Mkataba wa muungano uandikwe upya

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,810
2,000
Kwa mujibu wa mkataba wa muungano wa 1964 wenye vipengele 11, na baada ya nyongeza kufikia 22..bado Tanzania inabaki kuwa muungano wa nchi mbili huru.Muungano huu ni wa baadhi ya mambo tu.

Mambo yaliyobaki si ya muungano,kwa msingi huu ,nchi husika zitabaki kuwa na mamlaka kwenye mambo yasiyokuwa ya muungano.

Kwa msingi huu Kikwete alitaka kuandika katiba mpya kama vile Tanzanian ni nchi moja .Kosa lake ni kusahau washirika wa muungano kuandaa makubaliano mapya kwanza.Kukosekana kwa makubaliano mapya nakutumia yale ya zamani ni kasoro kubwa ya mchakato huu.

Pili huo mkataba wenyewe wa 1964 haufuatwi tena na umeshavunjwa na hauna tena uhai,Hii ndio kasoro kuu ya pili.Warioba kafanya kazi nzito sana ambayo haikuwa na ulazima.

Zanzibar wangekusanya maoni yao na mambo wanayotaka yawemo kwenye muungano na aina waitakayo ya muungano,kisha wakayaratibu . Hivyohivyo na Tanganyika wangalifanya mchakato wa aina hii.

Baada ya michakato hii ndio wangekabidhiwa tume ya warioba.

Katika bunge kila upande ungekuja kutetea mapendekezo waliyoyaleta katika " short list".

Bunge lingehitaji mwezi 1 tu kupitisha mkataba/katiba mpya.
 

Bobwe1

JF-Expert Member
Apr 8, 2014
396
0
Mkuu hakuna katiba mpya,kinachotafutwa ni uhalali wa kuimaliza zanzibar isipumue tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom