Mkasa wa kweli: ungefanyeje?

Kuzaliwa mwanaume ni sawa na SIMBA na mwanamke ni Sawa na Swala
 
Huyo mwanaume yupo katika kipindi cha uchaguzi 2020 lazima apige siasa zote ili aibuke kidedea maana anawajua wapiga kura wake walivyonahuruma
 
dada yangu,,,huyo ndo mumeo.......amekwambia alikuficha sbb hakupenda muachane....maadam ulialikwa kwenye kikao muhimu, elewe ndio wako na anakupenda hakutaka uingie kwenye migogoro mpaka talaka itoke...na kwa sbb wamekubaliana kutalikiana msisitizie daily....muyaanze maisha...umzalie na wana....msamehe...
 
Sikia dada yangu,huyo ni mmeo wala usihofie ule uongo. Kuna wakati wanaume huwa tunalazimika kudanganya baada ya kujua huyo mtu uliyenaye anataka kusikia nn! Yaani km mwanamke nampenda,na nnajua kuna vitu hapendi nitasema uongo kwenye hiyo category. Nikuhakikishie huyo mtu wala usihangaike na talaka,talaka ni makaratasi tu,mtakuwa mnachelewa tu kuanza kutengeneza familia. Kumbuka ndoa ya kanisani haina talaka. Mimi nilioa mwaka 1997,lkn kufikia mwaka 2005 ndoa yangu ilikuwa jehanam. Lkn nilivumilia kulinda heshima ya watoto wangu. Mwaka 2008,nilipata mtu na nikaanza naye urafiki nikiwa ndani ya ndoa. Sikuwa nimemuacha mke wangu,na muda mwingi niliutumia sana kwa mke wangu ingawa ukweli ndoa haikuwepo. Mwaka 2010 nikabahatika kupata mtoto na huyo rafiki yangu,huyu wa ndoa hata kujamiiana tulikuwa tumeacha. Tulibaki hivyo,na hakujua km nimezaa nje na nilikuwa kila ijumaa jioni naenda kwa mpenzi wangu narudi jpili. Mwaka 2013 niliumwa jicho na kufanyiwa upasuaji,nilikuwa nahitaji mtu mwenye upendo nami kunihudumia. Hapo ndo ulikuwa mtihani. Nilichagua kwenda kwa mke wangu wa ndoa baada ya kutoka hospital. Lkn kilichonipata Mungu anajua,siku 3 baadae nikaita taxi nikatimkia Kwa mpenzi wangu. Na siku iliyofuata nikampigia simu mke wangu nikaweka wazi uhusiano wangu na kwamba tayari tulikuwa na mtoto wa miaka 3. Hakuweza kustahimili zile taarifa,kesho yake akapeleka canter akabeba kila kitu cha ndani na watoto wangu akawaacha hapo. Sikumfanya chochote,kesho yake nikaenda keko nikanunua fenicha zote mpya. Na maisha yanaendelea na yule aliyekuwa mpenzi wangu,ndo mke wangu hadi leo. Na huwezi amini yaani hapa naona km nimekutana naye jana tu. tunapendana ile mbaya na tayari tuna mtoto mwingine now ana miaka 4. Baada ya maelezo haya marefu,leo ukienda usirudi tena kule kwako..
TOUCHED!
 
Mimi ni mwanamke
Nipo kwenye mahusiano ya kuishi pamoja kupika na kupakua na mwanaume Mwenye miaka 45 kwa muda wa miaka 3 Huku tulipanes Mipango yakuoana. Wakat tunaanza alidai Ana watoto 2 (ke na me) mama tofauti ila hajawaoa. Na mtoto mkubwa anaishi na shangazi yake. Anadai alichelewa kuoa kutokana na ugumu wa maisha aliyokulia na pia alihaso sana hadi Leo kufikia alipo.
Kuna kipindi niliwahi kupata tetesi kwamba améoa ila alikataa katakata. Juzikati alipata msiba wa moja ya mzazi wake ikabidi aende ila alikataa mimi nisiende. Baada yayeye kuondoka nikapanga Safari nikamfwata ila nilipofika stand akanipotezea hakuja kunipokea.
Niliamua kutumia mbinu zangu hadi kufika kwao na kukuta msiba.
Nilishangaa kukuta ameoa tena ndoa ya kanisani. Tulipokaa na kuzungumza alijitetea kwamba walishaachana kwa kuwa hawakuwa na maelewano na ni kama ndoa haikuwepo. Walishasuluhishwa ikashindikana. Ila Bado mwanamke alikuwa hajahamisha Mali zake kutoka kwenye nyumba ya mwanaume (aliikuta alipoolewa).
Pía alijitetea alinificha kwa kuwa aliogopa nitamwacha.
Mipango iliyopo: amesema anatoa talaka kisha mengine yaendelee kama yalivyopangwa.
Sasa wazoefu na wasio wazoefu naomba mnishauri nifanyejee?? Maana siko vizuri.

Nyongeza:
Tuliwekwa kikao mimi yeye mkewe na ndugu zake. Nikamuuliza alikuwa wapi mbona ckuwahi kumsikia Hata cku moja wala kumuona? Mkewe alikiri kutokuwa vizuri na mumewe na pía ashapata mwingine. Na watu wote walikiri kwamba ile ndoa kiuhalisia ilibaki vyeti. Na ndio wakashauri talaka ili kila mtu awe huru.
Bwana ameomba msamaha sana na anatishia Hata kujiua.

Pole Madam,haupo peke yako kwenye hicho kisanga sema tumetofautiana kidogo.

Wangu hakuniambia alinificha hadi uhusiano ulipokomaa nikawa nimepata mimba ikiwa na miezi miwili ndo akaniambia tena baada ya kuona picha .Nilishtuka kwakweli,nakummbuka ilikuwa ni siku ya kazi nikamsubiri aliporudi nikamwambia aliomba msamaha kwa sababu nilikuwa na mimba nilimwambia nimekusamehe akanionyesha hadi divorce yao .Tulipelekana kwa wazazi nikawaambia ukweli najua walilipokea kishingo upande tu ila walitoa baraka zao tukafunga ndoa ya Bomani mwezi wa kumi na moja mwaka 2009.wakati huo mimi nilikuwa na miaka 25 yeye alikuwa na miaka 35.Yeye alioa akiwa na miaka 27 .Nashukuru Mungu wazazi wangu na ndugu zangu wote walihudhuria shuhuli yetu .SASA TUNAMIKA KUMI YA NDOA YETU YA BOMANI NA TUMEBARIKIWA WATOTO WANNE WADADA 2 NA WAKAKA WAWILI NA TUNA AMANI NA FURAHA KWA KWELI.
uSHAURI wangu kwako Madam huyo jamaa ni wakwako usiamuache unaweza kumuacha ukaja kujuta milele na ukakosa hata wa kukuoa,msamehe kwa pale ambapo hakukwambia ukweli.
 
Duh. Kumbe kuna stori kama hii pia. Kwa kweli utani wa siku hizi una tisha yaani. Dhamani ya vitu vingi vina potea kwa kutaniana hivi hivi hadi ukiwa una sema ukweli hakuna wa kukusikia.

Anyway, kama huyu wa sasa ndio mnapendana hivyo, basi forgive and try and forget. I always say we are a congregation of sinners. No 2 perfect beings exist and meet. Making it work is messy. Your choice to stick with it or give it all up and start again with a new lie.
Ukweli utanisamehe bure ila ya leo ni ya kweli kabisa. Kama nadanganya MUNGU ANIHUKUMU. Watu8 NAKUHESHIMU MNOO.
 
Ninawasoma japo mambo ya utafutaji yamenibana. Huduma za kila Siku ninapatiwa (matumizi), kifupi ananithamini kwa kiasi cha ubinadamu wake... Siwezi kusema amekamilika ila mbali na hayo matatizo anajitahidi.

Naendelea kucheua maoni yenu wote. Nina Imani siku mmoja nitawaletea maamuzi na nitakapofikia. Ninawashuru na Nawaomba sana msisite kunishauri
 
Pole sana...

Kama ujuavyo ndoa za kanisani hazina talaka...

Follow your heart but carry your brain with you...


Cc: mahondaw
 
Ninawasoma japo mambo ya utafutaji yamenibana. Huduma za kila Siku ninapatiwa (matumizi), kifupi ananithamini kwa kiasi cha ubinadamu wake... Siwezi kusema amekamilika ila mbali na hayo matatizo anajitahidi.

Naendelea kucheua maoni yenu wote. Nina Imani siku mmoja nitawaletea maamuzi na nitakapofikia. Ninawashuru na Nawaomba sana msisite kunishauri

ukifikia uamuzi usisahau kunitag please
 
Update:
Japo alikiri kwamba hayupo na huyu bwana na pia ashapata mwingine kwa ushauri wa baadh ya ndugu Mke aliyeachwa amefungua kesi mahakamani kwamba ametelekezwa na mumewe.
 
Update:
Japo alikiri kwamba hayupo na huyu bwana na pia ashapata mwingine kwa ushauri wa baadh ya ndugu Mke aliyeachwa amefungua kesi mahakamani kwamba ametelekezwa na mumewe.
Which I think itapelekea talaka between them.
Au bado anamtaka?
 
Ameamua kumsumbua tu na pia anataka wagawane mali ambazo mume anadai hawakuchuma pamoja.
Ok, pole!
IWAPO WAKATI MALI HIZO ZILICHUMWA WAKIWA BADO HAWAKUPEANA TALAKA KISHERIA(which is true)
Dada atagawana nae tu, huna namna ya kuzuia!
Unless kama umiliki wa hizo mali unasoma tarehe za nyuma ya ndoa yao.
BADO NI MUME WAKE HUYO, until wamepeana talaka!
Sikushauri kuanza au kuendelea kuinvest nae huyo mwanaume mpka hapo utakapooneshwa talaka yao!
 
Update:
Japo alikiri kwamba hayupo na huyu bwana na pia ashapata mwingine kwa ushauri wa baadh ya ndugu Mke aliyeachwa amefungua kesi mahakamani kwamba ametelekezwa na mumewe.
Haya mambo yanasumbua sana kilichokukuta kinakaribia kufanana na kilichonikuta ila mimi niliamua kuwaacha wauane ama wapendane is up to wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom