Mke kuficha hati ya kiwanja/nyumba

"actually imeandikwa jina lake Mimi nipo kama shahidi"

Kumbuka mali ya baba/mwanaume ni ya wote, mali ya mama/mwanamke ni yake peke yake...
Umeshafanya kosa...
 
Wananzengo salamu kwenu.

Kuna jambo nakaa nalifikiria sipati jibu na sijui mwenzangu anawaza nini na ana nia gani.

Nilikuatana na huyu mwanamke mwaka 2011 nikiwa chuo na Yeye yupo tu kitaa baada ya muda akafanikiwa kupata kazi tukaendelea kuishi na kupata watoto hadi mwaka jana tulipofunga ndoa ya kiserikali maana tumetofautiana imani na hakuna Kati yetu aliye tayari kumfuata mwenzake.

Kimsingi huyu mwanamke alinunua kiwanja baada ya kukopa hela then akaanza ujenzi na mimi nikaweka hela yangu kidogo ninayopata na nilichukulia hii nyumba ni mali ya familia kwa maana tuna watoto watatu.

Sasa hivi karibuni mwenzangu kaichukua ile hati ya kiwanja na sijui kaipeleka wapi,actually imeandikwa jina lake Mimi nipo kama shahidi.

Ndoa yetu kwa sasa imekua ya migogoro sana natunaishi kwa mazoea tu na isitoshe tunaishi mikoa tofauti japo ya jirani.

Sasa kitu kinachonishangaza ni huyu mwanamke kuficha hati ya kiwanja Ili hali tumeamua kufanya hii mali iwe ya familia ina maana watoto sasa Yeye anapoficha hiyo hati likija la kutokea mi nitajua hiyo hati ipo wapi!!? Kama kitu tumeamua kiwe cha familia sioni haja ya kuanza kuficha document muhimu kama hati.

Niliwahi kumuuliza ile hati ipo wapi mbona tangu tumetoka kugonga mhuri kwa mwenyekiti siioni humu ndani ananipiga kiswahili tu.

Mimi naishi kwenye hii nyumba na yeye yupo mkoa jirani kikazi yupo pamoja na watoto.

Je huyu mwanamke yupo sawa kweli kuficha hiyo hati!!? Ili hali tumefunga ndoa na tuna watoto tayari. Sijui Nia yake nini nahitaji ushauri niishi nae vipi huyu mtu manake anaonekana ana ubinafsi mkubwa sana.
Pole mkuu Wanawake huwa na akili za kipekee keshaona siku moja hatakuwa na haki yeye wala watoto wake.
TAFUTA CHAKO MKUU UANDIKE MAJINA YAKO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom