fabinyo
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 2,991
- 2,108
......jana nilitembelewa nyumbani na rafiki yangu akiwa na mkewe(mjamzito miezi 6 sasa) na wamefunga ndoa wiki 3 zilizopita,tukapa dinner pamoja na mke wangu na baade usiku tukatoka kumalizia siku sehemu fulani kwa vinywaji....huko tukakutana na baba yake mdogo,mgeni kabisa mji huu hivyo ikabidi atafutiwe g/house kwa malazi,katika kujadili sehemu rahisi mkewe pia akasema sehemu anayoijua kuwa ninzuri na rahisi,hapo ndio shida ilipoanzia,ugomvi mkubwa uliibuka baina ya wanandoa hao mbele yetu,mke alipigwa,mume akimtuhumu mkewe ni malaya na anapelekwa sehemu hizo na wanaume wengine ndio maana anajua!mengi nilijiuliza hivyo nikaona ni vema niliweke hapa tujadili,hii imekaa kaaje wajamani?