Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,462
- 39,929
Nimesoma mahali fulani mama mmoja baada ya kuolewa siku moja akakuta barua na nyaraka mbalimbali zote zimebadilishwa kuwa Mrs. Rose Pesambili - Pesambili likiwa jina la ubin la mume wake. Mume aliporudi siku moja ukawa ugomvi.. kwanini amembadilisha jina lake bila kumuuliza na kwanini hata initials zikawa za mumewe..
Mwisho wa siku mke akafanya mgomo "baridi" kwani alisema kikabila cha kwao wao wanaitwa majina ya wazazi wao. Huyo mama ni Mngoni na kwao wanaitwa "Nakomba" yaani binti ya Komba. Alidai kuwa kuchukua jina la mumewe ni tamaduni za wazungu. "Kwa kuolewa mtu haachi kuwa binti ya babake" alinukuliwa kusema dada huyo.
Mume hakujua afanye nini kwani aliamini kuwa ndio kawaida "siku hizi"...
Mgomo baridi unaendelea...