Mke akikuzidi elimu,kipato penzi linaweza kudumu?

Mume ni kiongozi ndani ya nyumba kwa hiyo hata kama mke atakuwa na elimu zaidi, hela zaidi, akili zaidi. Mbona rais wa nchi anazidiwa elimu, akili, na uwezo wa kifedha na wananchi wengi tu na anaongoza fresh??
 
Inategemea na mwanamme vile vile,mwanamke unaweza kua na kipato cha juu na ukawa na adabu zako,mume ndioa akaanza vituko ukiuliza ndio anaanza ohh kwasababu wewe ndio unauwezo kuliko mimi hayaoni mapungufu yake......

Hapo umenena.naikubali sana hii
 
...mwanamke wa aina hiyo [mara nyingi] anakuwa amekuzidi na upendo wa kweli vile vile, chaguo ni lako!
 
Tatizo si nani anamiliki nini na nani kamzidi nani. Tatizo ni nani anatabia gani katika mahusiano.
Mwanamke au mwanamume kuwa na kipato kikubwa na elimu kubwa, lakini akawa ameikubali hali ya mwenzake na wakawa wanaishi kama mume na mke kwa mapenzi, heshima na mashirikiano, sioni kama kutakuwa na tatizo hapo. Tatizo litakuja ikiwa mwanamke/mwanamume huyo amelewa kipato na kuanza kumdharau na kumdharau, kumtesa na kumdhalilisha mwenzake.
 
Ukiliongelea mdomoni tu tatizo halipo ila kiundani lipo.Mwanamke si tu suala la mke na mume bali hata ktk jamii akiwa na elimu kubwa,kipato kikubwa wanajiskia sana,hata madaraka pia.Wenye mabosi wanawake wengi wao hawana furaha sana kama wenye mabosi wanaume.
 
Mimi kuzidiwa kipato na elimu sio tatizo.As long as the woman in question respects me and plays her role as a good wife is supposed to,no problemo.The relationship can be healthy,afterall i get to have someone who can help me in financial matters incase the downtimes kick in.

Ni ngumu sana kama mwanamke kakuzidi vyote hivyo kukuheshimu unavyotaka uheshimiwe.

Hii ni anecdotal observation yangu tu.
 
tatizo ni kwamba mwanaumme akiona amezidiwa kiuwezo na mke wengi wanajifeel inferior anaanza kuishi kwa kutojiamini na kwa kujidefend soo conflict zinaanzia hapo
kama mwanamme ataweza kurelax ndoa itadumu

Lipo tatizo Smile.Saikolojia ya wanawake ni tofauti sana na ya wanaume. Mwanamke akiwa na kipato kikubwa kuliko mumewe, ni nyodo tupu. Hiyo nyumba huyo mwanaume hatoweza kukaa. This is a general observation. Kuna baba niliyemfahamu alikumbwa na retrenchment ya miaka ile, akakaa nyumbani hana kazi. Mkewe alikuwa ameajiriwa na hakukumbwa na hiyo retrenchment. Bwana wee! we acha tu! Mama akifungua mdomo kuzungumza ni masengenyo tu. Ilibidi watoto waingilie kati kumwonya mama yao juu ya tabia yake ya kumsema baba. Baba akatafuta kazi akapata, na kilichofuata ni yule baba kuachana na mkewe. Hakuna binadamu hatari kama mwanamke mwenye pato kubwa kumshinda mumewe, Naomba niseme kwa herufi kubwa! Na kwa kiasi fulani mimi mwenyewe yalishanikumba; ntaeleza kwenye thread nyingine siku mwafaka.
 
Back
Top Bottom