Mke au Mtoto Wako Yupi wa Kumuokoa? Amuokoa Mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke au Mtoto Wako Yupi wa Kumuokoa? Amuokoa Mkewe

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Dec 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Mke au Mtoto Wako Yupi wa Kumuokoa? Amuokoa Mkewe
  [​IMG]
  Stacy Horton kulia akiwa ameshikilia picha ya mtoto wake aliyezama, kushoto ni mke wake Vanessa Tuesday, December 01, 2009 3:15 AM
  Baba mmoja wa nchini New Zealand alikuwa na wakati mgumu wa kuchagua yupi amuokoe kati ya mkewe au mtoto wake wa kiume wakati gari lao lilipozama kwenye kina kirefu cha maji. Ulikuwa ni wakati mgumu wa kutoa uamuzi wa haraka wa kuchagua yupi wa kumuokoa kati ya mke na mtoto wakati gari la familia lilipodumbukia na kuzama kwenye mto wenye kina kirefu cha maji.

  Stacy Horton aliamua kumuokoa mke wake aliyekuwa akipiga kelele akitapatapa kwenye maji akijaribu kujiokoa baada ya kufanikiwa kutoka kwenye gari lao ilililokuwa likizama huku mtoto wao wa kiume Silva akiwa amenasa ndani ya gari hilo mita 4.5 chini ya maji.

  "Nilijaribu kupiga mbizi chini kumuokoa mtoto wangu lakini sikuweza kulifikia gari alilonasa ndani yake, kitu kilichonijia akilini ni kumuokoa kwanza Vanessa", alisema Horton akiongea na televisheni moja ya habari nchini New Zealand.

  "Nilifanikiwa kumpata mkewe wangu na kumuokoa na tulikaa naye pembeni ya mto huku tukiziona taa za nyuma ya gari kwa mbali, tulibaki tukilia huku tukisali".

  "Nilikubali kuwa ndio ameishatutoka, sikuwa na uwezo wa kufanya chochote cha kumuokoa", alisema Horton.

  Vannessa alikuwa kwenye gari pamoja na mwanae mwenye umri wa miaka 14 siku ya jumamosi jioni wakati gari lao liliposerereka kwenye ukingo wa sehemu yenye mwinuko na kudondokea kwenye mto unaopita karibu na nyumba yao katika mji wa Wanganui nchini humo.

  Rafiki yake Silva, Robert Palmer ambaye naye alikuwa kwenye gari hilo alifanikiwa kujiokoa toka kwenye gari hilo wakati lilipoanza kuzama na kuwahi kumpelekea taarifa Horton kuhusiana na kuzama kwa mwanae na mkewe.

  Baada ya Horton kufanikiwa kumuokoa mkewe, maafisa wa polisi walijaribu kupiga mbizi kumuokoa Silva lakini walishindwa kulifikia gari alilokuwemo.

  Zimamoto nao waliingilia kati kwa kujaribu kulivuta gari hilo karibu ili kumuokoa Silva, lakini mpaka walipofanikiwa kufanya hivyo, Silva alikuwa ameishaiaga dunia. http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3655490&&Cat=2
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  kwa laifu la siku hizi bora angemuokoa mtoto. unaweza ukamuokoa mke halafu ndani ya mwezi mmoja akakupiga kibuti. hapa naweza nikapata mashambulizi kutoka jinsia inayovaa sketi na blauzi!
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  no diskasheni hapo mkuu!.
  unaokoa MTOTO, then kama mke utaoa mwingine,
  period.
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kweli wa mchungu!!! inasikitisha walimpoteza mtoto kwa kweli na inaonekana baba alitamani kuwaokoa wote ila uwezekano wa kumwokoa mtoto ulikuwa mdogo.

  on the sketi na blauzi point of view bora mama apone maana kuna uwezekano wa kutengeneza Silva mwingine!!!
   
 5. K

  Kawonganila New Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 11, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Umuokoe mkeo kwani mliweka ahadi. Kwenye raha/shida, uzima/ugonjwa......
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  deh deh deh tatizo linakuja bikozi nyinyi ma waif to be hamna gerentii, kumpiga mtu kibuti kwenu ni hobby. wewe sikiliza bbc sana keshokutwa utaskia jamaa kamwagwa na huyo mdada wizauti any sababu.
   
 7. GP

  GP JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaa,
  mkuu kibluurei chako kitamu sana!.
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  for beta for worse.....eeeh baba naona alirecall hiyo phrase akaimplement right away!!!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  From genetics point of view, your child has 50 % of your chromosomes! a wife has none......nitaokoa mtoto wangu after all nasogeza nyumba ndogo tu maisha mdundo!
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Dah. Aisee hapa umenifumbua macho. You must be a Doctor Masa
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Teh teh teh teh ......hapana mkuu ....LOL
   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sasa klorokwini huyu alikua wifu sio to be au mie nimeelewa ndivyo sivyo.

  hata hivyo mahasbandi tu bi na wao hivo hivo hawaeleweki utashangaa mtu anabutuliwa on the twinkling of an eye!!!

  siku hizi hamna garantii si kwa maHE wala maSHE!!!
   
 13. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkuu nabishana na wewe hapa, kitaalamu tatizo lililompata agent/mwokoaji kwa ki philosophy/ethicists linaitwa/wanaita moral dilemma-ni situation ambayo an agent(here refered as mwokoaji/mume) regards him/herself as having moral reasons to do each of two actions, but doing both actions is not possible.

  Na kutokana na maelezo utaona kuwa alimwokoa mke then akamfwata mtoto kwenye depth ya 4 point chini but found wedged and dead already. So it wasnt his wish to let the situation tht way.
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kama mwanamke...ningemuokoa mwanangu!
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  lakini kwa case hii ni mama na mtoto ndo walihitaji kuokolewa na baba
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  It makes sense! chukua tano
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hongera kwa post 536... but sikubaliani na hio sentence hapo juu
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ndio mana nikasema mie kama mwanamke ningemuokoa mwanangu, yeye yakimfika atajua mwenyewe wa kumuokoa mami, hebu sema kama ndio ingekuwa muokoaji ni wewe ungemuokoa nani?
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  dhahiri kabisa will go for my kid!!!
   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  ahhh mtoto wangu hakuna wa kuniambia kitu mweh, wacha tu nimuokoe yeye mana ananifariji kupita maelezo.
   
Loading...