Mimi nime kaa na mke kwa miaka kumi na nne sasa na tuna watoto wanne, lakini mwanzoni mwa mwaka huu mke alitoroka nyumbani na kwenda kwao na kukaa huko kwa miezi saba hivi, lakini aliporejea nilibaini kuwa ana uja mzito wa kama miezi mitano lakini kwa sasa amejifungua na imethibitika kuwa si mtoto wangu, uamuzi wangu ni kumtaliki hivyo naomba msaada kama niki mtaliki atakuwa na haki zozote juu ya mali yangu maana kwa sasa nina hali mbaya ki uchumi na nina miliki nyumba moja tu na ndiyo inayo tuhifadhi na watoto