Mke anapochukua likizo na kumficha mumewe ili ajirushe na bosi wake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke anapochukua likizo na kumficha mumewe ili ajirushe na bosi wake!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jangakuu, Sep 23, 2012.

 1. Jangakuu

  Jangakuu JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  KWA wale wenzangu na mimi ambao tayari tupo katika maisha ya ndoa, bila shaka wanaelewa ni jinsi gani mume na mke wanavyotakiwa kuheshimiana katika maisha yao ya kila siku ndani ya ndoa zao. Ingawaje kuna tofauti za staili za maisha kati ya watu na watu, lakini kwa ujumla iwe ni familia ya kimaskini au ya kitajiri, heshima ya maisha ya ndoa lazima iwepo pale pale bila ya kujali tofauti za aina yoyote ile, vinginevyo maisha ya ndoa hayawezi kudumu na kama yatalazimishwa yaendelee kuwepo wakati heshima hakuna, basi yatakuwa ni ya tafrani zisizokuwa na kikomo.

  Waswahili wanasema: "Ukitaka kujua utamu wa ngoma, ingia ucheze mwenyewe". Hivyo ni vigumu sana kwa yule ambaye hajaingia katika maisha haya kupata picha halisi ya jinsi mmoja wa wanandoa anavyoipokea au kushindwa kuipokea hali halisi baada ya kugundua mwenza wake jinsi anavyojichanga na watu wengine nje ya ndoa yao kwa kutumia visingizio vya hapa na pale vya kazini kwake! Lakini kwa wanandoa, hilo halina kipingamizi, lazima litamuumiza mwenza na kumnyima raha kwa kipindi kirefu.

  Hebu jaribu kufikiria, wewe ni mwanamme kila siku mnaondoka nyumbani kwenu pamoja na mkeo kwa minajili ya kuelekea sehemu zenu za ajira, mkifika kituo cha daladala mnaachana kwa kila mmoja wenu kupanda basi kuelekea usawa wa ofisi yake ilipo huku mkipeana maneno matamu tamu ya kutakiana kheri katika kazi zenu za siku hiyo na kuombeana amani mkutane salama jioni nyumbani kwenu.

  Baada ya siku kadhaa unapata fununu na hatimaye ukweli kuwa mkeo ana zaidi ya wiki nzima tangu alipoanza likizo, na katika kipindi cha siku hizo zote anavyokuaga kuwa anakwenda ofisini kwake kama kawaida siyo kweli, bibiye huishia kona na bosi wake ambaye naye amechukua likizo. Je, kama ni wewe na ukilitambua hilo utafanyaje? Ni dhahiri matokeo yake yatategemeana na kiwango cha hasira na busara za mwanamme husika.

  Haya yote nimelazimika kuyasema leo hii kutokana na bibiye fulani ambaye ana miaka kadhaa katika maisha yake ya ndoa yenye watoto wawili wa kike, lakini ghafla katika siku za karibuni kaanza mapepe ya kichangu changu ambayo labda kama ni ya muhimu sana kwake, basi alitakiwa awe ameyafanya takribani miaka kumi iliyopita, kamwe siyo sasa akiwa kama mke wa mtu na mtu mwenyewe ni yule anayejiheshimu vizuri mbele za watu wengine na nafsi yake pia.

  Mambo kama hayo mbali ya mwanamke huyo kumdhalilisha mumewe mbele ya watu wengine na yeye mwenyewe kuonekana kituko kwa kuwadhalilisha wale wanaoheshimu pete za ndoa zao, vile vile inashangaza zaidi bibiye huyo anaposhindwa kutambua kuwa tabia hiyo chafu aliyoianza ghafla akiwa na miaka kadhaa ndani ya ndoa yake inaweza ikamtumbukiza katika hatari ya kupata maambukizi ya ukimwi!

  Wewe ni mke wa mtu, tena wa ndoa iliyopata baraka zote za kasisi kanisani, vipi kwa ghafla namna hiyo umeamua kuingia ubia na bosi wako hadi kufikia hatua ya kumdanganya mumeo kuwa likizo yako bado kumbe tayari umeishaianza kwa kuitumia vema na bosi wako kona na kumtelekeza mumeo aliyekutoa huko mkoani na kukuhamishia Dar es Salaam!

  Ingawaje nafahamu fika kuwa wanawake wenye tabia kama hiyo ya huyo bibiye aliyoianza hivi karibuni wapo wengi, lakini kwa kweli ni mambo ya aibu sana kwa mwanamke ambaye alikuwa na heshima nzuri mbele ya mumewe, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wafanyakazi wenzake, ghafla anapokurupuka na kuanza kujiingiza katika matatizo mengine ya kugombania mume wa mtu mwingine wakati akijua fika kuwa yeye ni mke wa mtu na tena ambaye bado pete yake ya ndoa inameremeta! Kwa ujumla haipendezi hata kidogo.

  Nasema hivyo kwa maana kuna mambo mengine yanayofanywa na baadhi ya watu katika jamii zetu, si tu kwamba yanawadhalilisha wahusika, bali ni aibu pia kwa jamii husika kama itaendelea kuyaangalia na kuyaacha yaendelee kujichimbia mizizi bila ya kuyatafutia mikakati ya kuyakomesha au kuyapigia kelele ili yapungue kendelea kuwepo na kusababisha madhara kwa watu wengine pia.

  Na wewe bosi, ni nini hasa unachokitafuta kutoka kwa mke wa mwanaume mwenzako wakati wasio na waume wamejaaa kibao Jijini Dar es Salaam? Huu nao ni ufataki wa aina nyingine, bosi kwa kuwa ana madaraka na pesa yake ni ndefu ukilinganisha na mume wa bibiye huyo, basi hapo ndipo ndoana zake anapozirusha na kumharibia mwenzake ndoa yake.

  Hayo si mambo hata kidogo, utachukuaje likizo na kumficha mumeo ili uendekeze uasherati wako na bosi wako?
   
 2. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  utasutwa unajuaje kama wamekubaliana na mumewe!
   
 3. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duh, ngoja kidogo nitarudi!
   
 4. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na kweli,manake kwenye ndoa kuna mambo ya ajabu na mapatano ya ajabu na nyengine ni za mikataba. Unless utuambie hyo inakuhusu wewe kwa namna flani. Teh Teh!
   
 5. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mimi wala sishituki kabisa tena yeye ndio atakaeanza kujishitukia kwani namuonesha kuwa najuwa kinachoendelea halafu sitoomba mchezo kabisa na kwani sitoweza kumuamini tena ikiwa na ukimwi
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Hebu kaa chini ongea na mkeo, kwanini akufiche jambo kama hilo?
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,216
  Likes Received: 12,930
  Trophy Points: 280
  Mmmmh itauma kweli.lakini ndio hivyo watoto hao itabidi tu mvuniliane
   
 8. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama ndo hivi tutagongewa wake zetu kiulaini,

  kuoa nitafafikiria baadae
   
 9. Zambavuni

  Zambavuni Senior Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hello Janga kuu! Hayo ndiyo maisha ya ndoa ya kawaida yasiyo na chembe chembe za uwepo wa Mwenyezi Mungu. Si swala la pete kumeremeta wala heshima kwa majirani au wakwe, uwepo wa ukimwi n.k. Bosi wake anapesa, ni mke aliye mvaa Mwenyezi Mungu kwa kila sekunde ya maisha yake ambaye hataweza kuanguka kwa ajili ya pesa.

  Anatakiwa atambue kuwa Mungu hapendi uzinzi, na matokeo yake ni mabaya hasa yakiwemo kumdharirisha mume wake na hatimaye kuleta magonjwa ndani ya familia yatakayosababisha hao watoto wawili kubaki yatima. Kama ni wewe uliyeguswa usipaniki usije ukafa na BP bure na wala usijali sana watu wasema nini, Muombe mwenyezi mungu atakusaidia. Muite mkeo, kaa kitako, jadili kulikoni. Yawezekana wewe ndiye mwanzo wa matatizo.

  Kumbuka ndoa ni kama biadhaa nyingine dukani. ili iuzike yahitaji packing nzuri, matangazo ya mara kwa mara kutegemea na ushindani wa soko. soko likidolola unajipanga upya, waweza punguza size ya packing na kubadikisha rangi ya vifungashio yoteee hayo kuwavutia wateja waendelee kununua bidhaa yako. Mkisha tambua tatizo mwaweza sameheana na mkaanza upya na kumtanguliza Mwenyezi Mungu awe ndiye kiongozi wa maisha yenu.
   
 10. Zambavuni

  Zambavuni Senior Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Usisahau kupima VVU
   
 11. k

  kisukari JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  hii yote ni kuwa mnasema ndoa ya kanisani haina talaka,mwisho wa siku ndio kama hayo.kipo kilichomfanya huyo mke atoke,ingawa sio solution.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,075
  Trophy Points: 280
  Thank you GT.

   
 13. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  hahahaaaaaaaaaaaa, ulivyojibu hadi nahisi inakuhusu

  mhhh
   
 14. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Huyo mme ******* au? Yaani akubali mkewe akatafunwe?
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  kabla sijaanza kumlaumu huyo mke.... Humu si kuna wanaotetea nyumba ndogo? Sasa basi inawezekana huyo mke ni nyumba ndogo ya boss.....


  Anyway pole sana mkuu, inauma sana
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Pole sana, unaonekana umechanganyikiwa kabisa; tulia mkamishe chini mkeo sema naye ufikie maamuzi!
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Assume huyo mke ni SH ya The Boss na anayelalamika ni Asprin halafu mke wa The Boss ni SH ya Dark City hadi raha yaani!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Miaghay

  Miaghay JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  kwahiyo ilitakiwa mwanamke amweke wazi mmewe kwamba yuko likizo na kwamba huwa anaenda kumhudumia bosi?
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hahahahaha mtandao safiiiiiiii
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kamanda Moshi

  Kamanda Moshi JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,419
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  ushaamka mama?karibu kazini...!!
   
Loading...