Mke amkata ulimi mume wakibusiana............................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke amkata ulimi mume wakibusiana...............................

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Dec 9, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Mke amkata ulimi mume wakibusiana

  Wednesday, 08 December 2010 18:53 newsroom
  LONDON, Uingereza
  MWANAUME mwenye umri wa miaka 79 ameng’atwa hadi kukatwa ulimi na mkewe, wakati akimpa busu la kumtakia usiku mwema.
  Habari zilisema mume huyo Willard Luenders, baada ya kukatwa ulimi aliweza kumunyamunya maneno na kuita gari la wagonjwa. Luenders anaishi Wauwatosa, Wisconsin. Taarifa zilisema baada ya Luenders kufikishwa hospitali, madaktari walihitaji kipande cha ulimi kilichokatwa kwa ajili ya kukirejesha mahali pake. Hata hivyo polisi walipofika nyumbani kwa Luenders, Karen (57), alikataa kuwaruhusu polisi hao kuingia ndani ya nyumba, ambapo alichukua kahawa ya moto na kuwamwagia.
  Taarifa zilisema polisi hao walitumia nguvu kuingia ndani na walifanikiwa kukipata kipande cha ulimi kilichokatwa na Karen, walikichukua na kukipeleka hospitali kwa ajili ya kujaribu kukirejeshea kwa Luenders. Msemaji wa polisi Terry Meyer alisema wanandoa hao kabla ya kung’atana ulimi walikuwa wakiimba nyimbo za krismas, huku wakiwa kwenye hatua za kwenda kulala. Alisema Luenders aliamua kumpa mkewe busu la kumtakia usiku mwema, lakini Karen aling’ata ulimi na kuukata kipande. Meyer alisema Karen amekamatwa na amefunguliwa mashitaka ya kufanya vurugu nyumbani, na pia imeamuliwa akapimwe akili. Luenders katika taarifa yake ya maandishi polisi, alielezea tukio lilianza wakati yeye alipokuwa akienda bafuni na mkewe alikuwa akienda chooni. Alisema alipojaribu kumbusu mkewe alishangaa kushikwa sehemu nyeti na kung’atwa ulimi hadi kutatika kipande. Luenders alisema katika siku za karibuni mkewe amekuwa akifanya vitu vya ajabu, ikiwemo kuzungumza mambo ya mizimu.
   
 2. Ras

  Ras Senior Member

  #2
  Dec 9, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!!! hii inatisha man!!:faint::target:
   
Loading...