Mke kuzaa nje ya ndoa

Surabaya

Member
Nov 25, 2011
14
0
Mimi nime kaa na mke kwa miaka kumi na nne sasa na tuna watoto wanne, lakini mwanzoni mwa mwaka huu mke alitoroka nyumbani na kwenda kwao na kukaa huko kwa miezi saba hivi, lakini aliporejea nilibaini kuwa ana uja mzito wa kama miezi mitano lakini kwa sasa amejifungua na imethibitika kuwa si mtoto wangu, uamuzi wangu ni kumtaliki hivyo naomba msaada kama niki mtaliki atakuwa na haki zozote juu ya mali yangu maana kwa sasa nina hali mbaya ki uchumi na nina miliki nyumba moja tu na ndiyo inayo tuhifadhi na watoto
 
Mtimue, na hao uliodhani umezaa naye kawapime DNA, unaweza ukakuta mtoto wako ni mmoja tu hapo.
 
ukiomba talaka ukapewa, mlivyochuma pamoja lazima mgawane kaka. sheria haingalii nani mkosaji.
(nakutumia invoice kwa malipo ya ushauri, ushistuke)
 
Kwetu sisi tunaoamini biblia inasema, mke hataachwa bali kwa uzinzi. Kuzaa nje ya ndoa ni uzinzi. Weka mbali na tembo huyo mwanamke!
 
Mimi nime kaa na mke kwa miaka kumi na nne sasa na tuna watoto wanne, lakini mwanzoni mwa mwaka huu mke alitoroka nyumbani na kwenda kwao na kukaa huko kwa miezi saba hivi, lakini aliporejea nilibaini kuwa ana uja mzito wa kama miezi mitano lakini kwa sasa amejifungua na imethibitika kuwa si mtoto wangu, uamuzi wangu ni kumtaliki hivyo naomba msaada kama niki mtaliki atakuwa na haki zozote juu ya mali yangu maana kwa sasa nina hali mbaya ki uchumi na nina miliki nyumba moja tu na ndiyo inayo tuhifadhi na watoto

Pole ndugu kwa mkasa mkubwa uliokukuta.. Kipi kilimfanya mkeo akimbie miezi yote hiyo kwao. Pili je mmekuwa na ugomvi wowote hapo kabla, swala lako lazima lianzie kwenye baraza la usuluhishi kabla ya kwend mahakamani ili upate cheti cha ndoa yako kuvunjika, na vitakavyo ithibitishia mahakama kuwa talaka inafaa ni uhusiano wenu hapo kabla maana kuwa na mtoto tuu wa nje si kigezo cha TALAKA..ukifanikiwa kumtaliki nyumba yaweza kuwa ya familia ambayo weye unaweza kuamrishwa umpishe mkeo kama watoto ni wadogo sana lakini kama ni wakubwa unaweza kupewa nyumba kulinda watoto na kuomwa kumlipa mkeo japo kifuta jasho..

pole sana...
 
Nia yako ni nini? Kama kumtaliki fanya hivyo kama sivyo usimtaliki maana ukiwa na nia ya kumtaliki na unasita sababu ya nyumba au mali basi mtaishi ila hamtakuwa na a$ani kabisa!!! Kama linavumilika na historia inaonesha hakuwa na tabia mbaya msamehe muendelee yeye ni binadamu, ila kama mlipishana kidogo akakimbilia kwao akarudi na mimba anaweza kufanya.na mengine mengi huko baadaye.
 
Pole ndugu kwa mkasa mkubwa uliokukuta.. Kipi kilimfanya mkeo akimbie miezi yote hiyo kwao. Pili je mmekuwa na ugomvi wowote hapo kabla, swala lako lazima lianzie kwenye baraza la usuluhishi kabla ya kwend mahakamani ili upate cheti cha ndoa yako kuvunjika, na vitakavyo ithibitishia mahakama kuwa talaka inafaa ni uhusiano wenu hapo kabla maana kuwa na mtoto tuu wa nje si kigezo cha TALAKA..ukifanikiwa kumtaliki nyumba yaweza kuwa ya familia ambayo weye unaweza kuamrishwa umpishe mkeo.
Ahsante kwa maoni yako lakini hiyo ni sawa na kuhalalisha uzinzi, sasa kigezo gani kina weza tumika kuhalalisha uzinzi na kupendekeza mume ndiye atoke kwenye nyumba na wakati aliye kosea ni mke.
 
Mpe taraka huyo. Ukiakaa nae huwezi kuishi salama klmawazo mpaka unaingia kaburini.
 
Ngoja nimuulize lawyer wangu EMT atupe vifungu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nime kaa na mke kwa miaka kumi na nne sasa na tuna watoto wanne, lakini mwanzoni mwa mwaka huu mke alitoroka nyumbani na kwenda kwao na kukaa huko kwa miezi saba hivi, lakini aliporejea nilibaini kuwa ana uja mzito wa kama miezi mitano lakini kwa sasa amejifungua na imethibitika kuwa si mtoto wangu, uamuzi wangu ni kumtaliki hivyo naomba msaada kama niki mtaliki atakuwa na haki zozote juu ya mali yangu maana kwa sasa nina hali mbaya ki uchumi na nina miliki nyumba moja tu na ndiyo inayo tuhifadhi na watoto

Taliki fasta!!! Huyo umemrudisha wa nini? Miezi miwili tu ashashika mimba? Hujawahi safiri miezi miwili wewe? Kama umewahi basi watoto wengine sio wako hapo!!!
 
Mimi nime kaa na mke kwa miaka kumi na nne sasa na tuna watoto wanne, lakini mwanzoni mwa mwaka huu mke alitoroka nyumbani na kwenda kwao na kukaa huko kwa miezi saba hivi, lakini aliporejea nilibaini kuwa ana uja mzito wa kama miezi mitano lakini kwa sasa amejifungua na imethibitika kuwa si mtoto wangu, uamuzi wangu ni kumtaliki hivyo naomba msaada kama niki mtaliki atakuwa na haki zozote juu ya mali yangu maana kwa sasa nina hali mbaya ki uchumi na nina miliki nyumba moja tu na ndiyo inayo tuhifadhi na watoto
ndugu divorce haipatikani tu kirahisi..bongo..may be separation nayo ni kwa mbinde sana..kama vipi vumilia tu afu unamsamehe...tu..haya maisha..tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom