Mkasa Wa Kweli : Kuzimu Na Duniani

SEHEMU YA 20


Kusema kweli mimi nilishtuka sana, nikataka kupiga kelele za kuomba msaada lakini nilipokumbuka kwamba pale ni ujinini nikaacha kwani niliamini nisingeweza kupata msaada wowote na zaidi sana huenda ingechangia kifo changu.


“Mwingine.”


Ile sauti iliamuru tena, akaingia mwanamke mmoja ambaye alikuwa akitetemeka. Mlango ulipofungwa tu, tukasikia milio ya risasi. Mingi sana. Kama kuna watu walikuwa na bunduki, basi walizidi hata kumi kutokana na ile milio.


Ilipokoma kusikika, ikaja ile sauti ya kuamuru mtu mwingine aingie, mwanaume aliyekuwa mbele ambaye ilibidi aingie akarudi nyuma ya mtu aliyekuwa nyuma yake.


Sijui mimi niliupata wapi ujasiri nikajikuta nikisema mimi nakwenda. Lengo langu lilikuwa kujua kuna nini kule na je, tunayoyasikia ndiyo yanayofanyika kule ndani?


Niliwapangua watu kwenda mbele ili nikaingie mimi. Lakini kabla sijafika, nilisikia ile sauti ikisema ‘narudia tena, mwingine’.


Nilisukuma mlango, nikazama ndani lakini nilifikia kuanguka chini na kupoteza fahamu.

Niliposhtuka, nilikuwa katikati ya watu chini. Watu wenyewe ni waumini wa kanisani kwa mke wangu. Mke wangu pia alikuwepo na mchungaji wake, wote waliniangalia.


Ilionekana walikuwa wakisali, kujitokeza kwangu ndiko kuliwafanya wanyamaze. Nilipoangalia vizuri nikagundua nipo sebuleni kwangu.


“Pole sana bwana, habari za kuzimu?” aliniambia mchungaji huku akiwa ameshika Biblia.
Sikumjibu, nikainuka na kukaa kwenye kochi. Mchungaji akanisimulia kuwa, baada ya kutoweka nyumbani, mke wangu alimpa taarifa, ikabidi wafunge na kuomba kwa siku tatu na siku hiyo ndiyo ilikuwa ya tatu, wakaamua kuja kumalizia nyumbani kwa maombi mazito.


Mchungaji alisema aliona katika maono nikiwa nasulubiwa katika mikutano ya kuzimu, hivyo alizidisha maombi ili kunifungua katika kifungo hicho.


Niliwashukuru sana wote, hasa mke wangu. Mchungaji akaniambia nipige magoti ili aniongoze sala ya toba. Mpaka leo hii mimi ni muumini mzuri wa kiimani katika kanisa la kiroho analosali mke wangu, lipo mjini Iringa.


MWISHO.

Safi sana... Simulizi nzuri...

Ila kaa ukijua siyo kila siku binadamu hushinda majini, nao wanatuotea sana na kutuweza...

Chapter Closed


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom