Mkataba wa Stamico wa kuuza makaa ya mawe uchunguzwe

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Tanzania kupitia Stamico tumesaini mkataba wa kuuza Madini ya Makaa ya Mawe kwa dola 29.5 ambayo ni sawa na Shilingi 69,444 (Elfu sitini na tisa na Mia nne arobaini na nne tu) kwa Tani moja!

Bei ya Soko la Makaa ya Mawe kwenye Market Insider ni dola 315 sawa na shilingi za Kitanzania 740,250 (laki saba na elfu arobaini na mia mbili na hamsini).

Reuters wameripoti kuwa bei ya Madini ya Makaa ya Mawe inatazamiwa kupanda kwa mwaka 2022 kufikia dola za Kimarekani 500 sawa na shilingi za Kitanzania 1,175,000 (Milioni moja na laki moja na elfu sabini na tano)

Afrika Kusini wanauza makaa ya Mawe kwa bei ya Dola za Kimarekani 140.07 ambayo ni sawa na shilingi 329,164 hii ni bei iliyoporomoka toka kwenye bei ya Dola 214.27 sawa na shilingi 503,534 ya mwezi uliopita!

Ukiangalia bei ya Soko la Madini haya na wastani wa bei inaashiria dhahiri pasi na shaka kuwa Mkataba huu una viashiria vikubwa mno vya Rushwa!

Haiwezekani Madini yetu ya Makaa ya Mawe yauzwe kwa bei inayolingana na bei ya Kifusi cha Udongo/Mchanga!

Watoto na wajukuu zetu watakuta mapango na mashimo watatuuliza hapa palifanyika jambo gani?

Tukiwaambia palikuwa na Madini ya Makaa ya Mawe ambayo yaliuzwa kwa Tani elfu 69,444 watatulaani, watatutukana na kutuadhibu!

Ni heri haya Madini tuyaache vizazi vijavyo viyakute kuliko kuyachimba na kuyauza kwa Mikataba iliyojaa rushwa na Ufisadi!

Haiwezekani Mbuzi mmoja awe na thamani kubwa kuliko Tani moja ya Madini ya Makaa ya Mawe!

Naiomba Serikali kupitia vyombo vyake iuchunguze mkataba huu , iuvunje na ichukue hatua kali kwa kila aliyehusika kuruhusu Mkataba wa kifisadi kama huu ili iwe fundisho kwa watumishi wa Umma wote na wanasiasa wasio waadilifu!
Wizara ya Madini
 
Kama mliweka mkataba wa muda mrefu itabidi mkubali hadi siku mkataba ukiisha...

Japo nadhani kuna mchezo
 
Unapouza kitu chochote, kwanza unapiga mahesabu ya gharama za uzarishaji ikiwemo kodi zote halafu ndio unaweka asilimia zako za faida.. hapa kila mtu sasa huingia sokoni na bei, kumbuka pia, lazima uwe na bei shindani ili kuvutia soko..

STAMICO is the state owned company, sio private entity....vuta kumbukumbu na kufikiri zaidi....
 
Unapouza kitu chochote, kwanza unapiga mahesabu ya gharama za uzarishaji ikiwemo kodi zote halafu ndio unaweka asilimia zako za faida.. hapa kila mtu sasa huingia sokoni na bei, kumbuka pia, lazima uwe na bei shindani ili kuvutia soko..

STAMICO is the state owned company, sio private entity....vuta kumbukumbu na kufikiri zaidi....
So Wako sahihi Kuuza 1kg ya Makaa ya mastone kwa elfu69???

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom