Mkataba wa Fei Toto na Yanga na Mkataba wa Johnny Fontaine na Jamaa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,881
30,226
MKATABA WA FEI TOTO NA MKATABA WA JOHNNY FONTAINE

Naamini ni wachache wataelewa.

Mario Puzo aliandika kitabu kilichokuja kuwa maarufu na kikatengenezwa filamu iliyokuja kuwa maarufu kupita kiasi.

Jina la kitabu na filamu ni "The Godfather."

Huyu Johnnny Fontaine katika kitabu ni kijana mdogo wa Kitaliani mwimbaji wa sifa katika New York ya 1945 baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia.

Wakati anaanza kuimba hajawa maarufu alitiliana mkataba na kampuni ya kutengeneza sahani za santuri.

Jinsi alivyoendelea kutoa nyimbo baada ya nyimbo Johnny Fontaine akazidi kupendwa na mauzo ya rekodi zake yakazidi kupanda juu.

Mwenye kampuni akawa anapata fedha nyingi sana lakini Johnny Fontaine mrabaha wake ni ule kiduchu aliotia saini kuwepo kwa miaka mingi.

Kampuni nyingine kubwa na maarufu zikawa zinamtaka Johnny Fontaine kwa dau kubwa sawa na thamani yake.

Yule jamaa wa kwanza aliyefunganae mkataba akakataa kumwachia.

Johnny Fontaine akawa hana la kufanya.

Mwishowe akaenda kwa baba yake wa ubatizo, The Godfather kumshtakia na kutaka msaada.

Godfather akaenda kwa yule jamaa na Bouncer Mkuu, Luca Brassi wakashughulikie suala la mwanae.

Jamaa akawa mkaidi ingawa alipewa fedha nyingi afute mkataba wa Johnny Fontaine ili kijana aende kuboresha maisha yake kwengine.

Luca Brassi akachomoa bastola yake nzito akaiweka kichwani kwa jamaa Godfather akamwambia, "Weka saini makubaliano haya kwenye hii karatasi au damu yako ndiyo itakuwa saini yako kwenye karatasi hiyo."

Jamaa akawa keshajua kuwa waliyemfuata ni Mafiosi.

Hakusita haraka sana ikimwagika saini.

Mwanzo wa mazungunzo aliahidiwa fedha za maana kumwachia kijana wa watu akagoma.

Alipokubali kusaini baada ya vitisho Luca dau likashushwa dau chini kabisa jamaa akapewa vijisenti.

Godfather alikuwa mtu mjanja alikwisha mjua yule jamaa msumbufu kwa hiyo ingawa alikuwa na Mwanasheria Nguli, Tom Hagen hakumchukua Tom Hagen na mkoba wake kwenda kwa jamaa.

Alimchukua Mbabe Luca Brassi na bastola yake nzito kwenda kwa jamaa kumaliza uzia na kadhia.

Wanasema kisa cha Johnny Fontaine ni kisa cha kweli kuhusu mambo yaliyomfika Frank Sinatra muimbaji nguli wakati bado kijana mdogo anaanza muziki wake.

Siku alipokutana na Mario Puzo Frank Sinatra alimtolea Mario Puzo maneno makali akimlaumu kwa kuyatia maisha yake kwenye kitabu chake.

"Why did you put my life in your book?"

Frank Sinatra alifoka na yeye alikuwa na sifa ya ushari.

Lakini lililomuudhi khasa si hilo bali ni kule Mario Puzo kuiambia dunia kuwa yeye Frank Sinatra ana uhusiano na Mafia.

Nataka sana kujua muziki huu wa Fei Toto unachezwaje?

Kila ninapowasoma waandishi wa michezo wanapogusia mkataba wa Fei Toto na Yanga naukumbuka mkataba uliokonda wa Johnny Fontaine na jamaa.

Katika filamu nafasi ya Godfather ilichezwa na mwigizaji bingwa wa mabingwa Marlon Brando na Johnny Fontaine ilichezwa na mwimbaji Al Martino.

322590166_829392115018751_1540085188436339258_n.jpg

322485940_826515358452671_5519598236868001131_n.jpg
 
Mzee Mohamed hili suala la Fei nimelielewa kabisa, wachezaji wa ndani wathaminiwe, wizi na ujanja ujanja mishahara mibovu Kwa wazawa natumai unaelekea kukoma, tunathamini Sana wageni, inabidi kumuiga Morrison na Fei alichokifanya kitabadilisha upepo na wachezaji wazawa Maisha yataboreka,ashukuriwe Azam amebadilisha soka la Tanzania...
 
Je unaweza kuongezewa mshahara ukiwa bado unautumikia mkataba? Nini kilitangulia kati ya umaarufu wa Fei na mkataba wake wa sasa?
 
Back
Top Bottom