Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,445
- Thread starter
- #21
SEHEMU YA 15
Fuatilia sana tabia za kupoteza vitana nyumbani. Si vitana tu, vitu vyovyote vidogovidogo. Mara kalamu haipo, mara kuna CD ya muziki ilipotea, mara kuna glasi au kijiko hakionekani! Ujue unaishi nyumba moja na majini.
SASA ENDELEA MWENYEWE:
Kupotea kwa vitu hivyo mara nyingi kunasababishwa na wao kutovipenda vitu hivyo. Unaweza kununua kitana, wao, hasa yule unayeishi naye kwenye chumba kimoja hakipendi kitana hicho. Kwa hiyo anakichukua na kukitupilia mbali. Kwa upande wa wanawake, wengi hujikuta wakipotelewa na vibanio, vifuniko vya pafyumu, vioo, vitambaa vya mkononi na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.
Wengi utawasikia wakiwalalamikia wasichana wao wa kazi kwamba wanapoteza vitu hivyo lakini kumbe siyo. Hii huweza kutokea hata kwa nguo za ndani.
Kifupi ili ujue unaishi nyumba moja na viumbe hao, mara nyingi utatokewa au kusikia vitu visivyo vya kawaida. Umelala, unasikia kwa mbali kama mlango wa uani unafunguliwa, ukienda hukuti mtu wala hakuna dalili kama kuliingia mtu.
Kwa wale wanaopanga nyumba, cha kujihadhari nacho ni hiki! Kama nyinyi ni wanandoa, mnaweza kujikuta mmehamia kwenye nyumba ambayo ugomvi haushi kila siku. Kitu kidogo tu, ugomvi.
Na ugomvi huo, mara nyingi utamsikia mke akipenda kusema anarudi kwao au mume akisema utaondoka humu ndani. Kama hakuna historia ya hivyo, hapo mjue kuna jini mnaishi nalo, sasa halitaki tabia zenu za kufanya tendo la ndoa wakati lenyewe lipo.
Basi, turudi kule kwenye ile sherehe. Baada ya kumalizika, majini waliondoka mmojammoja kwenda nje ambako walisimama sehemu moja.
Hapa niseme kidogo, naamini mmewahi kusimama eneo ambalo ghafla mkahisi joto. Basi ujue kuna majini zaidi ya kumi yamesimama hapo jirani yenu yakiendelea na shughuli zao.
Basi, pale nje, mmoja wao aliniambia natakiwa kutafuta baa tano nzuri ambazo zinajaza sana wateja na nikishazipata wao watakuja kuchukua jibu usiku wa kesho yake.
Nilikubaliana nao, wakanisimamisha wima, kisha wakaniambia ninyooshe mikono yote juu, nikafanya hivyo. Wakasema usiku mwema, tutaonana kesho.
Ilikuwa kufumba na kufumbua, nilikuwa nje nyumbani kwangu. Mlango ulikuwa umefungwa, lakini nilipoanza kutembea kuelekea mlangoni, ulifunguka wenyewe, nikaingia ndani.
Nilimkuta mke wangu ameshalala, lakini nilipoingia tu, alishtuka sana na kuanza kusali.
Alisema anamshukuru Mungu kwa kumshindisha salama na kumfikisha usiku ule salama kwa vile kuna wengi walitamani kuimaliza siku hiyo lakini wameshindwa, lakini yeye aliyepewa nafasi hiyo hajatumia ufundi wowote, hajatumia maarifa, hajatumia nguvu wala kipaji, bali ni neema ya Mungu tu.
Nilisimama kumsubiri amalize kusali. Alipomaliza tu, akaniangalia na kuanza kulia. Kabla sijamuuliza kisa cha kilio chake, nikasikia hodi wenyewe.
“Karibu mchungaji,” mke wangu alimkaribisha, akaenda kufungua mlango yeye huku akifuta machozi.
Nilisikia wakisalimiana sebuleni bwana asifiwe, bwana asifiwe. Nikaachana na wao, sikutaka kutoka bali nikapanda kitandani ili kulala.
Baada ya dakika kumi kupita, nikasikia wakisali huku wakikemea. Hiyo ilinipa shida sana mpaka nikawa silali. Nikawa nahamahama pale kitandani, mara nahisi moto.
asema moto na si joto. Mara nikawa nahisi kuchomwa na vitu vyenye ncha kali.
Nikajua yote yale ni kwa sababu ya yale maombi. Nilishindwa kulala, nikakaa.
Ilikuwa kufumba na kufumbua, nikaona watu watatu wamesimama mbele yangu. mmoja akasema:
“Tumeona mateso yako. Mke wako amekuwa kikwazo kikubwa sana kwetu. Mara nyingi ndiyo amekuwa akisimama kuzuia mipango yetu mikubwa kwako. Sasa tunasema tunapambana naye.”
Walipomaliza kusema hivyo, wakafutika machoni pangu, nikabaki mwenyewe. Mara nikasikia sebuleni sauti za maombi zimeongezeka mara tatu zaidi ya mwanzo. Nilijua hali imebadilika, jamaa zangu wamezuka sebuleni sasa mchungaji, mke wangu na wengine wanapambana. Mchungaji alikuja na watu lakini sikujua ni wangapi ila kwa zile sauti za kukemea walikuwa zaidi ya watatu.
Nilitoka kitandani, nikatembea hadi mlangoni, nikafungua na kutokea sebuleni ambapo nilikuta watu saba, akiwemo mke wangu, wakiendelea kukemea.
Mchungaji aliponiona, akawasimamisha wenzake. Kukawa kimya, lakini ghafla wakaanza tena. Safari hii mchungaji ikawa, mkono mmoja ameshika Biblia mwingine anautumia kunielekezea mimi huku akiendelea kukemea.
Ghafla, nilishikwa mkono kwa nyuma na kuvutwa. Aliyenivuta sikumwona, lakini nikajua ni wale jamaa zangu. Nia ya kunivuta ilikuwa kunirudisha chumbani. Lakini wakati naingia, mchungaji aliamuru wenzake na yeye wanifuate chumbani.
Sasa nyumba yote ikawa ni maombi tu. Kukemea kwa sana hali iliyonizidishia maumivu makali sana ya kuchomwa moto mwilini. Nilianza kujinyonganyonga kuashiria kwamba, maumivu ya moto niliyasikia kwa undani zaidi kuliko awali.
Nikawaona wale jamaa zangu nao wamejitokeza. Sasa ikawa wamejitokeza laivu!!
Je, wewe msomaji unajua kilichotokea?