Mke alihama chumba, nimechukua msichana wa kazi, kuna kosa hapo?

dedan kimathi

Member
Dec 5, 2015
42
24
Nawasalimu wote,

Tangu mwezi February mwanzoni tumekuwa na mgogoro na mke wangu, mgogoro huu ulitokana na yeye mke kupoteza pesa zake za mkopo kiasi cha tshs million sita katika mazingira ya kutatanisha, akadai mimi ndie nimechukua pesa zake, tulipoitwa kwenye usuluhishi niliona niliona ni udhalilishaji hivyo nikagomea vikao vyote

In retaliation akaamua kuhama chumba na kwenda kwa watoto,
hivyo February yote sikupata matrimonial right na March yote pia sikupata.Baadae nikagoma kula chakula chake baada ya accurate intelligence information kuwa kuna dawa kama unga unga hivi huwa anadumbukiza kwenye chakula nilichoandaliwa mimi na mara zote msichana wa kazi hukimwaga kile chakula na kuniandalia kingine, kesho yake wife humuuliza msichana wa kazi baba alikula kile chakula? Pia ameonekana akibeba nguo zangu kadhaa ikiwemo boxer na kuondoka nazo, alipohamia kwa watoto hakubeba nguo zake hivyo kila asubuhi huja kuchukua master bedroom maana ana funguo zake.

Sasahivi sili nyumbani na nguo natembea nazo kwenye gari, mwezi huu wa nne ulipoanza nimehamia chumbani kwa msichana wa kazi ndimo ninapoishi sasa, binti huyu amekuwa mwema kwangu na ananipenda kwa dhati, ni mzuri wa umbo na sura, in fact hakua msichana wa kazi ni ndugu katika ukoo wa mke, alikuwa amefeli form 4 hivyo akaomba huo mshahara wa msichana wa kazi tumpe yeye atusaidie kazi wakati anasubiria mambo yake yakae sawa.

Mke ameniletea watu wa serikali ya mtaa waje wamtoe yule binti, maana nilipohamia chumbani kwa binti, mke alitufanyia fujo isiyosemekana, kwamba binti aondoke, sasa mimi ningeishije wakati mke amehama chumba?
Sasa nafanya utaratibu nimtafutie chumba mtaani, huyu binti ana adabu na ni God fearing tofauti na mke wangu anaejifanya mlokole wakati anataka kunidhuru na madawa.

Naombeni mwongozo wenu katika kukabiliana na jambo hili, na pia mniambie kama nimekosea katika kulishughulikia suala hili.
 
Inamaana wewe kama kichwa cha familia umeshindwa kabisa kurudisha heshima ya ndoa yako mpaka uhamie kwa mwanamke mwingine?

Yani unatembea na nguo kwenye gari kisa hutaki kujishuhulisha ndoa yako isimame?!

Hebu acha kupenda kitonga bana,jitahidi kurudisha ndoa yako
 
Katika mabwege ww namba moja.,Kumetokea upotevu wa pesa ndani..,umekuwa suspect no 1.,kwann ukataae vikao..?,Ninapokuona sio ni badala ya kukaa chini upate suluhu unajisifu eti umehamia kwa house girl..,Kama kweli ww mwanaume hama nyumba sio huo utoto unaoufanya bro...,Kulala na House girl ni sawa na kulala na Mwanao wa kike uliyemzaa kaka...,Kaa chini Jitafakari sana huo sio ujasiri Umepotea na Unazidi kuangamia
 
Ni rahisi kudai hivyo tatizo likiwa la mtu mwingine, sio rahisi kiasi hicho kama vile kuzima na kuwasha taa ukutani, ni Bahati mbaya sana sikutaka kuwaeleza ni kiasi gani nilihangaika kumbembeleza mwenzangu kuwa anakoelekea sio kuzuri, nilimweka Chini na kumweleza madhara ya huu mgogoro kama tutauacha uendelee hivi

Pia mwanamke mwenye busara hawezi kuhama chumba chake cha ndoa sababu ya kupoteza fedha, ni bora ingekua sababu ya uzinzi ningeelewa
Nilidhani angekaa kwa watoto siku mbili akarudi kwetu, amekaa miezi miwili na alikua na nia ya kuendelea

Nashukuru kwa ushauri wako unfortunately umekua one sided
 
Unfortunately you are far away disconnected from reality of this particular matter, therefore am not going to blame you young broda, stay blessed
 
Ni rahisi kudai hivyo tatizo likiwa la mtu mwingine, sio rahisi kiasi hicho kama vile kuzima na kuwasha taa ukutani, ni Bahati mbaya sana sikutaka kuwaeleza ni kiasi gani nilihangaika kumbembeleza mwenzangu kuwa anakoelekea sio kuzuri, nilimweka Chini na kumweleza madhara ya huu mgogoro kama tutauacha uendelee hivi

Pia mwanamke mwenye busara hawezi kuhama chumba chake cha ndoa sababu ya kupoteza fedha, ni bora ingekua sababu ya uzinzi ningeelewa
Nilidhani angekaa kwa watoto siku mbili akarudi kwetu, amekaa miezi miwili na alikua na nia ya kuendelea

Nashukuru kwa ushauri wako unfortunately umekua one sided
Umejaribu kwenda kwa wadhamini wenu na kuita watu wazima waongee nae?
 
Amemwaga mboga we umemwaga ugali :D
labda kama anatoka katik yale makabila yanayoruhusu kuoa ndugu wa mkeo. Vinginevyo ni AIBU kubwa kulala na HG hata ndugu wa mkeo.UTUELEZE KAMA KWENU HII INARUHUSIWA? Huku kwenye fb mbona tutsikia vituko vingi. Ondoa huyo HG kwanza kama haujafanya kinyume na mila zenu. Vinginevyo naona wwe na wife mkubaliane kuwa kuna mwenzie kimila au kidini
 
Back
Top Bottom