mke akiwa ni HIV+ na mume ni -ve inakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mke akiwa ni HIV+ na mume ni -ve inakuwaje?

Discussion in 'JF Doctor' started by rakeyescarl, Aug 2, 2011.

1. r

rakeyescarl JF-Expert Member

#1
Aug 2, 2011
Joined: Dec 9, 2007
Messages: 408
Likes Received: 9
Trophy Points: 35
Wakuu Salaam, naomba ushauri:
Hivi hapo kama ndoa ni ya kikristo i.e mme 1 na mke 1 na kwa bahati mbaya husband hana hivi kuna njia salama ya kuendelea kujamiiana au ndio mzee inabidi ubadilike kuwa paroko?Maana kuoa haiwezekani na kuzini hairuhusiwi.
Nimeshindwa kumjibu mwenye tatizo hilo,
Nawakilisha,
Asanteni.

2. Pdidy

Pdidy JF-Expert Member

#2
Aug 2, 2011
Joined: Nov 22, 2007
Messages: 33,249
Likes Received: 5,631
Trophy Points: 280
Na yeye amgaiye positive ujasoma hesabu - jumlisha + =si + so aamue ajaribu kumpa negative lakini hesabu nilizosoma + n mshind

3. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#3
Aug 3, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
'Discordant couples' ni challenge kubwa sana kijamii kwa watu wanaoishi na VVU. Inatokea kwa wote (Mwanamke +ve na mwanaume -ve, au mwanamke -ve na mwanaume +ve). Hii ya mwanamke +ve na mwanaume kuwa -ve ndio common sana, na ni kwa sababu ya kimaumbile...mwanamke yuko katika risk kubwa ya kupata maambukizi toka kwa mwanaume mwenye ugonjwa kuliko mwanaume kupata toka kwa mwanamke mwenye ugonjwa.

Mwanamke huko ndani ukeni kuna ngozi laini ambayo ni rahisi kuchubuka ikisuguliwa na uume ambao kwa kawaida ngozi yake ni ngumu (hasa kama mwanamke ni mkavu au hakutayarishwa), na pia mwanaume anaacha manii zenye virus ndani na zinakaa kwa muda hivyo vijidudu vinapata muda wa kuingia mwilini, tofauti na mwanaume ambaye kipindi pekee anachoweza kuambukizwa ni wakati uume uko ndani ya uke.

Mara nyingi inakuwaga vigumu kwa partner ambaye hajaambukizwa kukubaliana na hiyo hali (hasa wanaume, katika experience yangu ya kudeal na discordant couples nimeona hili), hivyo mara nyingi wanatafuta 'alternative'. Wengi wanaobaki ni wale ambao issue inakuwa imevuja mtaani kuwa mmojawapo ana 'ngoma' hivyo watu wanamuogopa na hapati partner hivyo inabidi tu arudi kwa partner wake muathirika.

Kisayansi kuna njia za kuzuia maambukizi kwa partner ambaye hana VVU, na pia njia za kupunguza sana tu uwezekano wa kumuambukiza mtoto iwapo wataamua kuzaa. Kiukweli, japo ngumu kijamii...mmoja kati ya partners kuwa na VVU sio sababu ya msingi ya kuachana, na kanisani sijui kama watatoa 'go ahead' ya kuvunja ndoa..and so is the court of law (labda wanasheria mtusaidie kama kuna sheria ya kuvunja ndoa kama mmojawapo amepata maambukizi).

Kumbuka maambukizi ya VVU sio lazima iwe kwa ngono kusema kwamba 'infidelity' is the issue there, it is difficult to prove beyond reasonable doubt kwamba huyo partner amepata VVU kwa kutoka nje ya ndoa, japo inaweza ikawa so obvious ukiangalia kijuu juu!

4. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#4
Aug 3, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
riwa asante kwa uchanganuzi. rakeyescarl, kwa issue kama hiyo wanahitaji counseling ili wajue wataishije. kuna some limits, lakini wanaweza kujamiiana kwa kutumia condoms wakati wote. ila ushauri wa kitaalamu ni wa muhimu, waambie waende vct. tbc1 waliwahi kuonesha couple moja, mwanamke alikubali kuolewa na jamaa+ wakazaa 3 kids. she is still -ve.

5. BAK

BAK JF-Expert Member

#5
Aug 3, 2011
Joined: Feb 11, 2007
Messages: 70,496
Likes Received: 81,820
Trophy Points: 280
Je, wanaweza kulana denda au itaongeza probability ya yule ambaye ni -ve kuambukizwa?

6. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#6
Aug 3, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
bak, mate yana uwezekano mdogo sana wa kubeba vimelea vya hiv. inategemea pia na hali aliyonayo huyo mwenye virusi. risk inaongezeka endapo ana vidonda ama magonjwa nyemelezi kama fungus za mdomoni. inahitaji constant monitoring kwa kweli. na isitoshe, pale ambapo kuna accidental exposure kuna kitu inaitwa prophylaxis ambayo ni combination itakayohakikisha aliyeko salama hapati maambukizi baada ya ajali. by the way, siku ukiuza mechi mchangani wahi kwenye kituo kabla masaa 72 hayajapita utapata hii huduma ya kukulinda.

7. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#7
Aug 3, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Thank you King'asti kwa ushahidi...mara nyingi wanaume wanakulaga kona. Ni wanaume wawili tu kati ya discordant couples karibu 30 nilizowahi deal nazo walibaki na partner. Kuna mmoja mkewe aligundulika baada ya kujifungua, aliumwa sana..mumewe alikuwepo 24/7 akimhudumia mama na mtoto mchanga japo ndugu walikuwa wanachonga mpaka kutaka kunihonga kama Daktari nimshauri ndugu yao aachane na huyo mama, nikawatimua kama mbwa! unfortunately yule mama alifariki kama miezi 7 baadae, jamaa is my friend mpaka sasa, he is still -ve and thank god the kid is now 4 years and -ve!

Couple nyingine walikuwa walokole walitaka kuoana, mdada akawa +ve na mkaka -ve....lakini huyu mkaka jasiri alikubali kumuoa akiamini yesu atawapigania..akaoa na nikawafuatilia wakifuata masharti na aliendelea kuwa -ve kwa miaka mi2, then wakataka kuzaa...nikawashauri wafanya in-vitro fertilization (IVF), yai linarutubishwa bila tendo la ndoa...kaka akakataa, akasema atampa mkewe ujauzito kwa njia ya asili (tendo la ndoa), series of counselling zikashindwa kutokana na imani yake ya kiroho. Akajaribu kumpa mimba mkewe lakini haikuwa rahisi kihivyo, wakarudia na kurudia, na miezi 6 baadae kaka akawa +ve. Tulipompa majibu alichanganyikiwa na akapotea sikumuona tena clinic, na jitihada zangu kumtafuta kwa contact nilizokuwa nazo hazikuzaa matunda...it is one of my saddest story in practising clinical medicine.

It is a challenge kwa kweli, hasa linapokuja suala la kuzaa. King'asti hiyo couple yako watianaje mimba 3?

8. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#8
Aug 3, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
bak, ila kula magadi ni no-no! i mean big NO!

9. BAK

BAK JF-Expert Member

#9
Aug 3, 2011
Joined: Feb 11, 2007
Messages: 70,496
Likes Received: 81,820
Trophy Points: 280
Dr Riwa inahitaji uwe na roho ngumu sana kubaki na mwenzio pale anapogundulika kwamba ni muathirika. Nimeshasikia waathirika wengine hutoa hata ruhusa kwa yule ambaye si muathirika kwenda nje ya ndoa ili kuweza kutimiziwa matamanio yao ya kimwili. Hii kitu pamoja na kuwa kuna dawa za kurefusha maisha inatisha sana kusema kweli.

10. Janja PORI

Janja PORI JF-Expert Member

#10
Aug 3, 2011
Joined: Jul 31, 2011
Messages: 808
Likes Received: 50
Trophy Points: 45
me i got ths frnd of mine wamekaa na demu miaka sita bt Men Ni -tive and the gal+positive the guy anataka kuoa mke _tive bt stil anampenda +tive one

11. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#11
Aug 3, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
this is one sad story! mara nyingi, pamoja na imani kuwa ya muhimu inaweza kupotosha wengi. sio kila mlemavu na kiwete aliyekuwepo wakati Yesu anatenda miujiza alipona. 2 wks ago amefariki my very close frnd kwa hiv wakati anamalizia phd yake! aligoma kutumia arvs kwa sababu za kiimani! it was such a waste of resource kwa kweli,manake alikuwa kama herbarium,lol!
that couple hawakusema kama walitumia njia gani coz it was on tv. waliongelea 'ushauri wa kitaalamu'tu. lakini nadhani zaidi ya avf hakuna muujiza mwingine. kwa sababu hiv zinakaa kwenye manii (majimaji yanayotumika kusafirisha mbegu). hivyo mbegu zikiwa separated kitaalamu na kupandikizwa kunakuwa hakuna maambukizi
aisee riwa, pole sana. urs is an emotional job. nilijihusisha na ushauri nasaha kwa kipindi tu na nikapata depression ya ajabu! had to quit. anyway umri pia ulikuwa tatizo na nilikuwa sijui matatizo ya duniani,lol!

12. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#12
Aug 3, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
mshauri asioe mke mwingine. hakuna kitu kibaya kama kukosa furaha maishani. kama anapata furaha kuwa na huyu, waendelee kukaa pamoja. kuzaa sio issue tena, watapata watoto wazuri wasio na virusi na maisha yataendelea. akimpa support mkewe anayohitaji kutumia dawa wataishi maisha mazuri kwa muda mrefu. na one of the side effects za hizi dawa ni kuwa mtumiaji ana-collapse tu, hakuna mateso ya muda mrefu. makes it less emotional

13. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#13
Aug 3, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
bak, hizi dawa za kurefusha maisha zinasaidia sana lakini zinahitaji support kubwa sana kutoka kwa jamii nzima! tatizo lenu wanaume wetu wa kiafrika tunawapenda sana lakini ni wabinafsi sana! mwanaume hata akipata dsyfunction tu, ndo wivu na kuhakikisha anabana mkewe asitoke nje. ila yeye akiwa na tatizo anaona ni haki yake kuvumiliwa etc. inatisha kweli, lakini kwenye upendo hakushindikani kitu aisee. i wish kungekuwa na kipimo kama upendo count au litmus flani hivi tujihakikishie b4 kuuvaa mwamba,lol

14. r

rakeyescarl JF-Expert Member

#14
Aug 3, 2011
Joined: Dec 9, 2007
Messages: 408
Likes Received: 9
Trophy Points: 35
Asanteni wadau wana JF,nioneeni huruma na muoneni huruma Mzee ambaye ni -ve,baada ya kumpa printed comments Zenu hapa na contacts za Dr.Riwa na King'asti,si akamwaga kilio- kweli kweli,namuuliza ni nini? rafiki hakusema lolote, anaishia kusema why me, ndio nilichoambulia na hakusema tena akaingia bedroom nikaondoka-hii dunia,hiiiii.
Tuombeane tu. Labda what I did was wrong labda sikupashwa kumpa asome ilibidi nitafute maneno laini zaidi?Maana personally niliona yamesemwa in a friendly way-kilichomliza sikukijua,ASANTENI SANA.

15. M

Manyiri Member

#15
Aug 3, 2011
Joined: Oct 27, 2007
Messages: 73
Likes Received: 1
Trophy Points: 15
Kuna mtu wa karibu yangu sana ameish na mke wake kwa miaka 8 na wamezaa mtoto hawajawah tumia kondom lakini mme ni negative mke ni postive na mtoto ni negative

16. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#16
Aug 4, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
Rakeyescarl, pole sana. NNi kitu ambacho kiko emotional sana. mshauri asijitenge wala kukaa peke yake. mwanzoni ataona ngumu sana, lakini muda unavyosonga ataweza kukubali hali na kuishi nayo. kila mtu anayepitia irreversible situation hujisikia hivyo. muambie amfikirie zaidi mkewe, ambaye anakabiliwa na mtihani mzito. upendo haujitangulizi. mnahitaji kuwa karibu na huyo mama, anahitaji urafiki na mapenzi yenu pia. yeye kwa kumsaidia mwenzie atajikuta anapata faraja.

17. Riwa

Riwa JF-Expert Member

#17
Aug 4, 2011
Joined: Oct 11, 2007
Messages: 2,601
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Pole sana Rakeyescarl...hii kitu haiko easy kama tunavyojadili hapa, ni kwamba hayajatukuta tu..tunaweza hata sisi tunaotoa ushauri huu, japo ni sahihi kabisa na tunajua hivyo...yakitukuta tukareact differently.

Anahitaji support rafiki yako...na kwa kweli anahitaji kuanza kwenda kwenye counselling sessions na huyo mpenzi wake. Nadhani hajawahi kwenda naye, au labda alikuwa ana uamuzi wake kichwani ambao alikuja hapa kupata 'go ahead' na kashuriwa tofauti. Ila ukweli ni kuwa, alichoshauriwa hapa kinatokana na facts ambazo zipo kisayansi (king'asti amecopy malink kadhaa kwenye hii thread anaweza soma zaidi).

Your friend needs you, and the good way for being there for him is not to tell him what he wants to hear...but to tell him the facts, and help him to deal with it. Mshauri awe anafuatana na mpenziwe kwenda kwa washauri nasaha.

18. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#18
Aug 4, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
manyiri, miracles do happen bt u cant just rely on them. inawezekana wana tatizo la viasili ambalo linawazuia kuambukizana. tunaweza kuwafanyia study...

19. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#19
Aug 4, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,507
Likes Received: 2,248
Trophy Points: 280
natamani kuwakumbusha stori hii ya mtu aliyepona ukimwi. alikuwa na sickle cell anaemia na aids pia. wakaamua kumfanyia bone-marrow transplantation ( ni process ngumu na ya ghali kweli, hata india sidhani kama wanafanya). lakini walimchukua donor ambaye ana genetic disorder, hana binding factor inayokubali kirusi cha hiv (ili kirusi akushambulie white blood cells zako anahitaji mahali pa kujibandika ambapo ni specific). wakamuwekea mgonjwa hiyo bone marrow, ambapo ndio kiwanda cha kuzalisha damu mwilini ila yenye upungufu. baada ya muda jamaa akawa hana hiv. so, kama kwenye human race itawezekana kuambukizana hiyo disorder itakuwa adaptive character dhidi ya hiv. tatizo la sayansi ni kuwa:
1 haijajulikana kama ina madhara gani kukosa hiyo binding factor.
2 huyu jamaa anaweza kubeba hiv na kuambukiza kwa watu wengine (kuwa vector) kutegemeana na dose ataayokuwa nayo mwilini kwani yeye hadhuriki

20. r

rakeyescarl JF-Expert Member

#20
Aug 4, 2011
Joined: Dec 9, 2007
Messages: 408
Likes Received: 9
Trophy Points: 35
Riwa,
Unajua shida yetu waswahili tumesihakuwa kama watu wa Europe/US lakini hatujna facilities.
Mtu Fundi unakuata anakwenda kuongea na mgonjwa bila hata elimu tunakuja hapa tunakkusanya vi info na kummwaga mgonjwa.
Hapo kwenye red mbona naona kiuswahili ni ngumu labda akawaone hao wanaotoa nasaha-wako wapi?

Loading...