Mke atongozwa, mumewe amuua kwa panga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke atongozwa, mumewe amuua kwa panga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 23, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Kijiji cha Nyaumata, Kata ya Somanda wilayani Bariadi, mkoani Shinyanga, Mayunga Mteremko ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mkewe.

  Inadaiwa kwamba, Mteremko alimkatakata mapanga mkewe hadi kufa kutokana na wivu wa mapenzi.

  Taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha inasema, Mteremko anadaiwa kufanya tendo hilo baada ya kumuona mkewe, Kabula Lugiko (38) akiwa anasalimiana na Majaba Kimini (40).

  Kamanda Kamugisha aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa mauaji hayo yalifanyika juzi saa 4 asubuhi katika Kijiji cha Nyaumata.

  Kwa mujibu wa Kamanda, siku ya tukio Mteremko akiwa amejibanza karibu na shambani kwao alimuona Majaba akiwa anazungumza na mkewe wakati mwanamke huyo akiwa shambani.

  Inadaiwa kwamba wanandoa hao walipokutana nyumbani, Mteremko alimhoji mkewe jambo alilokuwa akizungumza na Majaba hali iliyozusha mtafaruku.

  “Kabula alikiri kuwa Majaba alikuwa akimtongoza lakini yeye hakukubali, kitendo kilichopingwa na mumewe Mteremko na kuamua kuchukua panga akaanza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema Kamanda Kamugisha.
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh Hasira zingine bwana sasa 'nduhu tabu' amesababisha tabu kubwa kwake na kwa familia maana amewafanya wanae wawe yatima.
  RIP marehemu kabula lugiko
   
 3. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huyo mwehu!
   
 4. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wenye tabia ya kutongoza wake za watu nao wakome pia, ndo wanaoleta tabu kwenye jamii.
   
 5. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #5
  May 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Hasira Hasara....
   
 6. Graca

  Graca JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 472
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Poor woman!
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Usizini!

  mshahara wa dhambi ni mauti!
   
 8. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  Angeenda kumkabili huyo mtongozaji kwani aliwaona wakiongea tuu!asa atafia jela kwa upumbav wake
   
 9. s

  sawabho JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Uzinzi na wake za watu................... NOMA. Hapa kutakuwa kulikuwa na hear say au huyo Kimini ana tabia cha katika eneo hilo, sio rahisi kwa kuwaona wasogoa tu, aende kuchukua sheria kali mikononi namna hiyo.
   
 10. AlP0L0

  AlP0L0 JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 3,473
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  lakini amotoa somo kwa wazinifu.
   
 11. s

  sawabho JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kweli Mkuu hawa watu wanaudhi sana. kwa sababu mmiliki halali unajihidi kuboresha halafu mwingine anavuta utamu kiurahisi. Anapaswa kuwekeza kwenye "Congo Free State" ambazo siku hizi ni nyingi kinoma.
   
 12. K

  Kyeli Lula Member

  #12
  May 24, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huu ni ukatili wa kijinsia tu hata kama walikuwa wanatongozana adhabu yake ni mwanamke kupigwa mapanga? mbona hakumfata yule mwanaume na kumpiga mapanga, huu ni uonevu kwa wanawake amekatili maisha ya huyu mama kinyama sana watoto wamebaki yatima bila sababu yoyote ya msingi, inaumiza sana
   
Loading...