Mkazi wa Iringa Makosa atangaza kujinyonga kwa kiingilio.

Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
244
Hii Kali Kuliko: MAKOSA (mkazi wa Iringa) ATANGAZA KUJINYONGA KWA KIINGILIO, ALIKUWA MFANYABIASHARA MAARUFU SANA MJINI IRINGA

Katika mazingira ya kutatanisha Makosa ametangaza kujinyonga katika tukio atakalolifanya hadharani. Kwanini anataka kulifanya tukio hili hadharani? Hili ni swali ambalo kila mtu anaweza kujiuliza lakini jibu lake anataka iwe hivyo kwa kuwa atajinyonga katika tukio ambalo mashuhuda watalazimika kulipa kiingilio. Kwanini anataka kufanya tukio hilo kwa kiingilio?

Kila mtu anaweza kujiuliza swali hili. Katika majibu yake kupitia mtandao huu, MAKOSA anasema amefikia uamuzi huo ili zikusanywe fedha zikazosaidia kuendesha familia yake, watoto yatima na sehemu kuchonga madawati kwa shule zenye upungufu wa madawati mjini Iringa.

Alipoulizwa kama ana ufahamu wa sheria na kwamba kujaribu au kufanya hivyo ni kosa la jinai, katika majibu yake anasema litakuwa kosa la jinai mpaka pale atakapofanya hivyo na kwa kuwa atakufa hana cha kuhofia. Lakini MAKOSA ni nani?

Kwa wakazi wa mjini Iringa MAKOSA ni mtu maarufu sana, alifahamika zaidi kwa biashara zake nyingi alizoanza kuzifanya mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya kuacha shughuli yake ya ubaharia. Wakati akifika mjini Iringa, MAKOSA akiwa na itikadi za rasta, alikuwa hanywi pombe, mnyenyekevu na alijikita katika kuisaidia jamii ya watu wa Iringa kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti.

Miti ya aina mbalimbali inayonekana mjini Iringa, sehemu yake kubwa ilipandwa na MAKOSA. Hata hivyo pamoja na kuupendezesha mji kwa miti hiyo, historia ya MAKOSA katika uhifadhi wa mazingira ni kama vile imesahaulika kwasababu hakuna anayemuenzi kwa kazi kubwa aliyoifanya.

Pamoja na harakati hizo MAKOSA ndio mtu wa kwanza mjini Iringa kuingiza magari aina ya Coaster zilizokuwa zikifanya kazi ya kusafirisha abiria katika maeneo mbalimbali ya mjini Iringa. Pamoja na biashara ya usafirishaji, MAKOSA alikuwa anaendesha biashara ya hoteli.

Kabla ya kuanza kuendeshwa na MAKOSA, hoteli hiyo ilikuwa ikijulikana Cats Hotel (ipo jirani na Maktaba ya Mkoa wa Iringa) na akaibadilisha jina na kuiita MAKOSA CATS Hotel. Katika hoteli hiyo bendi nyingi zimepiga muziki na kwa mara ya mwisho, mwanamuziki Macay Fanta alikuwa akifanya shoo zake mpaka pale MAKOSA aliposhindwa kuiendesha mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Lakini mtandao wa biashara za makosa haukuishia hapo, alikuwa pia akimiliki hospitali maarufu sana iliyopo jirani kabisa na soko kuu la mjini Iringa, hii nayo iliitwa MAKOSA hospital. Taarifa kutoka kwake mwenyewe biashara zote hizo haziko tena mikononi mwake na ugumu wa maisha unazidi kumuandama.

Japokuwa hajasema hivyo, huenda kuteteleka kwa hayo yote ndio sababu ya MAKOSA kutaka kujiua. Tafsiri ya jina la MAKOSA imeendelea kuwa siri yake na amekataa kutoa maana ya kuacha majina yake halisi ya Ramadhani Mrisho na kujiita MAKOSA.
Chanzo: Frankleonard blog - at Iringa




My Take: Hii yote inatokana na ugumu wa maisha uliosababishwa na sarikali iliyoko madarakani, tuiondoeni sasa.
 
Makosa,nisubiri naja. Nikifika Iringa weekend hii nitakutafuta tuongee. Pole kwa yote...
 
Kachanganyikiwa tu huyu! alikuwa anaijiita "Ras" (offcourse sababu ya dreads zake), kabla ya coaster alikuwa na Isuzu journey ikienda Ilula-Iringa mjini.Nadhani kutokana na kazi yake ya ubaharia ama alipiga dollar ama alipata mfadhili flani na mihela mingi ila management ilimshinda kutokana na shule ndogo akafilisika!
 
Makosa uamuzi mzuri ila utamkosea mungu! kama hutabadili uamuzi wako mualike JK awe mgeni rasmi ashuhudie kuondoka wako kutokana na ugumu uliousababisha na yeye mwenyewe
 
heeee1jamani kwan mungu hayupo hadi jamaa ataka kujitoa uhai,MUNGU NI JIBU LA KILA KI2 TUMUOMBE NAYE ATAJIBU,Afu mkwanja atakusanya nani km mh mwanyewe atasepa?
 
huyu jamaa ni laana, kwa kuna kipin di nlisikia alikuwa anawa babu SEYA vijana wa mitaani waliokuwa wanakwenda kumuomba msaada kipindi ana pesa, anyway lazima na mimi ni hudhurie ilo tamasha
 
Dah nakumbuka jamaa aliwahi kuja kupanda miti miwili home kwetu mitaa ya Mwembetogwa karibu na kanisa la Kakobe, tena ile miti ilinitesa kuimwagilia chini ya uangalizi wa mzee. Duh jamaa ameamua kufanya maamuzi magumu.
 
viroba vinamtesa sana makosa, anashinda mabanda ya CCM tu, umaskini utamfikirisha mengi na hasa kwa kuwa aliichezea shilingi ikamtoka..R.I.P makosa.
 
mwanae njiti nae chenga km baba'ke kuna cku aliniambia dingi*makosa* kamwambia bange avutie home kama yeye na sio kwenye maskani za washikaji
 
hahahaa kweli siku hizi PESA NGUMU mpaka wa2 wanataka kujinyonga kwa kiingilio,J.k angalia watu wako wanaangamia sbb ya usanii wako
 
hata mimi ningependa kuhudhuria tamasha hilo na nnataka V.I.P ili nione vizuri anavyojinyonga
 
Back
Top Bottom