Mkazi mmoja wilayani Mbozi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Omary Katesi mkazi wa kijiji cha Sambewe wilaya ya Mbozi mkoani Songwe amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya mahakama kuu kanda ya Mbeya kumkuta na hatia ya mauaji ya kukusudia dhidi ya kaka yake sikujua katesi kutokana na mgogoro wa kugombania mali za urithi.

Jaji wa mahakama kuu kanda ya mbeya atughanile ngwala ametoa hukumu hiyo wakati wa kikao chenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji mkoani songwe ambapo katika shauri hilo la jinai namba 56/2014 lilikuwa likiwakabili washtakiwa watatu mshitakiwa namba moja maria senye ambaye ni mama wa mshitakiwa namba tatu omari katesi na mshtakiwa namba mbili alikuwa charles lason nzowa.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa washitakiwa kwa pamoja walitenda la kuua kwa kukusudia kinyume kifungu namba 196/197 cha kanuni ya adhabu tukio ambalo lilitendwa mnamo septemba 23 mwaka 2012 huko sambwewe, ambapo mshtakiwa alikodisha wauaji kisha kumuua kaka yake usiku akiwa amelala na kumjeruhi mke wa kaka yakekwa mapanga ambapo baada ya kunusirika aliwataja wahusika wote akiwemo mama mzazi.

Historia ya tukio imeeleza chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa mali za urithi ambazo ziliachwa na baba yao mzazi kates william shega, ambapo sikujua alimshauri kutouza holela mali ambayo ni mashamba na mifugo na kurudisha fedha kwa mmoja wa wanunuzi wa shamba kwa lengo la kuokoa mali jambo ambalo lilimkera omari na kukodi wauaji kutoka kwa mshitakiwa namba 2 charles lason nzowa kwa shilingi laki 9 na aliyetekeleza mauaji hayo mshtakiwa huyo namba 2 alifariki akiwa gerezani.

Jaji ngwala amesema kwa maelezo ya mashahidi nane yaliyotolewa mahakamani hapo, pasipo shaka yoyote mahakama imeridhishwa na ushahidi huo na kwamba adhabu ya mtu anayepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia na ukiri uliotolewa na mshitakiwa mara baada ya kurejea kijijini, kwa kifungu namba 322 sheria ya kanuni ya uendeshaji wa kesi za jinai sura namba 20 iliyofanyiwa marekeshi mwaka 2002, ikamtia hatia nakutoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa.

Aidha jaji ngwala amelazimika kuahirisha vikao vya kusikiliza kesi za mauaji kwa muda usio julikana baada ya mawakili watatu kuugua ghafla wakidaiwa kula chakula kinachodhaniwa kuwa na sumu kilichopikwa kwenye mgahawa wa ujulikanao kama be free hotel uliopo vwawa mjini, ambapo mawakili wote wamekimbizwa hospital ili kupatiwa matibabu na kwamba vikao hivyo awali vilipangwa kusikiliza kesi tano za mauaji kuanzia tar 6 nov hadi 17 novemba 2017.



ITV
 
Si nasikia bongo hakuna raisi aliyesaini hati ya kifo tangu enzi za Nyerere? Sasa hawa wananyongwaje?
 
Si nasikia bongo hakuna raisi aliyesaini hati ya kifo tangu enzi za Nyerere? Sasa hawa wananyongwaje?
Ukisoma Penal Code (S.196 na 197) utaona murder case adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa, lakini ili mtu anyongwe kuna utaratibu ikiwemo Rais kutia saini kuridhia kunyongwa kwa mtu husika.

Sasa kwanini wanaendelea kuhukumu kunyongwa ilihali hawanyongi? Ni kwa sababu katika penal code sheria hiyo haijabadilishwa kutamka adhabu tofauti na kunyongwa pale mahakama inapojiridhisha kuwa uliua kwa kukusudia.

Kwanini Rais hasaini tangu enzi za JKN? Kwa sababu nchi ilitia saini mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu hivyo inawajibika kulinda mikataba hiyo ikiwemo kutokunyonga binadamu.

Ile juzi ilikuaje JPM kuwabadilishia adhabu waliohukumiwa kunyongwa ilihali sheria iko wazi? Katiba ina Ibara ya 45 inaitwa "Prerogative of mercy" inampa Rais mamlaka ya kumsamehe mtu yeyote anayeshikiliwa gerezani iwe kwa masharti au bila masharti, yaan anaweza kumsaheme hata mtu alomuua ndugu yako wewe ukiwa unashuhudia
 
Back
Top Bottom