Mkataba wa Ulinzi Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,555
19,428
Mkataba kama wa NATO hufanya nchi wanachama wajione wamoja na huwa hawawezi kukwaruzana kijeshi. Kwa vile Jumuia ya Afrika ya Mashariki imepanuka na kuwa kubwa sana ikiwa na nchi zenye itikadi tofauti tofauti, kuna haja ya kufanya mambo kadhaa.

Kwanza ni kuweka sera ya pamoja ya ulinzi ili kuepusha migogoro ya kijeshi baina ya nchi wanachama, njia mojawapo ikiwa ni kuweka mkataba unaofanana na NATO kusudi wanachama wote wawe na lengo moja la kulindana kwa pamoja.

La pili ni kwa kila nchi kufanya marekebisho katika katiba zao kuwa na mifumo ya utawala inayofanana. Siyo kwa nchi kama Kenya na Tanzania wao kuwa na vipindi viwili vya rais kwa miaka mitano mitano wakati Uganda na Rwanda wao hawana term limits.

Nchi ikishakuwa na rais wa muda mrefu sana, huwa ni rahisi sana kutokufuata taratibu ikaishia kuwa inatekeleza yale yanayosemwa na kiongozi huyo hata kama ni kinyume cha sheria. Hii itakuwa pia ni pamoja na kuhakikisha kuwa mambo ya vyama vya siasa hayaingizwi kwenye serikali zote.

Mabadiliko hayo ya katiba za nchi husika yataweza kusaidia kuondoa migogoro na vita za wenyewe kwa wenyewe kwenye baadhi ya nchi. At the same time, mkataba huo utazifanya nchi zisisaidie waasi dhidi ya nchi nyingine.

Mwishoni mkataba huo unaweza kusaidia sana kuondoa baadhi ya migogoro ya mipaka, hususan Kenya na South Sudan, na vile vile Kenya na Uganda kwenye visiwa vya Migingo.
 
Wazo zuri ila utekelezaji wake ndio kisanga
Kufikia modality ya EU/ NATO tunatakiwa kujifunga mkanda kweli kweli, imagine tuna AU Agenda 2063 lakini mimi kuizunguka tu Afrika ni bora nikaizunguke EU. Afrika inahitaji mabadiliko makubwa sana kufikia hiyo ndoto
So far security assurance ziko mbili
US-UK
US-Israel
 
Back
Top Bottom