........mke kujua bei/gharama za g/house ama hotel ni kosa?

Kama huyo mke ni mfanyakazi wa ofisi ambazo uwa zinapokea wageni wa kiofisi anaweza kufahamu gharama za guest house. Pia si kila anayeenda guest house anaenda kwa ajili ya kufanya uzinzi.
Kwy RED kumbe huwa wanaenda kufanyaje?
 
Kama huyo mke ni mfanyakazi wa ofisi ambazo uwa zinapokea wageni wa kiofisi anaweza kufahamu gharama za guest house. Pia si kila anayeenda guest house anaenda kwa ajili ya kufanya uzinzi.
huyo mke anafanyakazi katika saloon ya kike
 
Unampigaje mkeo halafu mjamzito, kwanza angekuwa na tabia hizo asingeropoka chochote, itakuwa tu amejua maybe alipeleka wageni
kweli,hata yeye alijitetea hivyo lakini mume hakuelewa somo
 
sorry nimepost bila kumaliza nilichataka kusema.namuonea huruma huyo mke,kama huyo mume ameweza kumpiga mke wake mbele za watu,hiyo ndoa yao itakuwa ni ya vipigo tu.wanaume wa aina hiyo,huwa hawaachi tabia ya kupiga piga.akishakupiga ataomba msamaha,baadae atarudia tena.huyo jamaa angekuwa mstaarabu angalau angemuuliza vizuri,wakiwa wenyewe peke yao,na sio mbele za watu hivyo.watu wengine mbona hawana heshima?
teh teh teh,kweli wewe kisukari,uko sawa shost
 
wanaume wasiojiamini siku zote ngumi mkononi...pole zake huyo dada, shez preg, still jamaa kampiga , ni hv ndoa changa hapo ataambiwa vumilia ndio mumeo huyo bt wanaume wa ngumi mkononi huwa hawaachi wajameni hata wakiomba msamaha kwa machozi!
..kweli,tulimbeleza mke kuwa avumilie japo ilikuwa kazi ngumu sana na sisi tulishindwa kuwaacha katika hali hiyo kwani tulikuwa nao muda mwingi siku hiyo na jamaa angempiga sana bila sisi...mwishowe alikubali kuingia kwenye gari tukawapeleka kwao kwenye saa sita usiku hivi,pia tulimsihi mume asimpige tena
 
......jana nilitembelewa nyumbani na rafiki yangu akiwa na mkewe(mjamzito miezi 6 sasa) na wamefunga ndoa wiki 3 zilizopita,tukapa dinner pamoja na mke wangu na baade usiku tukatoka kumalizia siku sehemu fulani kwa vinywaji....huko tukakutana na baba yake mdogo,mgeni kabisa mji huu hivyo ikabidi atafutiwe g/house kwa malazi,katika kujadili sehemu rahisi mkewe pia akasema sehemu anayoijua kuwa ninzuri na rahisi,hapo ndio shida ilipoanzia,ugomvi mkubwa uliibuka baina ya wanandoa hao mbele yetu,mke alipigwa,mume akimtuhumu mkewe ni malaya na anapelekwa sehemu hizo na wanaume wengine ndio maana anajua!mengi nilijiuliza hivyo nikaona ni vema niliweke hapa tujadili,hii imekaa kaaje wajamani?
<br />
<br />
Pole zake bwana harusi hakujua kuwa kaoa kurumbembe Nazjaz
 
huyo mwanaume ana ufinyu wa akili, utampigaje mkeo? Tena mjamzito? Kwa wivu wa kipuuzi na kutokujiamini? Kwa nini asimuulize amejuaje akapata jibu? Kwani yeye bei za hoteli hazijui? Na kama anazijua amejuaje? Nachukia mijanaume inayogeuza wakezao punching bag

Tehe tehe tehe tehe tehe! Kazi kweli kweli!
 
Kwy RED kumbe huwa wanaenda kufanyaje?

Mm nasoma hapa tu"ninzuri na rahisi" hii ni hatari kwa mama wa familia! Hata kama angekuwa mfanyakzi wakupokea na kupeleka wagen kwny mahoteli hili liko wazi huyu ni kicheche jamaa imekula kwake hata mimba hiyo mmmmmmmmh!

Ofisi zinapeleka watu kwny mahotel co Guest au ofis gani hiz!!!!!!!!!!
 
Jamaa anagongewa, tena na guest za hapo hapo karibu kitaani duh! akapime afya kwanza!
 
makubwa ngumi tena ila imekaaje ameolewa wiki 3 nanaujauzito wa miezi 6 au mimba sio ya jamaa kuna maswali mengi yaliyosababisha jamaa kupiga mke wake
 
Huyo mwanamume ni mpuuzi...nadhani bado yuko under age!!

Kwa watu wenye A, B, C za uchnguzi, hiyo taarifa ilikuwa ni tip ya nguvu sana na alitakiwa aanze kuutafuta ukweli. Kwa sasa amehangaika na hisia zake na ukweli wenyewe hatakaa aupate maishani...Na kwa mwendo huo, hiyo ndoa imeshaingia doa...Aombe Mungu wapate hata huyo mtoto wakiwa bado wako pamoja...Mzimu wa bei za gust house utaendelea kumtafuna siku zoooote!!

Babu DC (1947)!!
 
......jana nilitembelewa nyumbani na rafiki yangu akiwa na mkewe(mjamzito miezi 6 sasa) na wamefunga ndoa wiki 3 zilizopita,tukapa dinner pamoja na mke wangu na baade usiku tukatoka kumalizia siku sehemu fulani kwa vinywaji....huko tukakutana na baba yake mdogo,mgeni kabisa mji huu hivyo ikabidi atafutiwe g/house kwa malazi,katika kujadili sehemu rahisi mkewe pia akasema sehemu anayoijua kuwa ninzuri na rahisi,hapo ndio shida ilipoanzia,ugomvi mkubwa uliibuka baina ya wanandoa hao mbele yetu,mke alipigwa,mume akimtuhumu mkewe ni malaya na anapelekwa sehemu hizo na wanaume wengine ndio maana anajua!mengi nilijiuliza hivyo nikaona ni vema niliweke hapa tujadili,hii imekaa kaaje wajamani?

Wakati huyo mume anampiga mkewe alikuwa ana akili timamu au alikuwa ameshagida pombe?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom