Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,204
- 4,692
Wadau wa JF
Nikiwa darasa la tano Shule ya Msingi Mgulani iliyopo jirani na DUCE Jijini Dar es salaam
Nakumbuka siku ya mkasa huo aliingia Mwalimu wetu wa lugha ya Kiswahili akijulikana kwa jina la Mwalimu Kanji ambaye alitoa somo la siku hiyo na kisha kutoa fursa kwetu kutoa vitendawili/ misemo/ methali
Utaratibu ulikuwa mwanafunzi mmoja anasimama na kutega kitendawili na kisha anayeweza kukitegua alinyoosha mkono wake na kusimama kutoa jibu kwa ruhusa ya Mwalimu
Tulifurahia sana zoezi hilo hadi ilipofika zamu yangu ndiyo hali ya hewa ikachafuka!
Nakumbuka nilinyoosha mkono wangu kwa muda mrefu na niliporuhusiwa nilisimama na nilianza kwa kuwaomba Wanafunzi wenzangu wakae kimya na wanisikilize kwa umakini
Kilichotokea hawakuamini na hata Mwalimu naye alipata mshtuko mkubwa kama sio mshangao kwani nilitamka "Mficha Uchi".....????
Ilikuwa mshikemahike darasani Wanafunzi wakishangilia huku wakicheka kwa nguvu!
Nakumbuka darasa hilo la vitendawili liliishia hapo hapo na Mwalimu alitaka kuniadhibu japo nilimsihi Sana asifanye hivyo kwani sikuwa na nia mbaya!
Namshukuru sana Mwalimu wangu alikuwa muelewa hakunichapa ila alinikanya nisirudie tena kutoa Vitendawili vya "Wakubwa"
Karibuni tujadili na kubadilishana uzoefu