Mke kuwafukuza ndugu wa mme ni halali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke kuwafukuza ndugu wa mme ni halali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NGUGO, May 3, 2012.

 1. NGUGO

  NGUGO Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je! Mke kuwafukuza nyumbani ndugu wa mme wake wakati huo anakaribisha ndugu zake ni halali? Dawa yake ni nini?
   
 2. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  hivi news alert na swali ni kitu kimoja?
   
 3. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,321
  Trophy Points: 280
  Kwa nin kawafukuza na kwa nin ameleta ndugu zake hebu fafanua vizuri epuka KUKURUPUKA ndugu.
   
 4. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio sahihi! Dawa ni moja. Kaeni chini muandike katiba mpya ya familia!
   
 5. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ni wazi kuwa tabia hiyo sio nzuri na haipendezi, mwanamke anapaswa kupenda ndugu wa mume wake kama anavyowapenda ndugu zake kwani kwa kuolewa huko yy amekuwa mmoja wa wanafamilia, kama mkeo au hata mume hapendi ndugu wa mwenzi wake ni vizur hueleweshana kwa busara kama haelewi sogea hata kwa mshenga na ikibd kwa viongoz wa dn na hata wazaz. Ila kwenye mahusiano ni vizur zaid mkajitahd kusolve matatzo yenu wenyewe msipende sana yatoke nje, fannya hvyo inaposhindikana kabisa.
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  haifai,na huo ni ubinafsi
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu labda nikusaidie kuweka wazi maana mambo haya si mageni katika jamii yetu.

  Kuna baadhi ya wanawake huwa hawapendi ndugu za wanaume kwa vigezo chungu mbovu.

  Kwa mantiki hiyo ndugu wa mume wakija hawachuki round ni lazima warudi kijijini walikotoka.

  Wakati huo huo ndugu wa mwanamke wakija wanakaa bila manyanyaso au lawama mara hiki leo au kesho kile.

  Suluhisho.

  Kaeni na mke wako mjadiliane ni kwa nini ndugu zako anataka warudi nyumbani na wa kwake wanakaa. Najua atasingizia ndugu zako ni wakorofi.

  Sasa ili kukata mzizi wa fifna inabidi mwanaume utoe maamuzi magumu ya kutotaka ndugu wa aina yoyote pale nyumbani kwako awe wa kike au kiumeni.

  Misaada yote itafikia huko waliko. Hapi utakuwa umesolve tatizo lakini linahitaji uwe rijali na siyo mume mbwege.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Akimwaga mboga wewe mwaga ugali, maji ya kunawa na maji ya kunywa. Na wewe embu jaribu kufukuza wakwake aone raha yake. . .mbaya kweli huyo mkeo.
   
 9. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Kama hao ndugu wa mwanaume wanamsema, au kumsimanga au kumtenga kiaina na yeye anafeel basi labda inaweza kuwa ni sabau, haya huwa yanatokea sana.

  cha muhimu ni mumewe kumkalisha chini na kumuuliza sababu, wengi huwa wanarukia kujaji bila kujua nini kilichomo ndani ya uhusiano wa ndugu hao. nimeshaona hii inatokea sana, na kuna moja ndugu wa mwanaume walikuwa tu hawampendi mke wa ndugu yao basi alikuwa hana raha kabisa. mume akawa amsikilizi kilio chake cha rohoni, ilipita miaka kabla hajagundua kujua mkewe alikuwa hana kosa as walikuwa wanamsingizia mambo mengine. Hata sie wa nje ya ndoa tulikuwa tukiona uhusiano wa ndugu hao na mke ndani ya nyumba na maongezi yao duh.

  so akalishwe chini aulizwe kuna nini, na hapo watafute kusahihisha. ila duh nasikia huwa ngumu, yaani mamabo hawawezi kurudi kama mwanzo hata iweje.
   
 10. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huu utamaduni mbona ni suala la kawaida kwa baadhi ya makabila yanayotumia mabinti zao kama vitega uchumi au chuma ulete. Kuna makabila mawili maarufu sitayataja kwa kuhofia kuchafua hewa. Huo ndiyo mchezo wao. Akiolewa tena anakuja maskini anaanza kudai utajiri mara mama au wazazi wanataka hiki. Simu toka kwao haziishi. Wanawake wa namna hii dawa yao ni kibuti ili kama anawapenda sana ndugu zake huku akichukia wa mumewe basi akaishi na hao ndugu zake. Mapenzi hasa ya ndoa ni pande mbili.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  kwa mie ambaye tumeishi na ndugu toka utotoni, najua challange zao, ndugu wa mume na wa mke hawapaswi kuishi nao. Tuma msaada huko aliko. Ikishindikana ikabidi kuishi nae ajue sheria, kanuni na taratibu za nyujba yenu....na ajue akizivunja atarudi kwao.

  Nikirudi kwenye mada yako, baadhi ya ndugu wa mume kuishi nao ni kazi sana, unakuta kwa sababu tu nyumba ni ya kaka yake wanafikiri wamemuoa na huyo mke, wanasahau nyumba ni baba na mama na mama ndo msimamizi wa mambo pale nyumbani.

  Sasa kuishi na mtu asiyefuata taratibu zenu, atakapokosea mke lazima aseme hapo ndipo chuki huibuka, mwingine hata kazi hashiriki atayakalisha atake kutengewe hadi maji ya kunawa nani anataka shida hizi?

  Baadhi yao umbea, na majungu kutwa kuchonga maneno au kuoeleka maneno ya uongo kwa wakwe kuwa mke hivi mke vile nani anataka shida hizi?

  Bahati mbaya ndugu wa mume anapokosea hawataki kuambuwa, hii nayo huleta vurugu, haiwezekani mke apelekwe kwenye nyumba yake.....

  Na wanaume mna tatizo la kutotatua matatizo ya ndugu zenu, mnajifanya kama hamuyaoni, mkiyaona mnamwambia mke avumilie mkeo ana moyo wa chuma?

  Nikija kwa ndugu wa mke, mke ni rahisi kudhibiti nduguzake, na ndugu ni wasikivu kwa mume maan hawatzki kuharibu, ndo maana huwa rahisi kuishi nao.

  Nasisituza kama hakuna umuhimu wa kuishi na ndugu wa upande wowote heri muishi wenyewe, pelekeni msaada huko waliko... Maana kaka zetu ndugu zenu wengine wanataka kushindana na mke ndani, mke akipata wax watataka na ndg yao awanunulie wax la sivyo midomo juu.....
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mimi hapo nitawatetea wanawake kidogo..inabidi ujiulize kwanini hapendi ndg zako...hivi unajua mke ni rahisi kunyanyaswa au kuchukiwa na ndugu za mume wake kuliko mwanaume kunyanyaswa au kuchukiwa na ndugu za mke wake?.. Kuna mawifi, mama mkwe shangazi na ndugu za mume ambao ni wakorofi sana...so muulize kwanini hawapendi kama kuna ugomvi kati yao basi utafute solution. Hamna kitu kizuri kama kukaa na mke wako pamoja na ndugu zenu wote pamoja...its such a good feeling :love:
   
 13. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Wewe ulivyomuuliza mkeo amekupa sababu gani?from there ndo naweza kusema kitu..
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani mimi mama gaude afanye hivi nikipata taarifa tu yaani nampa talaka kwenye skype na mahari yangu wanirudishie kwa MPESA...yaani haiwezekani afanye hivo hata kidogo....bora nikae bila mke niwe nagonga kazi za nje tu kuliko kuruhusu the so called wife awafukuze ndugu zangu....
   
 15. The Inquisitive

  The Inquisitive Senior Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Umeongea vizuri sana
   
 16. lolyz

  lolyz JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwanini mkae na ndugu?kwani hata kama kaka kajenga ndio muhamie?hamna kwenu? lazima tufike mahali tubadilike utakuta ndugu wa mume kaja kusalimia kakaa wiki ya kwanza ya pili hata kusuuza kijiko alicholia hawezi kisa kuna house girl c'mon kwani huyo dada nilikuwekea wewe wifi? wengi wao wanaboa hata inafikia kukufukuzia mdada wako wa kazi,mwingine wif anaumwa tumbo la mwezini mbio kwa kaka ake kwanini usiniambie mimi mwanamke mwenzio? ni vitu vidogo vinavyofanya mawifi na wake za kaka zao washindwe kuelewana.

  Mwanaume toa msimamo ukija kuambiwa kitu kama hicho unashindwa nini kumrudisha kwa mkeo?ukimuuliza kwanini mtoto wa kike akueleze wewe mwanaume vitu hivyo anakujibu eti ooh sababu mm kanizoea??hainiingii akilini..

  Ndugu wa mume heshimuni nyumba za watoto /kaka zenu na sio mnajiendea tuu bila utaratibu haipendezi lazima kuwe na sababu maalum na ukifika pale funga mdomo wako.
   
 17. m

  mtotopendwa Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Jamani kuishi na ndugu wa mume ni jaribu kubwa kuliko kujitwisha gunia la misumari. Mimi ninaishi na wifi alieachika kwa mume na ameshakaa zaidi ya miezi sita sasa.
  Hasaidii kazi yoyote hapo ndani,anarudi mda anaotaka cku nyingine mpaka saa tano ucku,mkipika chakula asichokipenda hali na mengineyo mengi. Nimeongea na kaka yake mara kadhaa amuonye ndugu yake anajibu ameshaongea nae and lets hope for the best. Sioni mabadiliko yani naudhika mpaka nataka niondoke mimi niwaache wanafamilia wafaidi undugu wao.
  Kwa kweli sishauri wanandoa kukaa na upande wowote wa ndugu.
   
 18. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  kali zaidi ni kukaa na shemeji wa kiume ambaye ni mtu mzima , na milango ya bedrooms kwa bahati mbaya inafuatana, mwanaume unakuwa huna freedom/privacy utafikiri unakaa ukweni!
   
 19. NGUGO

  NGUGO Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ushauri wenu,lakini, kama hashauliki iweje? Maana anasema kila mtu na kwake wakati ndugu zake huja, ukimuuliza anasema wafukuze na wewe, hata ukisema ukitoka ukarudi unawakuta?
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mi sijawahi kuishi na ndugu wa mume wala wa me (ndugu zangu) kwa kuwa hakuna aliyekuwa na shida ya kuishi kwangu lakini najua saaana mtihani wanaoupata wanawake wenzangu wa kuishi na ndugu wa mume. Tena leo nimetoka kupiga story na dada mmoja anatokea mkoa maarufu kwa mawifi wakorofi na yeye ni wa huko huko lakini anasema na ulokole wake alinawa mikono siku moja akawaambia wote hataki kuwaona ndani mwake.

  Yaani mtu anatia timu Dar na hata sura hamjawahi kuiona anasema mimi ni mume wako (wakati ni mwanamke mwenzio kisa kaka kaoa) anaanza mashari kuliko mume mwenyewe huku kaja na mimba na katoto kengine. Anamwambia h/girl kamuoshe mwanangu; mbona mmpepika maharage etc. Mbaya zaidi anasema narudi nyumbani mwakani ila ntamuacha mwanangu asome mjini. Mdada akasema inahuuu. Timulia mbali.
  Mumewe nduguze wakamnunia mwaka mzima baada ya hapo nadhani walijaribu na kwa mawifi wengine wakakuta ndio worse wakaanza kumwambia huyo mume wa rafiki yangu; tumeamini mke umepata.

  Mawifi si wa kuendekeza kabisa kama hawana adabu TIMUA.

  Upande wa pili ni rahisi kuishi na ndugu upande wa mke kwa kuwa wanakuwa wapole (wameolewa Lol.) Na wana msaada mkubwa tu kwa kazi za ndani. Hivyo kama mnapenda kukaa kwa watu mkae kwa dada zenu.
   
Loading...