........mke kujua bei/gharama za g/house ama hotel ni kosa?

fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,987
2,100
......jana nilitembelewa nyumbani na rafiki yangu akiwa na mkewe(mjamzito miezi 6 sasa) na wamefunga ndoa wiki 3 zilizopita,tukapa dinner pamoja na mke wangu na baade usiku tukatoka kumalizia siku sehemu fulani kwa vinywaji....huko tukakutana na baba yake mdogo,mgeni kabisa mji huu hivyo ikabidi atafutiwe g/house kwa malazi,katika kujadili sehemu rahisi mkewe pia akasema sehemu anayoijua kuwa ninzuri na rahisi,hapo ndio shida ilipoanzia,ugomvi mkubwa uliibuka baina ya wanandoa hao mbele yetu,mke alipigwa,mume akimtuhumu mkewe ni malaya na anapelekwa sehemu hizo na wanaume wengine ndio maana anajua!mengi nilijiuliza hivyo nikaona ni vema niliweke hapa tujadili,hii imekaa kaaje wajamani?
 
Imekula kwake!ajiulize kama alishapata wageni hapo nyuma?kama hapana ahesabu maumivu.
 
Kama huyo mke ni mfanyakazi wa ofisi ambazo uwa zinapokea wageni wa kiofisi anaweza kufahamu gharama za guest house. Pia si kila anayeenda guest house anaenda kwa ajili ya kufanya uzinzi.
 
Kama huyo mke ni mfanyakazi wa ofisi ambazo uwa zinapokea wageni wa kiofisi anaweza kufahamu gharama za guest house. Pia si kila anayeenda guest house anaenda kwa ajili ya kufanya uzinzi.
 
huyo mwanaume ana ufinyu wa akili, utampigaje mkeo? Tena mjamzito? Kwa wivu wa kipuuzi na kutokujiamini? Kwa nini asimuulize amejuaje akapata jibu? Kwani yeye bei za hoteli hazijui? Na kama anazijua amejuaje? Nachukia mijanaume inayogeuza wakezao punching bag
 
Kumpiga mwanamke haijakaa sawa...tena binti wa watu ni mjamzito...makofi ndio yatamfanya asiwe kiruka njia?
 
Unampigaje mkeo halafu mjamzito, kwanza angekuwa na tabia hizo asingeropoka chochote, itakuwa tu amejua maybe alipeleka wageni
 
Mwenyewe nina daut na huyu mwana dashost kajulia wapi. Na pia sio njema kumpiga angemuuliza taratibu ndo angepata ukweli zaidi
 
Mpaka hapa nimeshakua na dought juu y hiyo mimba cyo y jamaa ......
 
sorry nimepost bila kumaliza nilichataka kusema.namuonea huruma huyo mke,kama huyo mume ameweza kumpiga mke wake mbele za watu,hiyo ndoa yao itakuwa ni ya vipigo tu.wanaume wa aina hiyo,huwa hawaachi tabia ya kupiga piga.akishakupiga ataomba msamaha,baadae atarudia tena.huyo jamaa angekuwa mstaarabu angalau angemuuliza vizuri,wakiwa wenyewe peke yao,na sio mbele za watu hivyo.watu wengine mbona hawana heshima?
 
Kwakua wameona muda si mrefu inaelekea huyo mke kakumbuka bei zile ambazo alikua akipelekwa na mwenzi wake kabla ya ndoa
 
wanaume wasiojiamini siku zote ngumi mkononi...pole zake huyo dada, shez preg, still jamaa kampiga , ni hv ndoa changa hapo ataambiwa vumilia ndio mumeo huyo bt wanaume wa ngumi mkononi huwa hawaachi wajameni hata wakiomba msamaha kwa machozi!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom