Mke kugombana na mmewe na kisha kulipiza kisasi kwa watoto walio wazaa ni sahihi?

Aug 9, 2017
33
62
Tumedumu na mke wangu kwenye ndoa kwa muda wa miaka sita, tunawatoto wawili. Sasa imekuwa tukikorofishana na mke wangu kisasi analipiza kwa watoto tulio wazaa mimi na yeye kwakuwapiga, hivi ni sahihi?
 
Watoto hao tulizaa mimi na yeye!
Aisee, nadhani hao watoto huwa wanakosea sio kwamba anawapiga kwa kuwaonea, si unajua ile feeling wee umekabwa na kitu rohoni halafu anakuja mtu mwingine muda huohuo anakuudhi.

Ushauri, jaribu kumaliza tofauti zako na mwenzio mara tu zinapojitokeza sio huo utaratibu wako wa kumkera mwenzio kisha unaondoka....hata sijui huwa unaondoka kwenda wapi ni mchepukoni au bar?
 
Aisee, nadhani hao watoto huwa wanakosea sio kwamba anawapiga kwa kuwaonea, si unajua ile feeling wee umekabwa na kitu rohoni halafu anakuja mtu mwingine muda huohuo anakuudhi. Ushauri, jaribu kumaliza tofauti zako na mwenzio mara tu zinapojitokeza sio huo utaratibu wako wa kumkera mwenzio kisha unaondoka....hata sijui huwa unaondoka kwenda wapi ni mchepukoni au bar?
Bar
 
Mnapokwazana muwe mnakaa chini mnazungumza, huenda huwa unamuonea nae anatafuta anaoweza kuwaonea, kuwapiga si sawa ila huenda anawapiga kwasababu wanakosea afu wewe unajishtukia kuwa anamalizia hasira kwao ....Bro ili mapenzi yawe imara mazungumzo ndo nguzo hata mnapokwazana.
 
Back
Top Bottom