Mkasa wa kweli: Kilichonitokea baada ya kubakwa na kaka yangu

Mar 17, 2020
46
63
MTUNZI: KULWA MWAIBALE






MWANZO




Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni yatima niliyezaliwa peke yangu kwa wazazi wangu ambao sikubahatika kuwaona, kwa sasa naishi jijini Dar es Salaam.
Kutokana na mikasa niliyopitia maishani mwangu, sitapenda kuliweka wazi jina langu halisi ila nitambue kwa jina la Dorcas.
Kwa mujibu wa mama niliyejikuta nipo mikononi mwake kimalezi, mama yangu yangu alikuwa mtu wa Rukwa na baba yangu alikuwa raia wa Zambia aliyekuwa akifanya biashara za bidhaa tofauti pamoja na samaki kutoka Ziwa Tanganyika eneo la Nkasi na kuwapeleka kwao Zambia.
Nilielezwa kwamba, mama na baba walikutana Kilando Namanyele, Rukwa wakaanzisha uhusiano wa kimapenzi ambao ulisababisha kupata ujauzito ambao mama aliubaini baada ya baba kurudi kwao.
Nilielezwa na mama huyo ambaye alifahamiana na mama mjini Sumbawanga katika biashara zao kwamba, mama alipobaini alikuwa mjamzito alitarajia baba akifika Kilando angemfahamisha kuhusu hali yake.
Jambo la kusikitisha ni kwamba baba hakurudi tena Tanzania ambapo mpaka leo haijulikani kama alikufa au alikumbwa na masaibu gani.
Kwa mujibu wa mama huyo ambaye naye hivi sasa ni marehemu, mama aliyekuwa amepanga chumba eneo la Chanji Sumbawanga aliendelea kuilea ile mimba peke yake.
Mama mlezi aliniambia kwamba, mama alipokaribia kujifungua alikwenda kwao Mpanda ili Mungu atakapomsaidia kujifungua salama awe chini ya uangalizi wa wazazi na ndugu zake.
Rafiki huyo wa mama aliniambia alimfanyia maandalizi ya safari ambapo mama alikwenda Mpanda akajifungua salama na kurejea Sumbawanga mjini kuendelea na maisha.
Aliongeza kunieleza kwamba, waliendelea kushirikiana na mama waliyeitana mtu na mdogo wake kiasi cha watu ambao hawakuwafahamu vizuri kudhani walikuwa ndugu wa damu.
Maisha yaliendelea lakini kutokana na mama kuwa na mtoto mdogo yaani mimi, hakuweza kusafiri kwenda mbali zaidi ya kuwa bize kunilea na kufanya biashara ndogondogo.
Nilielezwa kuwa nilipofikisha miezi sita, mama aliondoka na mimi kwenda mkoani Mbeya kwa rafiki yake waliyesoma pamoja aliyemuomba aende huko wakashirikiane kufanya biashara.
Kufuatia ombi hilo la rafiki yake, mama alikwenda Mbeya na kufikia Isanga ambapo rafiki yake huyo ambaye ni Mnyakyusa wa Masukulu wilayani Rungwe alikuwa amepanga chumba.
Mama huyo alinieleza, mama na rafiki yake huyo walikuwa wakifanya biashara ya kununua marahage, mchele na mahindi na kwenda kuyauza.
Wakati mwingine, siku ya Jumanne na Ijumaa ambayo inakuwa na mdana sehemu inayoitwa Kiwira, walikuwa wakienda kufanya biashara huko.
Aliongeza kunieleza kuwa, kwa vile hawakuwa na mtaji mkubwa walikuwa wanapata fedha kiasi walizoendeshea maisha yao huku mama akinilea.
Baada ya mama kukaa Mbeya kama miezi sita alikutana na mama mmoja wa Sumbawanga ambaye alikuwa akifahamu uhusiano wake na baba akamwambia aliwahi kumuona baba akifanya biashara zake Nkasi.
Kufuatia habari hiyo ambayo kwa mama ilikuwa njema sana, aliamua kurudi Sumbawanga kwa lengo la kwenda Nkasi akiwa na imani kabisa angeweza kukutana na baba.
Lengo lake lilikuwa ni kumuonesha mwanaye (mimi) na kama angekuwa tayari waanze kuishi maisha ya mume na mke.
Yule mama alinieleza, alipomshirikisha rafiki yake wa Mbeya alifurahi sana. Baada ya maandalizi tuliondoka na mama kwenda Sumbawanga na kufikia kwa rafiki wa mama aliyekuwa anaitwa mama James.
Sumbawanga tulikaa wiki moja tukaenda Kirando lengo likiwa ni kumtafuta baba..
 
SEHEMU YA 02




Mpenzi msomaji, toleo lilipita niliishia pale mama yake Dorcas akiwa na mama yake walipokwenda Kirando Rukwa lengo la mama huyo lilikuwa kumtafuta mzazi mwenzake ambaye tangu alipompa ujauzito hawakuonana. Je, alifanikiwa? Endele mbele…
Baada ya kuwasili Kirando, tulifikia kwa mama mmoja Mfipa ambaye alitupokea vizuri, mama huyo na mama walikuwa wanafahamiana vizuri.
Kwa mujibu wa mama huyo, siku iliyofuata, tulikwenda Nkasi ambako baba alikuwa akipeleka biashara zake na kuwauliza watu kama walikuwa wakimuona.
Jambo la kusikitisha ni kwamba, tulipofika huko baadhi ya watu walisema waliwahi kumuona na wengine walisema hawakuwahi kumuona muda mrefu.
Mama huyo alisema kwa jinsi mama alivyokuwa akihaha kumtafuta baba, wapo wanaume waliomtania kwamba kama angewakubalia walipokuwa wakimtokea asingepata tabu lakini kwa kuwa ‘alimshobokea’ Mzambia ndiyo ilikuwa faida yake.
Aliongeza kuwa, kauli za watu hao zilimuumiza mama ambaye licha ya kukaa kule mwezi mmoja akiamini siku moja baba angefika na kuonana naye hazikuzaa matunda.
Baada ya mama kukaa muda huo alikata tamaa akarudi Sumbawanga kwa rafiki yake ambapo aliendelea na biashara zake huku akinilea.
Niliambiwa kwamba wakati wa udogo wangu sikuwa nasumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara na watu walikuwa wakimpongeza mama kwa kunizaa mtoto mzuri.
Maisha yaliendelea huku mama na rafiki yake wakifanya biashara ndogondogo lakini baada ya mwaka mmoja, Yule rafiki wa mama wa Mbeya alimtumia ujumbe kwamba alimhitaji aende huko.
Tulikwenda Mbeya, ambapo mama aliendelea na maisha. Kwa bahati mbaya sana kwa muda wote huo mama hakuwahi kunipeleka Mpanda ili nikaujue ukoo wake.
Nikiwa na miaka minne tukiwa Mbeya, aliwahi kuja mwanaume mmoja ambaye mama alinitambulisha kwamba alikuwa mjomba wangu.
Mama alinitambulisha kwamba mjomba wangu huyo alikuwa anaitwa Samweli na kwamba alikuwa akiishi Morogoro alikokuwa akifanya kazi katika mashamba ya miwa ya Mtibwa.
Mjomba wangu alifurahi sana kuniona, siku hiyo hiyo alipokula alituaga kwamba anakwenda Tunduma kasha Mpanda kuwasalimia wazazi na ndugu wengine.
Ingawa nilikuwa mdogo nilitamani sana kuongozana naye lakini mama aliniambia tungeenda wote atakapopata muda, nikamwambia sawa na maisha yakaendelea.
Kwa kuwa nilikuwa mtundu sana, nikiwa na miaka mitano nilipelekwa katika shule moja ya chekechea ambayo haikuwa mbali na eneo tulilokuwa tukiishi.
Maisha yaliendelea hadi nilipoanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Isanga, kwa kuwa kipindi hicho nilikuwa nina ufahamu nilitamani sana kumuona baba.
Kila nilipokuwa nikimuuliza mama baba yangu alikuwa wapi, alikuwa akiniambia alikuwa nchini Zambia, nilipomwambia lini angenipeleka nikamuone akawa ananidanganya tu siku zikawa zinakwenda.
Kuna wakati nilipokuwa namuuliza alikuwa akikosa raha na kuanza kulia, nilipohoji sababu za kulia alikuwa akinidanganya kwamba alikuwa anaumwa.
Ukweli ni kwamba kitendo cha mimi kutaka kumuona baba yangu ambaye hakujua alikuwa wapi kilimuweka katika wakati mgumu sana.
Nakumbuka siku moja rafiki yake ambaye nilikuwa namuita mama mkubwa, aliniita; “Mwanangu Dorcas!”
Nilipoitika aliniambia nikakae karibu yake, wakati huo mama alikuwa amekaa kwenye kiti kilichokaribiana naye.
“Dorcas!” mama huyo aliniita tena.
Nilipoitika aliniambia kwamba nilikuwa mtoto mzuri sana na mwenye akili nyingi, nikamshukuru, wakati huo sikujua mama mkubwa alitaka kuniambia nini.
Je, kiliendelea nini?
 
SEHEMU YA 03





Nilipomwambia ndiyo, akasema baba yangu alikuwepo hivyo nisiwe na wasiwasi ipo siku nitamuona kikubwa kuomba uzima, akaniomba nisiwe namuuliza mama kila wakati habari za baba.
Baada ya mama mkubwa kutoa kauli hiyo, mama alinitazama kwa huruma akaanza kulia, mama mkubwa akaanza kumbembeleza na kumsihi anyamaze kwani haikuwa vizuri.
“Dada naumia sana niache nilie tu!” mama alimwambia mama mkubwa.
Kitendo cha mama kulia, kilinihuzunisha sana nami nikajikuta nalia bila kujua kilichomliza mama, mama mkubwa akawa na kazi ya ziada kutunyamazisha.
Mama alipoendelea kulia, mama mkubwa aliniambia niende nikacheze na wenzangu, nikatoka ndani huku nikiwa sina amani kwani kitendo cha mama kulia kiliniumiza sana.
Nikiwa nimesimama kibarazani, nikawa natafakari kilichokuwa kikimliza mama nikahisi huenda baba yangu alifariki dunia lakini walinificha kuniambia ukweli.
Baada ya kuwaza sana, niliamini baba alifariki nikaanza kulia kisha nikaingia ndani ambapo mama mkubwa na mama waliniuliza nilikuwa nimepatwa na nini.
Kwa kuamini mawazo yangu, niliwaambia kwa nini walikuwa hawataki kuniambia ukweli kama baba yangu alikuwa amefariki, wote walipata fadhaa.
Mama mkubwa aliniambia nisogee karibu yake ambapo alinipakata na kuniambia niondoe mawazo hayo kabisa kwani baba alikuwa hai ila alikuwa Zambia.
Baada ya kuambiwa hivyo na kubembelezwa nilipata amani ya moyo, nilinyamaza nikatoka mapajani mwa mama mkubwa nikaenda nje nikaanza kuosha vyombo sikujua mama zangu waliendelea kujadili nini.
Mwezi wa nne tangu nilipoanza shule, mama alipata tena habari kwamba baba alikuwa akionekana Nkasi, bila kuchelea aliondoka na kuniacha na mama mkubwa akaenda huko kama mwanzo akiamini angekutananye.
Mama akiwa huko, mara kwa mara mama mkubwa alikuwa akiniambia nisiwe napenda kumuuliza mama kuhusu alipokuwa baba, nilipomuuliza sababu aliniambia ipo siku ningekutana naye.
Binafsi nilikuwa nakosa amani ya moyo nilipokuwa nikiwaona wenzangu ambao walikuwa wakilelewa na baba zao ndiyo maana nilikuwa siwezi kutulia bila ya kumbana mama anieleze alipokuwa baba.
Kama ilivyokuwa awali, baada ya mama kukaa Nkasi majuma mawili alirejea na kutufahamisha kwamba licha ya kuwa kule kwa muda ule hakuweza kumuona baba.
Mama alipotueleza hivyo, alianza kulia na kusababisha mashavu yake kuwa na michirizi ya machozi, mama mkubwa akapata kibarua cha kumbembeleza.
Kwa kuwa tayari nilikuwa nina ufahamu, nilimuuliza mama sababu hasa ya kulia kila nilipomhoji habari za baba ilikuwa nini, akaniambia alikuwa akiumia sana mimi kutomuona baba yangu.
Aliongeza kuwa, kikubwa zaidi kilichokuwa kikimuumiza ni pale nilipokuwa nambana kwa maswali aliko baba yangu ambaye hata yeye hakufahamu.
Wakati huo nilikuwa sielewi kama mama alijutia sana kitendo cha kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hakumfahamu kiundani wala ndugu zake na kufikia hatua ya kupata ujauzito.
Ingawa kitendo cha kutomuona baba kilinikosesha raha sikuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea na maisha, hata hivyo wenzangu walipokuwa wakiletewa zawadi na wazazi wao nilikuwa nikimfuata mama na kumwamba nami baba yangu angekuwepo ningepewa zawadi.
Ili kuniweka sawa, mama aliniambia nikiwaona wenzangu wamenunuliwa au kufanyiwa jambo lolote zuri na baba zao niwe ninamwambia kama ni nguo aninunulie nk.
Kweli tangu siku hiyo kila ilipotokea wenzangu wamenunuliwa nguo, viatu au kufanyiwa jambo lolote na baba zao, waliponiambia nami nilikwenda kumwambia mama.
Licha ya mama kuwa na kipato kidogo alikuwa akifanya juu chini kuhakikisha ananiweka sawa kwa kuninunulia chochote ambacho wenzangu walifanyiwa na baba zao.
Miongoni mwa marafiki zangu waliokuwa wakiniweka katika wakati mgumu na kutamani kuishi na baba yangu alikuwa Atuganile ambaye baba yake alikuwa bosi kazini kwao na mfanyabiashara.
Msichana huyo alikuwa anapendwa sana na baba ambaye kila alipopata nafasi alikuwa akimtoa ‘out’ na kumununulia nguo, viatu na vitu vingine mara kwa mara.
Zaidi ya yote kila alipokuwa akimpeleka sehemu za kucheza watoto walitumia gari, nilitamani sana na kuzungumza moyoni kwamba kama name ningekutana na baba yangu angenifanyia hayo.
Kila nilipowaza hivyo, nilikuwa namfuata mama na kuanza kulia nikimtaka anioneshe baba yangu, mama akaishia kulia kwani hakujua angempata wapi.
Tuliendelea kuishi na mama mkubwa aliyekuwa akinipenda sana hadi nilipofika darasa la nne, kipindi chote hicho mama hakuwahi kunipeleka Rukwa.
Mpaka sasa nashindwa kuelewa sababu iliyomfanya mama ashindwe kunipeleka huko licha ya mara kwa mata tulipofunga shule kumwambia anipeleke nikawafahamu babu, bibi na ndugu wengine.
Siku moja nilimbana anitafutie nauli kisha anielekeze ningefika, lakini alinipiga chenga kwamba kipindi kile cha Juni Rukwa kulikuwa na baridi hivyo ningeweza kupatwa na maradhi ya pumu ambayo yalikuwa ya hatari.
Kwa kuwa aliyeniambia hivyo alikuwa mama yangu, niliamini kauli yake, maisha yakaendelea huku nikizidi kupendwa shuleni na nyumbani kutokana na kumheshimu kila mtu.
Kwa upande wa shuleni, walimu walinipenda sana kwani nilikuwa nina akili, msafi nisiyependa mambo ambayo hayakuwa na maana.
Nilipofika darasa la tano siku moja mama mkubwa aliporejea nyumbani kutoka kwenye biashara zake aliongozana na mama mmoja.
Tukiwa tumeketi ndani, alitutambulisha na mama kwamba yule mama alikuwa rafiki yake waliyekutana kwenye mambo ya baishara na kwamba alikuwa akiishi Shinyanga.
Mama yule aliyeonekana alikuwa na uwezo alifurahi kutufahamu na kwa muda mchache aliokuwa pale nyumbani alitokea kunipenda.
Baada ya maongezi, mgeni huyo ambaye alisema alikuwa safarini kwenda Tunduma alinipatia shilingi elfu tano na kuahidi kupita tena wakati akirudi Shinyanga.
Kabla ya kuondoka aliwapatia mama na mama mkubwa kiasi cha fedha ambacho sikukifahamu, tulimshukuru ndipo aliagana akina mama wakamsindikiza.
Akina mama waliporejea, mama mkubwa alitueleza kwamba alifahamiana na yule mama miaka minne iliyopita baada ya kumsaidia kujumua maharage Mbozi na kumuunganisha na jirani yake aliyekuwa akilima mpunga Usangu.
Tangu wakati huo kila yule mama alipokuwa akienda Tunduma kununua nguo na vitu vingine alikuwa akimtembelea japo hakuwa akilala pale nyumbani.
Mama mkubwa alisema, urafiki wao ulikomaa na kuwa kama ndugu ambapo mama mkubwa alikuwa akimuita yule mama dada.
Kama yule mama alivyoahidi, siku mbili baadaye alirejea kutoka Tunduma na kuja Isanga ambapo kila mmoja wetu alimletea zawadi, akina mama walipewa suti na mimi nilipewa gauni zuri sana.
Baada ya kupiga stori za hapa na pale, alituaga ambapo aliondoka na gari binafsi kuelekea jijini Dar es Salaam alikokuwa anafuata mizigo flani kisha aende Shinyanga.
Usiku wa siku hiyo, baada ya kula mama alimsifia sana yule mama wa Shinyanga kwamba alikuwa mkarimu, mcheshi na mwenye upendo wa dhati.
“Ni kweli kabisa unachosema, mimi amenisaidia sana na aliwahi kuniambia asingekuwa na majukumu makubwa ya kuilea familia baada ya mumewe kufariki angeniongezea mtaji,” mama mkubwa alituambia.
Kufuatia kauli hiyo, mama alisikitika sana na kusema:
“Kumbe yule mama ni mjane? Kweli amepata pigo kubwa sana!”
“Ndiyo hivyo, Mungu akiamua kumchukua mtu wake achagui atangulie nani ndicho kilichotokea kwa mama Evance, mume wake katangulia,” mama mkubwa alituambia.
ITAENDELEA
 
We kijana rudi haraka sana na mwendelezo atutaki arosto na story nzuri nzuri Kuja upesi tunakusubili 😉
 
SEHEMU YA 04




Kutokana na ukarimu aliokuwa nao mama huyo, mama alihuzunika sana alipoambiwa kwamba mumewe alikuwa amefariki dunia ndipo alimwuliza mama mkubwa kama alikuwa na watoto.
“Aliniambia kwamba ana watoto watatu, wawili wa kike na wa kiume anaitwa Evance,” mama mkubwa alimfahamisha mama.
Mama na mama mkubwa waliendelea kumzungumzia mama huyo wa Shinyanga jinsi alivyokuwa na upendo kwa watu wengine ndipo niliwaacha na kwenda kulala.
Katikati ya usingizi niliota ndoto tupo sokoni mama ambapo alikuwa akiuza mchele na watu walikuwa wengi sana, wakati mama akiwa bize kuwahudumia wateja mtu nisiyemfahamu alinigusa begani.
Nilipogeuka kumwangalia, alikuwa ni mtu mzima ambaye alitabasamu na kunionesha mwenzake na kuniuliza:
“Unamfahamu huyu hapa?”
Kabla sijamjibu, mama aliyewasikia watu hao alipogeuka kuwaangalia aliruka kwa furaha na kumkumbatia yule bwana niliyeulizwa kama nilikuwa namfahamu.
“Gilbert, hivi ni wewe kweli au naota ndoto ya mchana, siamini macho yangu!” mama alimwambia yule bwana.
Jamaa huyo akiwa amekumbatiana na mama huku akitabasamu, alimjibu kwamba alikuwa yeye ndipo mama aliniita na kunifahamisha kuwa yule alikuwa baba yangu.
Kama alivyofanya mama, nami kwa furaha nilimkumbatia baba yangu na kuanza kulia huku nikimuuliza alikuwa wapi muda wote.
Baba ambaye alikuwa amepigwa butwaa kuambiwa mimi nilikuwa mwanaye, akamuuliza mama nilikuwa mwanaye kivipi, ile mama anataka kumwambia nilishtuka kutoka usingizini.
Ndoto hiyo ilinikosesha raha sana nikajikuta ninalia kwa sauti kitendo kilichosababisha mama mkubwa na mama kuamka na kuingia chumbani kwangu kujua nilipatwa na nini.
“Dorcas mwanangu umepatwa na nini mbona unalia?” mama aliniuliza.
Baada ya kuwaona akina mama nikazidisha kulia bila kuwaambia sababu, mama mkubwa aliketi kwenye mfumbati wa kitanda na kuanza kuniuliza sababu ya kulia.
“Nimemuona baba yangu, lakini kabla sijazungumza naye ameondoka,” nilimwambia mama mkubwa.
Kauli yangu iliwashtua ambapo mama aliniuliza baba yangu nilimuona wapi na kusema mbona niliwaacha njia panda!
Niliwafahamisha kwamba nilimuona kwenye ndoto, akiwa na rafiki yake kisha kwa hamaki nikamwambia mama nilimtaka baba yangu, kauli ambayo ilimuumiza sana akaanza kulia.
Kitendo cha mama kulia, kilinifanya nami niendelee kulia, mama mkubwa akawa na kazi ya ziada ya kutubembeleza kisha aliniita:
“Dorcas!”
Nilipoitika aliniuliza kwa nini nilikuwa namuweka mama katika wakati mgumu na kwa nini sikupenda kumuelewa aliponiambia nivumilie ipo siku ningekuja kumuona baba yangu!
Kufuatia kuniuliza hivyo, nilimwambia kilichoniliza ni kitendo cha baba kunijia kwenye ndoto wakati nilitamani sana kumuona laivu ili nami nifurahi naye kama wenzangu.
Kama ambavyo alikuwa akifanya mara kwa mara nilipokuwa nalia kuhusu kuhitaji kumuona baba, aliniomba nisilie na kunipa moyo kwamba ipo siku ningekutana naye.
“Mwanangu Dorcas, kwa kuwa umeanza kumuota baba yako ni dalili kwamba karibu mtaonana, hivyo kuwa na subira, sawa mama?” Dorcas alimkalili mama mkubwa.
Nilimwambia sawa japo sikufahamu ningeonanaje na baba yangu ambaye katika ndoto niliyoota nilisikia mama akimwita kwa jina la Gilbert.
Baada ya mama mkubwa kuniambia hivyo alinieleza nilale kwa amani kisha wakaniacha na kwenda kulala chumbani kwao, sikujua walichoongea huko.
Japo nilikuwa bado mdogo, nikiwa nimejilaza kitandani, sikuweza kupata usingizi kwa wakati kwani muda mwingi nilikuwa namuwaza baba yangu.
Hata hivyo, baadaye nilipitiwa na usingizi hadi nilipokuja kushtuka saa kumi na moja alfajiri na kujikuta kichwa kikiuma sana.
Kutokana na maumivu niliyopata nikaanza kulia na kumwita mama, wote waliamka na kuja chumbani nilikokuwa nalala wakifikiria sababu iliyoniliza ilihusu baba.
Mama mkubwa aliponiuliza nini kilinisibu niliwaambia kichwa kilikuwa kinauma sana, waliniuliza kilianza muda gani niliwafahamisha kwamba ni baada ya kushtuka kutoka usingizini.
Kwa kuwa ndani kulikuwa na panadol, mama mkubwa alizifuata pamoja na maji nikameza kisha akaniambia nilale kitapoa, cha kusikitisha ni kwamba sikupata nafuu.
Haukupita muda mrefu nikaanza kulia kwa sauti huku nikipiga kelele, mama mkubwa akamwambia mama alihisi malaria ilipanda kichwani.
Kutokana na hali niliyokuwa nayo, baadhi ya majirani zetu waliamka na kuja kujua sababu ya kulia kwangu, wakawaambia walihisi malaria ilipanda kichwani.
Akina mama walijiandaa, wakaniandaa na kunipeleka kwenye zahanati moja iliyopo Isanga, daktari aliyekuwepo zamu baada ya kuona situlii, kwa mujibu wa mama mkubwa, alinichoma dawa ya usingizi, nikalala.
Nililala saa nzima, dawa hiyo ilipoisha nguvu niliamka na kujikuta nimepumzishwa pale hospitali nikawauliza nilipatwa na tatizo gani, mama akaniambia nilikuwa naumwa.
Tukiwa tunazungumza na mama, yule daktari aliingia akaniita jina langu na kusema: “ Unajisikiaje sasa?”
Nilimwambia nilihisi kichwa kuniuma akanipa pole na kuniambia nilikuwa nina malaria, kumbe tayari alinichukua damu na kuipima.
Baada ya daktari huyo kuniandikia dawa alimpa mama maelezo ya namna ya kutumia kisha alinitania kwamba niache uoga wa kuumwa, tukarejea nyumbani huku kila mmoja wetu akiamini nilikuwa naumwa malaria.
Kama mama alivyokuwa amepewa maelezo na daktari, baada ya kula alinipatia dawa kisha nilikwenda kulala, mama mkubwa alikwenda kwenye biashara zake na kumuacha mama aliyekuwa akiniangalia.
Siku hiyo nililala hadi alasiri, nilipoamka nilijisikia nimepata nafuu jambo lililomfarahisha mama. Hata mama mkubwa aliporejea na kunikuta katika hali hiyo alifurahi.
Kufuatia kuumwa, sikwenda shuleni siku tatu hadi nilipopa kabisa. Tangu nilipougua nilimaliza wiki mbili ndipo nilianza kutokewa na vitu vya ajabu nikiwa nimelala.
Siku moja nikiwa nimelala chumbani nilijikuta nikikabwa shingoni na mtu ambaye sikumuona, kila nilipojaribu kuwaita akina mama sikuweza kufanikiwa kwani sauti haikutoka.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye mtu huyo alianiachia nilipotazama ukutani niliona kama kimvuli cha mtu kikiishia ndipo nikaanza kuwaita akina mama.
Mama mkubwa na mama walipoingia chumbani kwangu walinikuta nimekaa kitandani huku nikihema, mama aliponiuliza nilipatwa na nini nikawaeleza.
“Huenda ulipolala uliangalia juu, mara nyingi mtu akilala chali huota ndoto za kukabwa,” mama mkubwa aliniambia.
Kwa kuwa sikulala chali niliwaambia, mama mkubwa akasema basi kulikuwa na jinamizi lilikuja kunisumbua, kwa hofu niliyokuwanayo niliwaambia siwezi kulala peke yangu mle chumbani.
Akina mama walikubaliana nami tukaenda chumbani kwao ambako tuliendelea kuongea kuhusu jinamizi hilo.
Mama mkubwa alisema alishangazwa sana na jambo hilo kwani tangu alipohamia pale aliwahi kukabwa mara mbili tena zamani, baada hapo haikuwahi kutokea tena.
Kulipokucha nilijiandaa, kutokana na baridi ya Mbeya nilikunywa chai na kipande cha mkate mweusi ulioandaliwa na mama mkubwa ambaye alikuwa akipenda sana kitafunwa hicho kisha niliwaaga akina mama.
Wakati wa kwenda shuleni ilikuwa lazima nipite kwenye uwanja wa nyumba ya mama mmoja sitapenda kumtaja kwa jina, nikamkuta akifagia, nilipomsalimia hakuitikia.
Awali nilifikiriA hakunisikia, nikamwamkia tena akawa bize kufagia, nikaamua kumuacha nikaongeza mwendo kuelekea shuleni lakini nikawa najiuliza nilimkosea nini yule mama mpaka asiitikie salamu yangu.
Hata hivyo, kwa akili za kitoto wala sikumfuatilia. Nilipofika shuleni, tulifanya usafi wa mazingira kisha tuliingia darasani tayari kwa kuanza vipindi.
Nakumbuka siku hiyo mwalimu wa kwaza kuingia darasani alikuwa wa kipindi cha hesabu, alipokuwa akitufundisha ghafla nilihisi kichwa kuniuma.
Mwanzo nilifikiria kingepoa lakini kadiri muda ulivyosonga mbele kikazidi kuniuma, nikainama chini ya dawati.
Mwalimu aliponiona aliniuliza sababu za kuinama chini, nilimwambia kichwa kilikuwa kinauma, jambo la kushangaza nilipomweleza hivyo mwalimu, kichwa kikazidi kuuna nikashindwa kuvumilia nikaanza kulia.
Yule mwalimu kwa kushirikiana na wanafunzi watatu walinibeba na kunipeleka ofisini ambako niliendelea kulia, mwalimu alimuuliza mmoja wa wale wanafunzi kama alikuwa akipahamu nyumbani ili akamwambie mama.
Kwa kuwa yule mwanafunzi alikuwa anapajua nyumbani, alikwenda mbio, kwa bahati mbaya hakumkuta mama wala mama mkubwa kwani walikuwa wamekwenda kwenye biashara zao.
Kwa kuwa kutoka pale shuleni kwenda ilipokuwa zahanati hapakuwa mbali, walimu wawili na mwanafunzi mmoja walinipeleka, nikafanyiwa kipimo cha malaria.
Majibu yalipotoka sikuwa nayo, nilipewa dawa ya kutuliza maumivu, hata baada ya kumeza bado kichwa kilikuwa kikiuma sana.
Wakati walimu na daktari wakitafakari, akina mama walipopewa taarifa nwa mwanafunzi mmoja walifika na kuniuliza nini kilikuwa kikinisumbua, kwa shida niliwaambia kichwa.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 05




Baada ya akina mama kufika, mama mkubwa aliniuliza nini kilinisumbua kufikia hatua ya kulia, nilimwambia kichwa, akaniuliza kilinianza saa ngapi nikawaambia.
Mama alipomuuliza daktari kuhusu matibabu, alimweleza alikwisha nipima kwa lengo la kujua kama nilikuwa na malaria lakini sikuwa nayo.
Kufuatia hali hiyo daktari alishauri niendelee kutumia dawa za kutuliza maumivu na kama hali ingekuwa si shwari wanirudishe tena pale hospitali.
Akina mama walipopewa ushauri huo, tulirudi nyumbani lakini wakati huo nilikuwa nimepata nafuu kiasi, nafikiri ni kwa vile niliwaona wazazi wangu.
Tulipofika nyumbani, mama mkubwa aliniandalia uji wa ulezi, nilipokunywa nilikwenda kulala kisha nikapitiwa na usingizi kwa muda mrefu.
Nilipoamka kichwa kilianza kuniuma sana, nilishindwa kuvumilia nikaanza kulia, akina mama walinipeleka tena pale zahanati.
Kutokana na hali niliyokuwanayo, daktari alishauri wanipeleke Hospital ya Rufaa ya Mbeya, walikodi gari na kunipeleka huko.
Daktari wa hospitali hiyo alinipima tena malaria, sikuwa nayo ndipo alinilaza kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini kilichokuwa kikisababisha kichwa kuuma.
Nikiwa nimelazwa pale, daktari alishauri niwe napewa maji mengi na kutumia dawa za maumivu, kesho yake jioni kichwa kiliacha kuuma na siku iliyofuata niliruhusiwa kurudi nyumbani.
Baada ya kukaa nyumbani siku mbili kwa ajili ya mapumziko ya kuumwa, nilianza masomo bila kujua mbele yangu hakukuwa na amani.
Niliendelea na masomo kwa muda wa miezi miwili bila kusumbuliwa na jambo lolote ndipo siku moja usiku nikiwa nimelala nilishtuka usingizini kufuatia kusikia watu wakicheka.
Nilipoamka zile sauti sikuzisikia, nikawa najiuliza kama nilikuwa naota au lilikuwa tukio halisi, hata hivyo baadaye niliamua kulala nikapitiwa na usingizi.
Katikati ya usingizi, nikasikia tena watu wakipiga filimbi, kucheka na wengine wakizomea, nikaamka kama ilivyokuwa awali wale watu sikuwasikia tena.
Kitendo hicho kiliniogopesha nikaamka na kwenda kwenye mlango wa chumba cha akina mama, nikawaita, mama aliamka na kuniuliza sababu za kuwaamsha.
Niliwasimulia kila kitu, lakini cha kushangaza mama alisema zilikuwa ndoto za kawaida, hata hivyo niligoma kwenda kulala chumbani kwangu.
“Na wewe Dorcas unaonekana muoga sana, hata mambo unayoota yanakuogopesha?” Dorcas anasema mama yake alimwambia.
Kulipokucha, nilijiandaa na baada ya kunywa chai niliwaaga akina mama nikaondoka kuelekea shuleni.
Kama ilivyotokea siku ile, nilipopita nyumbani kwa yule mama ambaye hakuitikia salamu yangu, kama kawaida yake ya kupenda kufanya usafi asubuhi na mapema, nilimkuta akifagia.
Kwa kuwa ni jirani yetu na ninamheshimu kama mzazi wangu, nilimwamkia kwa uchangamfu lakini hakunichangamkia na wala hakuitikia salamu yangu.
Kufuatia kitendo hicho kujirudia mara mbili, nilihisi huenda nilifanya kosa ambalo sikulielewa, nikamuuliza na kumuomba kama nilikosea sehemu anisamehe.
Jambo la kushangaza, aliniangalia kwa dharau kisha akaendelea kufagia, nikaamua kuelekea shuleni huku nikijiuliza sababu za mama yule kunifanyia vile.
Nikiwa njiani nilipanga nikifika nyumbani niwaeleze akina mama kuhusu yule mama ambapo niliamini wangeenda kuzungumza naye kwa lengo la kujua sababu ya kutoitikia salamu yangu.
Kama ada, nilipofika shuleni tulifanya usafi wa mazingira kisha kengele ya kuingia madarasani iligongwa, wanafunzi wote tulikusanyika kwa ajili ya kukaguliwa usafi.
Nikiwa nimesimama mstarini, ghafla nilipata kizunguzungu nikaanguka na kupoteza fahamu, nilipozinduka nilijikuta nikiwa kwenye ile zahanati ya karibu na shule.
Niliwaona akina mama, walimu wawili na madaktari wawili, mama akaniita; “Dorcas!”
Baada ya kuitika akaniuliza nilipatwa na nini, sikumjibu kwani nilikuwa najiuliza nilikuwa wapi na nilifikaje pale, nikamuuliza pale nilifikaje!
Mama aliniuliza kwani sikukumbuka chochote kilichonitokea mpaka nikapelekwa pale? Nikamwambia sikukumbuka ndipo daktari mmoja akasogea, akanishika kichwani na kuniuliza:
“Sasa unajisikiaje?”
Nikiwa nimeshajua nilikuwa nipo hospitali, nilimwambia nilijisikia vizuri na kuomba wanieleze nilipatwa na nini kilichonifanya nilazwe wakati nilikuwa shuleni.
Yule daktari ili kuhakikisha kama nilikuwa sawa, aliniambia nivute kumbukumbu nikiwa shuleni nilipatwa na nini kisha niwaambie, nilipofanya hivyo nilikumbuka matukio yote mpaka tuliposimama mstarini na kupata kizunguzungu.
Je, nini kinasababisha Dorcas kuumwa kichwa na tukio la kupata kizunguzungu na ilikuwaje hadi akabakwa na kaka yake?
 
Dah na zimemwagwa kama mvua

Najua ni je ya mada lakini umecheki avatar yangu?
 
SEHEMU YA 06




Niliwapowaambia, mama alisema alishangazwa sana na matukio ya kuumwa yaliyokuwa yakiongozana mfululizo ambayo awali sikuwa nayo.
“Unasema, hana tatizo la kupatwa na kizunguzungu?” yule daktari alimwuliza.
Kufuatia kuulizwa hivyo, mama alimweleza yule daktari kwamba sikuwa nasumbuliwa na tatizo hilo na kwamba alishangazwa na hali hiyo iliyokuwa ikimkosesha amani.
Baada ya mama kumweleza hivyo, yule daktari aliniandikia dawa flani ambazo nilipaswa kuzitumia siku tano, akasema ikitokea tena tatizo hilo wanipeleke hospitali ya rufaa.
Alipotukabidhi zile dawa, nikiwa nimeanza kuchangamka tuliondoka pale zahanati nikiwa na walimu, mama na wanafunzi wenzangu hadi nyumbani ambapo walimu walituaga.
Kilichowaweka akina katika wakati mgumu ni kitendo cha kupata kizunguzungu na kuanguka na wakati mwingine kuumwa na kichwa maradhi ambayo sikuwa nayo.
Akina mama walishindwa kuelewa kiini cha maradhi hayo, nakumbuka hadi jioni ya siku hiyo nilikuwa nimepona na kuchangamka kama siyo mimi niliyeanguka shuleni.
Kwa kuwa nilikuwa nimeandikiwa dawa za kumeza, niliendelea nazo hadi nilipozimaliza, nikawa nahudhuria shuleni kama kawaida nikiwa buheri wa afya.
Wiki mbili baadaye, siku moja nikiwa nimelala usiku, nilihisi nywele kunisisimka pamoja na mwili, nilipoamka niliona kimvuli cha mwanamke aliyenipa mgongo kikiishia kupitia kwenye kingo za ukuta.
Awali nilijiuliza niliona kitu halisi au nilikuwa naota, lakini kwa kuwa nilikuwa nimeamka niliamini yule alikuwa mtu, kwa uoga nikapiga kelele na kuwaita akina mama.
Wa kwanza kuamka alikuwa mama, ambaye tulikutana mlangoni akitaka kuingia nami nikitaka kutoka, akaniuliza kulikoni, nikamwambia nimemuona mtu chumbani kwangu.
Kauli yangu ilimshtua na kuniuliza huyo mtu aliingiaje, nilimfahamisha sikuelewa, wakati tukizungumza na mama, mama mkubwa alikuwa yupo jirani yetu.
“Mama Dorcas, vipi mtoto amepatwa na nini?” Dorcas anasema mama mkubwa alimwuliza.
Kama nilivyomwambia, naye alimjulisha mama mkubwa ambaye alishangaa na kuhoji kama yule mtu bado alikuwepo.
Niliwafahamisha kwamba alitoweka ghafla kwa kupitia pembe ya ukuta, nilipotoa kauli hiyo, mama mkubwa alisema alihisi hakuwa mtu nilikuwa naota ndoto.
Niliwahakikishia kwamba sikuota ni kweli nilimuona laivu mtu akitoka huku kanipa mgongo, akina mama wakabaki wakishangaa nilichowaambia.
Mama mkubwa aliniambia twende tukalale chumbani kwao huku akisema huenda kuna mchawi alikuwa akija kunisumbua usiku, mama alikubaliana na maneno ya mama mkubwa.
Alfajiri ya siku hiyo kichwa kilianza kuniuma sana, nikaishia kulia, mama mkubwa alinipatia panadol, hata baada ya kuzimeza hali iliendelea kuwa mbaya.
Kama walivyoshauriwa, walinipeleka hospitali ya rufaa, huko daktari aliwauliza historia ya maradha yangu wakamwambia, akasema huenda kuna tatizo kwenye mishipa flani ya kichwa changu.
Kwa kuwa kichwa kiliendelea kuniuma, nililazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku nne lakini daktari ambaye alinifanyia vipimo alisema sikuwa na tatizo na kushauri niendelee kutumia dawa za kutuliza maumivu.
Miongoni mwa akina mama waliokuwa wakija kuniona hospitali alikuwa ni mama Jacob aliyekuwa rafiki wa akina mama, mama huyo alipoona sipati nafuu alishauri nirudishwe nyumbani.
Tukiwa nyumbani, aliwaambia akina mama kwamba maradhi yangu hayakuwa bure, alihisi yalitokana na nguvu za giza akashauri nipelekwe kwa mtaalamu wa mambo ya jadi.
Baada ya kujadiliana na kufuatilia historia ya maradhi yaliyokuwa yakinisumbua, akina mama waliamini kabisa kwamba nilikuwa nachezewa na mtu, wakamuomba mama Jacob awaelekeze au awapeleke kwa huyo mtaalam.
Mama huyo alikubali, siku iliyofuata alfajiri tuliondoka Isanga kwenda Songwe, nje ya Jiji la Mbeya kwa mtaalam huyo ambapo kwenye saa moja kasoro tulifika.
Mganga huyo aliyekuwa akifahamiana vizuri na mama Jacob alitupokea vizuri, zaidi walichangamkiana sana na mama Jacob kisha alitukaribisha sebuleni kwake.
“Naona umekuja na wageni?” yule mganga alimwuliza mama Jacob ambaye aliitikia kwa kusema ndiyo.
Mama huyo alitutambulisha kwa yule mganga na kumweleza kilichotupeleka pale ni matatizo yangu, mganga akaniangalia na kunipa pole.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 07




Baada ya kunipa pole, nilimshukuru ndipo alituambia kwamba mara atakapoangalia na kuzungumza na watu wake angebaini chanzo cha matatizo yangu.
Kwa kuwa pale sebuleni hapakuwa sehemu aliyokuwa akifanyia uganga wake, alituambia mimi na akina mama twende kwenye chumba cha kazi yaani kilingeni kwake.
Mganga huyo alituongoza tukapita mlango wa uani na kutoka nje ambapo kulia mwa nyumba yake kulikuwa na nyumba ndogo ambapo nje palikuwa na mwanamke na kijana aliyekuwa akitwanga dawa na yule mwanamke alikuwa akichambua mboga ya majani.
Tulipowakabiria, wote walitusalimia ndipo yule mganga akatutambulisha kwamba yule mwanamke alikuwa mkewe na yule kijana alikuwa msaidizi wake, tukasalimiana.
Tulipofika mlangoni, yule mganga alivua ndala alizokuwa amevaa nasi tukafanya hivyo, akatukaribisha ndani, tukaingia.
Kama ilivyo kawaida ya waganga kuwa na masharti, tulipoingia aliwaambia akina mama wakae kwenye mkeka uliokuwa karibu na tunguri zake, nami akaniambia nikae juu ya ngozi nyeusi ambayo sikujua ilikuwa ya mnyama gani.
Hata hivyo, mapigo yangu ya moyo yalikwenda kwa kasi kufuatia wasiwasi niliokuwanao, nilipokaa mganga huyo alichukuwa kipande cha ngozi kilichokuwa na tundu akakivaa shingoni.
Haikuishia hapo, alichukua usinga akaushika mkono wa kushoto na kuupunga kuzunguka chumba kizima akauweka alipouchukua, akakaa kwenye kigoda cha ngozi na kupiga mbinja iliyokwenda sambamba na chafya nne.
Baada ya kufanya hivyo, alichukua tunguri iliyokuwa imevilingwa shanga akamimina kitu kama mafuta kiganganjani na kujipaka usoni.
Alipomaliza kufanya hivyo, alichukua kioo kilichotengenezewa fremu nyeusi na kuzungushiwa shanga, akaniambia niiname kwani alitarajia kuzungumza na wazee ili kujua chanzo cha matatizo yangu.
Wakati akifanya hivyo, akina mama walikuwa wametulia wakimwangalia kwa makini na woga, nilipoinama akaanza kuvuta pumzi na kusema maneno yasiyoeleweka na kutikisa kichwa.
Alifanya hivyo kama dakika tano, akaniambia niinue kichwa na kusema:
“Akina mama, kuna mtu mwanamke ndiye anamuumiza binti yenu, huyo mwanamke ni mtu mzima, kaamua kumtesa kwa wivu wake tu, kwa sababu mtoto ana nyota ya kupendwa, tena anashirikiana na mwenzake mmoja.”
Baada ya mganga kutueleza hivyo, wote tulitazamana kwani taarifa ile ilitufanya tupigwe butwaa, mganga akatuambia isingekuwa miiko ya kazi yake angetuonesha wanawake hao.
Mama mkubwa alimuomba mganga asijali atuoneshe, lakini yule kalumanzila aligoma na kutuambia atanitibu na kuondoa vitu nilivyotupiwa mwilini ambavyo vilikuwa vikinitesa.
“Ametupiwa vitu?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza yule mganga.
Mganga alitufahamisha kwamba nilitupiwa vitu vitatu, kimoja kilikuwa kichwani, tumboni na mgongoni na lengo lao walitaka nilale ndani maisha yangu yote.
Mimi na akina mama tulinyong’onyeshwa na taarifa hiyo ndipo yule mganga alisema tusijali kwani uchawi walionifanyia ulikuwa mdogo kikubwa tumtafutie kuku mweusi, kitambaa cheusi, mbegu kavu za papai, kipande cha kanga niliyokuwa nikitumia na kwamba vitu vingine angeviandaa mwenyewe.
Baada ya mganga kusema hivyo, mama aliyekuwa na dukuduku la kumjua yule mama alimuomba sana awaoneshe wale akina mama lakini yule mganga alisisitiza asingeweza kufanya hivyo.
“Ila kama mnataka niwachape kwa sababu wamemuonea tu huyu binti niruhusuni, akishapona nao nitawapa adhabu ili wakome kuwasambua watu,” Dorcas anasema mganga aliwaambia.
Mama alikubali mganga huyo kuwaadhibu watu hao lakini mama mkubwa alipinga na kusema awaache kwani Mungu pekee ndiye anayepaswa kutoa hukumu.
Baada ya mama mkubwa kusema hivyo, mganga alicheka na kusema alichosema ni sawa lakini pia kuwaadhibu watu wanaowatesa wenzao pia ni sawa.
Hata baada ya mganga kutoa kauli hiyo ya ushawishi ili mama mkubwa akubali awaadhibu wale akina mama wachawi, mama mkubwa alipinga.
Baada ya maongezi hayo, mganga aliwauliza akina mama ni lini wangeleta vitu alivyowaagiza, kwa kuwa vyote ilikuwa rahisi kuvipata walimwambia kesho yake.
“Kwa kesho hapana, nitaenda porini kuchimba dawa njooni keshokutwa au siku ninyingine yoyote,” Dorcas alimkariri mkanga huyo.
Baada ya kutuambia hivyo, mganga alivua ngozi aliyokuwa amevaa kisha tuliinuka akatuongoza kwenda nyumba kubwa tulikomuacha mama Jacob rafiki wa akina mama.
Je, kilifuatia?
 
SEHEMU YA 08





Tulipofika mganga ambaye alikuwa mkarimu sana alituuliza tulikuwa tunakunywa soda gani, wote tulimshukuru na kusema tungekunywa siku nyingine.
“Hapana, lazima mnywe soda jamani, wala hazifuatwi mbali,” Dorcas anasema mganga aliwaambia kisha alimwita kijana wake ambaye alifika haraka.
“Hebu waletee soda wageni,” Dorcas anasema mganga alimwambia kijana wake.
Yule kijana alituuliza soda ambazo tulikuwa tukinywa, aliingia chumbani akatuletea na tulipomaliza kunywa, tuliondoka nyumbani kwa mganga huyo na kuanza safari ya kurudi Mbeya mjini.
Licha ya kwamba kila mmoja alitaka kulizungumzia suala la wale akina mama walionekana kwa mganga, lakini hatukuweza kuongea ndani ya basi hadi saa nane alasiri tulipofika nyumbani.
Tukiwa tumeketi sebuleni, mama alianza kumuuliza mama mkubwa kama aliweza kuwatambua akina mama hao, mama mkubwa akasema kama waliofanya hivyo ni majirani zetu, akamtaja yule mama ambaye kila nilipomsalimia hakuitikia kwamba alikuwa mmoja wao.
Baada ya kumtaja, kwa mbali mama alionekana kuamini nami nilipokumbuka kitendo cha mama huyo kutoitikia salamu yangu nikahisi huenda ndiye aliyetajwa na yule mganga.
“Mama mkubwa nahisi hujakosea, kwa maelezo yako nahisi mama (akamtaja jina) ndiye anayemtesa Dorcas, lakini mtoto amemkosea nini?” mama alimwuliza mama mkubwa.
Hata hivyo, kwa kuwa hatukuwa na ushahidi kama ni kweli mama huyo alihusika mama mkubwa alishauri tuanze kumchunguza tungebaini ukweli.
Baada ya kusema hivyo, moyoni nilisikia sauti moja ikiniambia yule mama ndiye haswa alikuwa akinitesa, nikaanza kutafakari tabia yake ya kutoitikia salamu zangu na kuninua bila sababu.
Sikuishia hapo nilipotafakari kwa undani nikagundua karibu mara zote ambazo nilikumbwa na ugonjwa wa kuumwa kichwa na lile tukio la kuanguka shuleni, yalitokea baada ya kumsalimia yule mama na kutoitikia salamu yangu.
Nilipowaambia akina mama moja kwa moja walikubaliana nami ndipo mama mkubwa ambaye hakuwa na simile akataka kumfuata mama huyo kwa lengo la kumchana laivu lakini mama akamzuia.
“Hata kama ni kweli ndiye anayefanya hivyo, utafanya kosa kubwa sana kumfuata na kumwambia anamroga mtoto, tena akikupeleka mahakamani utaingia kwenye matatizo,” mama alimwambia mama mkubwa.
“Hapana inauma sana, mtoto kila siku anaumwa kumbe yeye ndiye anayemroga, Dorcas kamkosea nini? Ngoja nikamchane laivu,” mama mkubwa aliyepatwa na hasira alisema.
Kwa kuwa mama alijua hatari ambayo ingetokea, licha naye kuamini yule mama ndiye aliyetajwa na mganga japo hakuweka wazi, alimsihi mama mkubwa awe mpole.
“Haya, ila nafikiri keshokutwa tukienda kwa mganga tumwambie amuadhibu ili naye aonje machungu ya kuwatesa wenzake,” mama mkubwa alimwambia mama.
Pamoja na kupanga kufanya hivyo, mama alituambia kama kweli yule mama ndiye aliyekuwa akiniroga lilikuwa jambo la ajabu sana kutokana na jinsi tulivyokuwa tukicheka na kushirikiana kama majirani.
“Na wewe mama Dorcas, hivi huwajui wachawi walivyo, huwezi kuwadhania na ni wapole na wenye upendo lakini ni balaa kwa kuwatesa watu,” mama mkubwa alimwambia mama.
Baada ya maongezi yaliyochukua muda mrefu mama akainuka na kusema tangu tulipofika tulifikia kumzungumzia Yule mama na kusahau kama hatukula.
Kwa kuwa ndani kulikuwa na mboga, akaniambia niwashe mkaa kisha niinjike maji ya kusongea ugali, mama mkubwa huku akionekana kuwa na jazba na Yule mama akainuka na kwenda chumbani.
Tulipomaliza kula, mama mkubwa alikwenda sokoni kununua vile vitu tulivyoagizwa na mganga, kwa upande wa mama akaenda kuoga. Siku hiyo hawakwenda kabisa kwenye biashara zao.
Siku ya tatu, tukiwa na vitu alivyotuagiza mganga huku tukiwa tayari tumeshamjua mbaya wetu, alfajiri tuliondoka kuelekea Songwe kwa mganga, lakini hatukuwa na mama Jacob.
Tulipofika mganga alitupokea na kutupeleka kilingeni kwake, kwa kuwa tayari alikwisha niagua, sikukaa kwenye ile ngozi nyeusi bali nilikaa kwenye jamvi na akina mama.
Tukiwa pale alituuliza kama tulifanikiwa kupata vitu alivyotuagiza, mama mkubwa akasema tulivipata akammkabidhi ambapo alituambia naye alikwisha andaa vyake.
Baada ya kumkabidhi alituambia twende tukakae nje sehemu palipokuwa na viti vya wageni, tukafanya hivyo.
 
SEHEMU YA 09




Tukiwa pale tulimuona yule mganga ambaye tangu siku ya kwanza hakutuambia kuhusu malipo ya kazi yangu ingekuwa shilingi ngapi akiwa amemshika kuku mweusi mkono wa kusho na kulia alishika kisu.
Moja kwa moja tulijua alikuwa akienda kumchinja, kwa kuwa nilikuwa mdogo nilijua yule kuku alikuwa kwa ajili ya kitoweo maalumu kwa ajili yetu kwa sababu tulikuwa wageni.
Mama mkubwa alituambia kwamba kwa alivyokuwa akifahamu mambo ya waganga, japo hakutuagiza tumtafute kuku wa aina ile alikuwa ni wa dawa na lazima zingewatoka fedha alizomnunua.
“Na wewe mama mkubwa! Nani kakuambia ni kuku wa dawa?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza mama mkubwa.
“Najua tu, kwanza si mnamuona mganga kabadili nguo kavaa ile ngozi yake shingoni…nahisi ndiyo masharti ya kazi yake kumchinja kuku huyo akiwa kiganga,” mama mkubwa alituambia, tukacheka.
Wakati akina mama wanazungumza, nilikuwa makini kuwasikiliza kwani kila kilichojiri pale kilikuwa kigeni machoni pangu.
Wakati mganga huyo akimchinja yule kuku, yule kijana tuliyemkuta siku ya kwanza alitoka na kwenda upenuni palipokuwa na mtungi akachota maji na kuyaweka kwenye sufuria, alipotupia macho upande tuliokuwa tumekaa akatuona na kutusalimia.
Alipotusabahi aliingia ndani, mama mkubwa aliyekuwa akipenda sana kushadadia mambo akatuambia yale maji aliyochota yule kijana alikwenda kuyachemsha kwa ajili ya kumnyonyolea yule kuku, tukacheka.
“Mama mkubwa unaonekana unayaelewa sana mambo ya waganga?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza.
Kufuatia kuulizwa hivyo, mama mkubwa alimwambia alikuwa na uzoefu wa waganga kwa vile huko kwao, marehemu babu yake mzaa baba alikuwa mganga.
Yule mganga alipomaliza kumchinja kuku, alimwita msaidizi wake ambaye alitoka na ungo mweusi akaenda kumweka kuku kisha wakaongozana na mganga kuingia ndani.
“Mpaka kuondoka hapa leo tutajionea makubwa,” mama mkubwa alituambia kwa sauti ya kunong’ona, tukacheka.
“Kwa nini unasema hivyo?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza.
Alipoulizwa hivyo, alitaambia si tuliona tukio la kuku aliyechinjwa alivyowekwa kwenye ungo mweusi huku kichwa chake kikiwa kimewekwa juu ya kitambaa cheusi.
Ingawa katika hali ya kawaida lile tukio lilikuwa la kustaajabisha lakini tulijikuta tukicheka ndipo mama akasema kweli ukiwa na matatizo utakutana na mengi.
Baada ya kukaa kama saa moja na dakika kumi, msaidizi wa mganga alitufuta na kutuambia tuingie ndani, tulipoingia tulikuta kuna chungu cheusi kilichofunikwa kikiwa kilingeni, chupa ambayo ndani ilikuwa imejaa dawa.
Ukiacha chungu hicho, palikuwa na blanketi jeusi ambapo mganga akatuambia tayari aliandaa dawa, akaniambia nijongee karibu yake.
Nilipofanya hivyo akanielekeza kwamba baada ya kunichanja kwenye paji la uso wangu na kunipaka dawa, nitainama juu ya kile chungu ambacho kilikuwa na maji ya moto yenye dawa kisha atanifunika blanketi ili mvuke unifikie vizuri.
“Binti naomba fuata maelekezo yangu kwa umakini, hata kama utahisi unaungua usitoke kichwa juu ya chungu kwani dawa zitakuwa zinavuta vitu ulivyotupiwa ambavyo vinakutesa,” mganga aliniambia.
Mama aliyehofia ningeunguzwa na mvuke huo alipomuuliza mganga kama sitapata madhara, alicheka na kuniambia nisingeungua, ndipo alifunua mfuniko kikabaki kitambaa cheusi kilichokuwa juu ya kile chungu ambacho kilipitisha kwa mbali mvuke akaniambia niweke kichwa changu.
Baada ya kukiweka kichwa, alinifunika lile blanketi na kuniambia hata kama nitahisi naungua nisitoe paji la uso wangu juu ya kile chungu kwani nitakapohisi naungua ndipo vitu nilivyotupiwa kichawi vinatoka.
Nikiwa nimeinamisha kichwa ndani ya kile chungu, nilihisi kuungua nikawa nainua kichwa lakini mganga alinishika kichwani na kunizuia nisikitoe akanimbia nikiona naungua ndipo vitu nilivyotupiwa vilikuwa vikitoka.
Kila nilipojaribu kuinua kichwa, mganga alisisitiza nisikitoe na baada ya kufanya hivyo kwa dakika zisizopungua kumi, alifunua lile blanketi ambapo kila mmoja wetu alipigwa butwaa baada ya kuona vitu vya kutisha juu ya kile kitambaa cheusi kilichokuwa juu ya chungu.
Je, ni vitu gani hivyo vya ajabu vilivyoonekana?
 
SEHEMU YA 10






Tukiwa tunashangaa, mganga alisogea na kuchukua kichwa cha jogoo kilichokuwa cheusi, mdomoni kikiwa na kitambaa chekundu na utosini kilikuwa na unyoa mrefu.
Baada ya kushika kichwa hicho, alisogea karibu yetu na kutuambia kichwa hicho na vitu vingine vilivyokuwa juu ya kile kitambaa juu ya chungu ndivyo nilivyotupiwa kichawi.
Alipotoa kauli hiyo alitaka kumpatia mama akishike, kwa uoga mama akakataa, mganga alipomwambia mama mkubwa akishike kwa vile hakikuwa na madhara naye alikataa.
“Msiogope kwani hivi sasa hakina madhara yoyote,” Dorcas ambaye huo ndiyo ulikuwa mwanzo kukumbwa na mikasa alimkariri mganga.
Kufuatia akina mama kugoma, mganga alikitupa kile kichwa sakafuni na kusonya akaenda kuchukua vitu vingine vilivyokuwa juu ya kile kitambaa cheusi.
Kwa kuwa tulikuwa tumeketi mbali kidogo, hatukuweza kuona vizuri kitu alichokichukua hadi alipotusogelea akatuonesha, kila mmoja wetu alishangaa alipoona hirizi ndogo iliyokuwa ikipumua.
Akatuambia kama asingeitoa hirizi hiyo siku ambayo ingeacha kupumua ambayo ilibaki kidogo kufika ungekuwa mwisho wa maisha yangu.
Kama alivyofanya awali, hakutaka kumkabidhi mtu aliitupa sakafuni kisha alikwenda kuchukua kitu kingine na kurejea nacho, kilikuwa kitambaa ambacho ndani yake hatukujua kilikuwa na nini.
Alipokifungua, zilimwagika punje za mchele, maharage, unga na vitambaa vilivyofanana na baadhi ya nguo zangu na za mama, tulishangaa sana.
Yule mganga alisema vitu hivyo ndivyo nilitupiwa kichawi mwilini mwangu, akafafanua kwamba zile punje za mchele, maharage, unga na vipande vya nguo zangu nilifanyiwa na mbaya wangu kwa sababu ya wivu.
Aliongeza kuwa, watu wake yaani mizimu ilimwambia mwanamke huyo mchawi alikuwa akiwaonea wivu akina mama waliokuwa wakiuza maharage, mchele, na unga ndiyo aliamua kunitengeneza uchawi wa vitu hivyo ili anitese.
Pua aliongeza kuwa alikuwa akikereka sana jinsi mama zangu walivuokuwa wakinijalia kuanzia kula na mavazi ndipo alichungua nguo zangu kichawi na kutengeneza uchawi na kunitupia ili anitese.
“Sasa hautaumwa tena, kila uchawi uliotupiwa nimeutoa, nafikiri kila mmoja wenu ameushuhudia kwa macho yake, pole sana mjukuu wangu…hii dunia ina watu wabaya sana,” Dorcas anasema yule mganga aliwaambia.
Baada ya kutuambia hivyo alikusanya vile vitu vya ajabu akachukua kipande cha gazeti na kuviweka na kusema mama aliyefanya ule uchawi huko alikokuwa alikuwa akijua kilichokuwa kikiendelea na alikuwa analia.
Mama mkubwa ambaye alikuwa na hasira alisema na ushenzi wake alionifanyia alikuwa kilia nini, mganga akacheka na kusema:
“Si nimeuharibu uchawi wake ambao alitumia fedha nyingi na muda mwingi kuutengeneza ndiyo maana analia.”
Kutokana na kauli hiyo, mama alimwuliza alikoutoa uchawi huo, mganga alimwambia alioneshwa kwamba aliufuata Mbozi kwa mzee mmoja ambaye licha ya kujifanya mganga alikuwa mchawi.
Mganga huyo aliwaliza akina mama walitaka yule mama apewe adhabu gani, mama mkubwa akasema ili kuwapunguza wachawi majumbani hata akimuua ilikuwa sawa.
“Eti mama, unakubaliana na ushauri wa mwenzako?” mganga alimwuliza mama.
Mama ambaye alikuwa na huruma sana alipinga na kusema kwa kuwa nilikuwa nimepona hakukuwa na sababu ya kumfanya jambo lolote yule mchawi, mama mkubwa akaguna!
“Huyo hafai kuendelea kuishi, hivi mama Dorcas kama angekuulia huyu mtoto wako wa pekee ungejisikiaje, mimi sioni kama kuna sababu ya kumuonea huruma,” mama mkubwa alimwambia mama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom