Mkazi Mafinga ajitokeza kufukua kaburi la Kiyeyeu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkazi Mafinga ajitokeza kufukua kaburi la Kiyeyeu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 29, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SIKU mbili baada ya gazeti hili kuripoti taarifa za Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), mkoani Iringa kushindwa kuhamisha kaburi la Martin Kiyeyeu kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara kutokana na imani za kishirikina, mkazi wa Mafinga Sadick Mhomanzi, amesema anaweza kufanya kazi hiyo kwa muda mfupi tena bila gharama kubwa.

  Kaburi la Kiyeyeu linakadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 50 sasa lipo katika kitongoji cha Isimila, Kijiji cha Ugwachanya, wilayani Iringa karibu na barabara kuu ya Iringa kwenda Mbeya likiwa na historia ndefu kutokana na kushindikana kuondolewa katika eneo hilo mara kadhaa kutokana na miujiza iliyopo katika eneo hilo

  Moja ya vituko vya kaburi hilo ni kushindikana kwa umeme kupita juu ya kaburi na pia linadaiwa kushindikana mara mbili kulitoa na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga kulitoa kaburi hilo.

  Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana Mhomanzi alisema kaburi hilo linaweza kuondolewa bila madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.

  Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.

  Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika. "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.

  Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema . Mwisho.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  THIS POST HAS BEEN DELETED BY GAmA...............
   
Loading...