Mke ammwagia mafuta ya moto mume na mtoto baada ya kupewa talaka

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Mohamed Maulid mkazi wa Pugu Kinyamwezi
ambaye ni mfanyakazi wa Tanesco na mtoto wake
Sumaiya Mohamed (3), wamemwagiwa mafuta ya
moto na mke wake (Severine) baada ya mke huyo
kupewa talaka siku mbili kabla ya tukio hilo. Maulid alisema baada ya kumpa mwanamke huyo
talaka alikuwa anampiga tu tarehe kuwa
‘ntaondoka kesho, ntaondoka kesho.’ “Na
nilivyokuwa naenda kazini nilimuuliza utaondoka
saa ngapi akasema ataondoka jioni, nikahisi
kwamba anaona aibu kuondoka mchana ataondoka jioni,” amesimulia. “Nilikuwa nimelala nikasikia kama moto
umelipuka, nilikuwa nimelala fofoFo, nikashtuka
nikaanza kupiga kelele nimemwagiwa maji ya
moto nikapiga kelele majirani wengine wakanisikia
wakatoka nje, wakaenda kumuangalia na mtoto
wakakuta na mtoto naye kaungua sana na yupo kule wodi ya watoto.” Baadaye majirani wakanisaidia wakamuita dereva
taksi nikawaambia nikimbizeni hospitali kwa uzima
wangu. Mimi nilipomwagiwa mafuta yale,
nilikurupuka nikakuta mlango upo wazi na wakati
mlango nilikuwa nimefunga nimefunga na
misumari kwasababu nilikuwa simuamini tena kwanini hataki kuondoka, nikakuta mlango ule
umefunguliwa na wa nyuma umefunguliwa na
mtoto wangu alimwagiwa mafuta kichwani
nilimuona.” Jirani yao aliyejulikana kwa jina la Sofia Ngumbali
alisema, “usiku mwanamke huyo alienda jikoni
kuchemsha mafuta na akapanga viti akarukia
chumba cha mumewe kufika pale mlangoni kwa
kuwa funguo alikuwa hajaichomoa akafungua
mlango na akachukua mafuta akaja kuwamwagia yeye na mwanae waliokuwa wamelala pamoja.” “Yule mwanaume alivyokurupuka akapiga kelele
majirani tulijua mwizi kukurupuka tukamkuta
anagalagala nje anasema kuwa mkewe
amemmwagia mafuta, na sisi tulikuwa tunaona
wanaishi kwa amani wakitoka wanatoka wote na
kurudi wote kwahiyo ya ndani mtu huwezi kujua yaliyopo ndani ya ndoa,” aliongeza jirani huyo. Kwa upande wake mama wa mtuhumiwa huyo
akiwa na mjukuu wake katika hospitali hiyo
aligoma kutoa ushirikiano alipokuwa akihojiwa na
waandishi.
SOURCE: bongo5
 
balaa stress , hakuna mazungumzo ya suruhu , kesho yake itakuwaje , kiufupi ni ngumu kumeza na kutema pia pole yake sana , wote baba , mama na mtoto
 
Back
Top Bottom