na kiakili.
Mke niliye naye si wa ndoto yangu ila ni mke aliyenipa Mungu na Malaika wake pia sijutii kuwa naye kwani ni zaidi ya yule niliyekuwa namtaka (my dream woman). Bila huyu mwanamke niliye naye sijuwi ningekuwa wapi, kwangu ni Mama yangu, Baba, best friend, msiri wangu mkubwa, yaani ni mambo yote kwangu.
 
Back
Top Bottom