Mke hawezi kushindana na ubabe wa mwanaume! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke hawezi kushindana na ubabe wa mwanaume!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, May 7, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanaume kimaumbile hataki kuona aina ya mashindano na mke. Anapogundua kuwepo kwa aina ya mashindano, huwa anajitahidi sana kuhakikisha kwamba, anashinda. Katika juhudi yake ya kutaka kushinda ndio hapo anapofanya vituko vikubwa na vya ajabu zaidi. Mwanamke anashauriwa kuhakikisha kwamba hampigii magoti mwanaume, bali anaepuka kushindana naye. Mwanaume anaweza kumuudhi mwanamke, badala ya mwanamke kusema, ‘mwache tu,' na kuanza kufanya vituko kama kumkasirikia, kutomjali, kuonyesha kwamba hata yeye ni ‘mbabe,' anatakiwa kuonyesha kukerwa kwake kwa kiwango cha mumewe kujua kwamba amemkera. Baada ya hapo aendelee kufanya mambo yake kama vile hakujatokea jambo.

  Kwa mfano mume ametoa majibu yasiyopendeza kwa mkewe, mke anaweza kumwambia mumewe kwamba hajaridhishwa na majibu hayo. Bila kujali mume amejibu nini, mke anatakiwa kuendelea kufanya mambo yake kama vile halijatokea jambo lolote. Kama mume ni muungwana, hatakaa kimya, baada ya muda atamuomba mke radhi. Mwanamke yeyote anaweza kujaribu jambo hilo leo.

  Kwa hiyo mwanamke anatakiwa kujua ‘ubabe' ndiyo asili ya mwanaume na upole na upendo viko ndani ya damu ya mwanamke na ndio maana huwa inasemwa kuwa, kama mwanamke akitaka anaweza kumfanya mumewe akafuata kila anachomwambia (kwa manufaa ya wote)kwa kutumia silaha yake ya upole na upendo. Lakini ni wanawake wangapi wanaitumia silaha hii? Bila shaka sio wengi na ndio maana wengi hushindwa kulinda ndoa zao.
   
 2. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Ngoja kina Asnam waje, mie hayo mambo nimeshajiwekea 'efu' kabisa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kipipi ................Ndio unatakiwa uhudhurie hii twisheni yangu............Nitakufunda bibie na ndoa yako itakuwa imara kama chuma cha pua
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Thats what makes different between man and gentleman. Hiyo stori yako haimhusu gentleman, vya aina hapo juu ni wengi sana fungu kwa mia.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  MadameX .................. hapo nilikuwa nawashauri wale wanawake walioolewa na Man ..............Haiwahusu walioolewa na Gentleman kama Mama Ngina...........LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Yataka moyo haki ya nani!
  Jitu limekuudhi kwelikweli afu uendelee kulionyesha mahaba??
  Hivi mi ndoa ntaiweza kweli?HAPANA
   
 7. J

  JOJEETA Senior Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh kwa kweli ni ngumu.mie cwezagi kukaa na kijiba cha roho,na mwenyewe keshanizoea kwani ukinikosea nakupa live ikitokea nikanyamaza cmalizi cku walah nahic kama moyo unaungua moto,hata yeye atashangaa.mbona me nikikosea ananipa live?kwa nini mwanamke ndo awe mpole na mwenye upendo?y not men?jamani hata kwenye mapenzi bado kuna gender?fifty fifty bwana
   
 8. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Na bahati mbaya saana sitokaa niweze hata kujikongoja walau niscore daraja 'D'! To me kama umenikera there is no kunyenyekea..... its either A or B.......choose accordingly, yamekushinda sepa fastaaa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hahaha!!! Mtambuzi you must be kiddin me...huyu mke wa namna hii kwangu mimi :nono::nono:...lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Una akili sana Mtambuzi! U spoke my mind! huwa na mwambia mke wangu kitu hikihiki! U dont want to worsen mambo kaa kimya usishindane, maana u dont expect me to keep quite, I always want on top! Halafu sifanyi hivyo kwa sababu nataka kudominate hapana huwa inatokea tu wakati mwingine bila hata kujijua! Reflex badae mambo yakishapoa unaanza kujiuliza
   
 11. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  mmmh hiyo balaa yani alete uchuro afu umpelekee maji bafuni atakula jeuri yake ikibidi na chakula aende kwa mama ntilie manake hata hamu ya kupika haitakuwepo.chezea maudhi ya mtu mzima
   
 12. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Utaiweza tu hii chungu-tamu.....................
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kwa Zamani, wanawake walifunzwa vilivyo kupitia unyago namna ya kuishi na wanaume na kuwavumilia. Na ndiyo sababu ndoa nyingi za zamani zilikuwa zinadumu sana ukilinganishi na hizi za sasa. Ila kwa sasa, kutokana na elimu, exposure waliyopewa wanawake pamoja na mfumo wa haki sawa na zile tamaduni za ki-magharibi, suala la Wanawake kunyamaza kimya na kutii waume zao hata kama kosa ni la mume, hilo halipo na kama lipo basi ni kwa wachache sana.

  Mfumo mzima wa sasa kaka mtambuzi, wa mahusiano ya wanandoa ni wewe ukimwaga mboga, mke anamwaga ugali, hapo tunaita ngoma droo!

  Natamani kama mila na desturi zetu zingerudi na kufanyiwa maboresho kidogo dada zetu wasinyanyaswe but wapewa mafundisho sahihi ya kutunza na kuheshimu ndoa zao, huku na sisi vidume tukipewa yale mambo ya jandoni basi ndoa zingedumu sana.

  Samahani kwa kutoa mchango nje kidogo ya mada, I was just tying to think beyond kidogo ya hii mada ...
   
 14. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wanaume wa kihaya wanatofauti kubwa na sisi wakulya!! Mtambuzi ni mhaya stori kama hizo anazifagilia wakati hapa Tarime ukisikika unamdekeza mkeo au kumuomba msamaha watu watajipanga kukuvamia na kukuchinja wewe na mkeo, jambo hilo kulizungumza hadharani unaweza kuhatarisha maisha yako
   
 15. mambo

  mambo JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 2,377
  Likes Received: 5,013
  Trophy Points: 280
  Well explained nakubaliana na maelezo yako kwa kiasi kikubwa, ni kweli mwanamke anapokuwa na kelele kila wakati mume anakimbia kisailensa .
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  JOJEETA .............Umesoma vibaya, hebu rejea maelezo yangu..............Nilisema akikuudhi mweleze lakini usijisumbue kumuwekea kiburi......Mweh !
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma mzee na nakubaliana na wewe, kuna wengine wanakuwa successful kwenye hii area mpaka unashangaa hiki kidume mbele ya mke topetope. Na kuna wengine wanatumia upole wa mke kumwangamiza zaidi hapo unasemaje?
   
 18. Mabuzuki

  Mabuzuki Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kaka mutabuzi mtu akikusoma vizuri ataelewa unachosema, asipo tulia ataona kama vile unashauri wake za watu kuwa makondoo., sio kweli. MWANAUME kuwa juu maana yake sio kumtukana/kumpiga/kumnyanyasa/kumdharau ........ mwanamke, la hasha!!! ni kuskilizana na kuheshimiana MWANAMKE akijua hivyo na akawa anajitahidi kuwa chini kama mtoa mada anavyo sema Ndoa zitatulia sana. Mwanaume mwenye akili akikosea na akaambiwa na mkewe kwa heshima bila kutaka kuchukua nafasi isiyo yake atafanikiwa. Shida ya kizazi cha sasa ni elimu, BEIJING. Huu sio mpango wa MUNGU. Soma vitabu vitakatifu utalibaini hili.

  NASISITIZA: SIO KUMNYANYAPAA MWANAMKE ila MWANAMKE AJUE NAFASI YA MUMEWE NA AIHESHIMU, Mwanaume asiyefanya hivyo naye hana maana tu.
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  hiyo ilikuwa zamani siku hizi ukimwaga ugali mkeo anamwaga mboga
   
 20. J

  JOJEETA Senior Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtambuzi,nimekusoma bt ili niwe normal must aombe msamaha hata kama anazuga bila hivyo ni KUNUNA TU mpaka kieleweke.
   
Loading...