Mke aja juu kubadilishwa jina na mumewe...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Nimesoma mahali fulani mama mmoja baada ya kuolewa siku moja akakuta barua na nyaraka mbalimbali zote zimebadilishwa kuwa Mrs. Rose Pesambili - Pesambili likiwa jina la ubin la mume wake. Mume aliporudi siku moja ukawa ugomvi.. kwanini amembadilisha jina lake bila kumuuliza na kwanini hata initials zikawa za mumewe..

Mwisho wa siku mke akafanya mgomo "baridi" kwani alisema kikabila cha kwao wao wanaitwa majina ya wazazi wao. Huyo mama ni Mngoni na kwao wanaitwa "Nakomba" yaani binti ya Komba. Alidai kuwa kuchukua jina la mumewe ni tamaduni za wazungu. "Kwa kuolewa mtu haachi kuwa binti ya babake" alinukuliwa kusema dada huyo.

Mume hakujua afanye nini kwani aliamini kuwa ndio kawaida "siku hizi"...

Mgomo baridi unaendelea...
 
nimevutiwa sana na huu mgomo baridi nifafanulie ni kwenye maeneo yepi............................isije jamaa yangu ananyimwa haki zake za kimsingi.........
 
Mwanakijiji umeanza,lol! Mgomo gani huo unaoendelea usio na athari kwa huyo mama pia?
 
kama ningekuwa mimi wala nisingemsumbua hata kidogo..ningemkubalia atumie jina lake bila tatizo lolote...hii ni dhana tu ..ya kumbadilisha mwanamke jina ila kama mtu ni muelewa hakuna ulazima ...obey your thirst
 
mume : david pesambili
mke: rose nkomba
baada ya ndoa: rose pesambili

hivi wewe mume ndo umemzaa huyo mke?

ila ni "uanaume " tu unafanya kutaka mke atumie ubini wako, wengine wanadai ndo inaongeza mapenzi. lakini haizidishi wala haipunguzi kama mke anakupenda anakupenda tu atumie jina la mume, la baba yake hata la mjomba wake it doesnt make any difference

"Mgomo baridi" haifanyi kazi siku hizi ..
we lete huyo mgomo ye ana leta vinjemba vidogo vina fanana na yeye
.
. ..
 
Haya mambo yameanza juzi juzi tu, Enzi za mwalimu kulikua hakuna ubishi baada ya ndoa tu jina linabadilika. Siku hizi ndo ni "very risk", sasa wanaona watabadili jina mara ngapi? Leo Pesambili baada ya miezi umeachwa waolewa tena unakua Mrs Karata and the list goes on!
 
Kazi kweli kweli. Sio lazima kuchukua Surname ya Mwanamme lakini pia mgomo baridi sio suluhu
 
Hapa naona kuna tatizo kwa pande zote mbili. Kwa upande wamwanaume ndio tatizo limeanza kwani yeye kiustaarabu alipaswa kujadili suala hilo na mkewe kwa hiyo angejua kilichopo moyoni mwa mkewe bf hajabadili jina hilo.

Kwa upande wa mwanamke tatizo lake ni kuendeshwa na mila bila kujali mabadiliko kwani mtu ukisha olewa jina la ukoo linabadilika once unakuwa ukoo wa mwanaume, sasa ni makubaliano baina ya wanandoa hao kuona kama kuna umuhimu wa kubadili jina la mwanamke au la, wakikubaliana mwanamke aendelee kutumia jina la ukoo wake fine au wakikubaliana abadili na kuitwa ukoo wa mwanaume fine, ni suala la makubaliano tu btn the two
 
What if kama huyo mumewe angekuwa na surname "Kikwete" I am just thinking in the kibongobongo environment!
 
Nimesoma mahali fulani mama mmoja baada ya kuolewa siku moja akakuta barua na nyaraka mbalimbali zote zimebadilishwa kuwa Mrs. Rose Pesambili - Pesambili likiwa jina la ubin la mume wake. Mume aliporudi siku moja ukawa ugomvi.. kwanini amembadilisha jina lake bila kumuuliza na kwanini hata initials zikawa za mumewe..

Mwisho wa siku mke akafanya mgomo "baridi" kwani alisema kikabila cha kwao wao wanaitwa majina ya wazazi wao. Huyo mama ni Mngoni na kwao wanaitwa "Nakomba" yaani binti ya Komba. Alidai kuwa kuchukua jina la mumewe ni tamaduni za wazungu. "Kwa kuolewa mtu haachi kuwa binti ya babake" alinukuliwa kusema dada huyo.

Mume hakujua afanye nini kwani aliamini kuwa ndio kawaida "siku hizi"...

Mgomo baridi unaendelea...

Sawa mkuu,
ila hako kekundu umetukosea kidogo sisi akina manyani, manguruwe, mafisi.....Ni Nyakomba!
 
Mwanamke hana thamani hata ya kutumia jina lake kwa wale wanaowabadilisha majina, halafu wanawake wengine wanaona sifa kubadilishwa jina. Hawajui kama ni dharau kwake na kwa asili yake.
 
Kwa maisha ya kileo uzoefu unaonyesha kwamba mwanamke pindi akiolewa na mwanaume mwenye jina kubwa haraka haraka huwa anabadili ubini,akiolewa na mchovu kama Bishanga wakati kwao jina kubwa ndo utasikia anaitwa mrs Chaupele Bakhresa Bishanga au Mrs Rose Mkapa Bishanga.

Na hapo Bishanga utakuwa na bahati maana wengine wanapotezea kabisa kama huyo Nyakomba anayekataa kuitwa Pesambili. Hiyo ndo hali halisi ya maisha yetu maana hata mke wa Clinton(aliolewa wakati bwamzee bado kidampa) naye mpaka leo anajiita Hilary Rodham Clinton,bila shaka Rodham lilikuwa jina kubwa. Na Nancy Reagan ambaye aliolewa na superstar mcheza sinema Reagan haraka haraka alijiita Nancy Reagan.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom