Mke aliyenikimbia anataka kuninyang'anya mtoto!! Your advice pls!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke aliyenikimbia anataka kuninyang'anya mtoto!! Your advice pls!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by GAMBLER, Dec 21, 2009.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanajamii, nakupeni story fupi ya maisha yangu, mwaka wa pili baada ya kuzaa na mke wangu,aliniambia kuwa hataweza kuishi na mimi kwa kuwa sina kipato kizuri,akaondoka na kuniachia mtoto wa kiume wa miaka 2, kupita mwaka akataka nimpe talaka yake,kwa kuwa tulifunga ndoa kiislamu, nikampatia talaka yake kwa njia hiyo, sikwenda mahakamani.Mtoto nimemlea toka ana miaka 2 mpaka sasa ana miaka saba yuko grade two. Sasa hivi amenipigia simu ameniambia kuwa anataka kumchuka mtoto, na ameniambia kuwa hata kama sitampa mtoto atamchukua kinguvu amlee yeye, sasa naombeni ushauri wenu kuhusu mtoto anapofikisha miaka 7, nani ana haki ya kumtunza mama au baba? pia mnanipa ushauri gani nifanye kuhusu hili tatizo? nitashukuru sana kwa msaada wenu..
   
 2. tovuti

  tovuti Senior Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana ndugu kwa matatizo, huyo mke hakuwa na upendo, kuhusu masuala ya ushauri wa kisheria, mimi si mtaalamu sana, lakini humu kuna wataalamu utapata ushauri mzuri tu
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  naona huyo ameona chambichambi ''zimerejea'' ANATAKA KURUDISHA TIMU!stuka mpwaa:D
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  just LISTEN TO YOUR HEART!unajua zile zama za kushauriana ACHANA NAE SIJUI NINI ZIMEPITWA NA WAKATI!

  usikilize moyo mkuu
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mazee umecheza ndivyo sivyo, kwa kanuni za Bluray, ikibidi mama na baba kutengana, na kuna uhusiano wa mtoto mdogo,basi mama anachukua mtoto mpaka umri wa kati ya miaka 7- 11, na baada ya hapo, kwa mujibu wa vitabu vya mtume Bluray, ni halali kwa baba kuchukua mtoto kumlea mpaka akiwa na miaka 18, hususan kama ni mtoto wa kiume. Baada ya hapo ni halali kwa mtoto kuanza kivyake kujitafutia mwenyewe, akiwa na contacts na wazazi wake wote wawili throughout.

  Sasa wewe umelea mtoto mdogo na aanafikisha umri sasa mama anamtaka. Ungemwachia tangu mchanga labda ungekuwa na chance sasa.
   
 6. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Geoff, hata mimi nimepatwa na hayo mawazo, kwa sababu miezi 3 ilopita niliagiza gari kutoka japan
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kuna tofauti kati ya kutunza mtoto na kukaa na mtoto. Mtoto anaweza bado akakaa na mama yake lakini ukawa wewe (au ninyi wote) mnamtunza: kwa mahitaji yake muhimu. Au anaweza kukaa kwako na mkaendelea kumtunza wote.

  Katika suala lako inaonekana mama mtoto anataka kumchukua mtoto aende kukaa naye lakini uendelee wewe (bila shaka na yeye mama) kumtunza akiwa kwa mama. Kama ni suala mtoto akae kwa nani, naona unaweza kumpatia akakaa naye ukawa unapeleka matumizi. Shida ni kwamba kama anakaa mbali inabidi kumhamisha mtoto shule anayosoma, jambo ambalo ni usumbufu. Vinginevyo sidhani kama anaweza kukunyang'anya mtoto. Huyo ni wenu wote. Kila mmoja ana haki naye.
   
 8. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekupata mkuu, mtoto namtunza mimi.., naomba unifafanulie kuhusu sheria za nchi kama unazijua, mtoto akifikisha miaka 7 nani anapaswa kumlea na kumtunza. baba au mama
   
 9. tovuti

  tovuti Senior Member

  #9
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wadau, mimi naona hoja muhimu anayouliza huyu jamaa, ni kuwa mtoto akifika umri gani anatakiwa atunzwe na baba?
   
 10. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sema ni umri gani anapaswa kukaa na baba: kwa sababu kama ni matunzo mtoto anatunzwa na baba yake tangu akiwa mchanga. Ila kama wazazi wametengana atakaa kwa mama, na baba atapeleka mahitaji, yaani ataendelea kumtunza. Akishakua anaweza (si lazima) kwenda kuishi na baba yake.
   
 11. tovuti

  tovuti Senior Member

  #11
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa nimekupata, umesema akishakuwa anatakiwa akae kwa baba, umri gani unahitajika akishakua?
   
 12. tovuti

  tovuti Senior Member

  #12
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  imeeleweka??
   
 13. b

  bnhai JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mie naona bora umwache kwa mama yake maana wewe upo addicted na kamari na pia sasa hivi unayule wa Mombasa.
  Inaonekana upo busy na unamambo mengi muache mtoto akalelewe na waleaji
   
 14. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Soma sehemu hii ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kuhusu utunzaji wa mtoto mambo ya wanandoa yanapokwenda kombo:

  (h) Custody and Maintenance of Children
  125-(l) The court may, at any time, by order, place an infant in
  the custody of his or her father or his or her mother or, where there
  are exceptional circumstances making it undesirable that the infant be
  entrusted to either parent, of any other relative of the infant or of any
  association the objects of which include child welfare.
  (2) In deciding in whose custody an infant should, be placed the
  paramount consideration shall be the welfare of the infant and, subject
  to this, the court shall have regard-
  (a) to the wishes of the parents of the infant; and
  (b) to the wishes of the infant, where he or she is of an age to
  express an independent opinion; and
  (c) to the customs of the community to which the parties belong.
  (3) There shall be a rebuttable presumption that it is for the good
  of an infant below the age of seven years to be with his or her mother
  but in deciding whether that presumption applies to the facts of any
  particular case, the court shall have regard to the undesirability of
  disturbing the life of an infant by changes of custody.
  (4) Where there are two or more children of a marriage, the court
  shall not be bound to place both or all in the custody of the same
  person but shall consider the welfare of each independently.
  126.-(1) An order for custody may be made subject to such
  conditions as the court may think fit to impose, and subject to such
  conditions, if any, as may from time to time apply, shall entitle the
  person given custody to decide all questions relating to the upbringing
  and education of the infant.
  (2) Without prejudice to the generality of subsection (1), an order
  for custody may-
  (a) contain conditions as to the place where the infant is to reside,
  as to the manner of his or her education and as to the religion
  in which he or she is to be brought up;
  (b) provide for the infant to be temporarily in the care and control
  of some person other than the person given custody;
  (c) provide for the infant to visit a parent deprived of custody or
  any member of the family of a parent who is dead or has been
  deprived of custody at such times and for such periods as the
  court may consider reasonable;
  (d) give a parent deprived of custody or any member of the family
  of a parent who is dead or has been deprived of custody the
  right of access to the infant at such times and with such
  frequency as the court may consider reasonable; or
  (e) prohibit the person given custody from taking the infant out of
  Tanganyika.
  127. (1) The court may, when granting a decree of separation or
  divorce or at any time thereafter, on the application of the father or
  the mother of any infant of the marriage, or where the father or
  mother is dead, on the application of a relative of the deceased parent,
  make an order declaring either parent to be a person unfit to have the
  custody of the infant and may at any time rescind any such order.
  (2) Where an order has been made under subsection (1), and has
  not been rescinded, the parent thereby declared to be unfit shall not, on
  the death of the other parent, be entitled to the custody of such infant
  unless the court otherwise orders.
   
 15. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nakushauri uende kwenye ofisi za ustawi wa jamii watakusaidia kisheria!
   
 16. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  umesema vema.
  huyu mwanamke nahisi yuko kibiashara zaidi maana kwa miaka mi5 hakufuatilia maendeleo ya mwanae sasa ana miaka 7 ndo anamtaka? kwa kipindi kile mtoto anamuhutaji zaidi alikuwa kwa wenye hela sasa kasikia mzazi mwezie kaagiza gari ndo anajisogeza!
  kwa ninavyojua mimi wanandoa wakitalikia mtoto akiwa under 7 anakaa na mama, akifika 7 baba anaweza kaa naye.
   
 17. f

  furahaeliud Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kisheria mtoto anaweza kutunzwa au kulelewa na baba kuanzia miaka 7 lakini kwa kesi yako yeye alimtelekeza tangu akiwa na umri ambao anatakiwa kutunzwa na mama so kwa msingi huo bado wewe unahaki na bilashaka sheria itakufeva maadam uweze kuthibitisha kuwa alimtelekeza na mtoto wakati mnapeana talaka
   
 18. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kama alikuwa ana taka kweli kulea mtoto angemchukua akiwa mdogo, hata kama mambo hayakuwa mazuri kwa upande wake si angerekebisha kwanza au angekwambia atarudi baadae kumchukua?

  maadamu alikuachia basi na akuachie hivyo hivyo
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  huyu hataki mtoto tu!anamtaka na BABA WA MTOTO!mimi nawafahamu vizuri sana wanawake na tricks zao.nina experience na hii kitu
   
 20. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mtoto hagombaniwi kabisa,mtoto ni zawadi kutoka kwa mungu sasa kulingana na matakwa ya mama kama anataka mwanae basi apewe na wewe kama baba mpe pesa ya matumizi wala usijali nini au watu wanasemaje kwani mama ndio mlezi wa watoto..sisi ni wasaidizi...mtoto lazima akuwe na atakutafuta baba yake ilo lazima ujue...hakuna mtoto asiyetaka kujua asili yake wapi.
   
Loading...