Mkasa wa kweli: Kazi za ndani nchini Oman zilivyonikutanisha na kifo

SEHEMU YA 06



Niliegemeza mgongo wangu kwenye ukuta, taswira ya kijiji cha Makose mkoa wa Tanga huko nchini Tanzania ikanijia, kwa mara nyingine nililia mno kuona ndoto zangu za kuikomboa familia yangu katika maisha duni zimegonga mwamba huku nikisubiri kunyongwa hadi kufa masaa machache yajayo.
Nilikaa ndani ya kile chumba hadi asubuhi, mwanga wa jua la asubuhi ukapenya kupitia matobo ya kwenye bati na kuingia hadi ndani ya chumba kile.
Niliumia nilipo baini kuwa jua hilo ndio jua la mwisho kuliona duniani, masaa mawili badaye, mlango ulifunguliwa. Wakaingia askari wawili na wakanitaka nitoke nje.
Nilitolewa nje na kupelekwa tena kwenye ile ofisi ndogo ambayo niliingizwa jana usiku nikiwa na Hussein Jabal.
“Yuko wapi Hussein?” niliuliza.
“Unamuuliza nani maswali ya kijinga, nyamaza kimya” askari mmoja alinifokea.
“Nifanyie ikhisani ya jambo moja,” nilimwambia kwa upole huku machozi yakinilenga.
“Jambo lipi?”
“Naombeni msaada wa kuwasiliana na ubalozi wa nchi yangu ili nipate msaada wa kisheria. Pia yupo mwenyeji wangu aitwaye Mariamu ambaye anaishia hapa hapa Muscut maeneo ya Deira...”
“Tunasikitika hilo pia hatuwezi kufanya , taarifa zitakazo mfikia huyo Mariamu ni kuja kuchukua maiti yako.” alisema tena yule askari.
Nililia nikalia na kulia, hofu ya kunyongwa kwa kamba ilisambaa ndani ya kifua changu vibaya sana.
Walinifunika kitambaa cheusi usoni, mikono yangu ikiwa kwenye pingu. Nikachukuliwa na kupelekwa mahali ambapo nilisikia wakipataja kuwa panaitwa ‘slaughuter place’
Nilifikishwa ‘slaughuter place’ na kufunguliwa kitambaa, mbele yangu nikajiona nipo eneo lenye uwazi kama uwanja wa mpira, kulikuwa na jukwaa kubwa ambalo lilitengenezwa kama goli la mpira wa miguu, kamba nyingi zenye vitanzi zilikuwa zikining’inia kwenye goli lile nikabaini eneo hilo ndipo eneo lililohusika kwa kunyongea watu.
Katika kutazama huko nikaendelea kuona kitu kingine kilicho upasua moyo wangu vibaya mno, nilimwona Hussein akiwa kando ya jukwaa lile la kunyongea akiwa anafanya ibada kwa imani ya dini ya Kislamu.
“Husseiiiin!!” niliita kwa nguvu huku nikiamini kivyovyote vile Hussein amepewa nafasi ya kusali sala ya mwisho kabla ya kuning’ininzwa kwenye kitanzi. Wale askari wa kijeshi walinikaba shingoni.
“Wewe!!!. Kuleta ghasia kwa mtu anaye fanya ibada ni jambo baya...Eeh!!”
Nilishindwa kujibu kwa kuwa tayari nilikuwa nimefungwa kitambaa mdomoni, nikaishia kulia, wakati huo nilimwona Hussein akiwa amemaliza kufanya ile ibada na sasa askari walimfunga pingu mikononi mwake. Aligeuka akanitizama huku akitoa tabasamu lenye kila dalili ya kukata tama.
“Agripina naenda kunyongwa, nisamehe kwa kushindwa kukupeleka Mogadishu, nisamehe hata kwa kukusababishia kifo ilihali ukiwa na mtoto tumboni mwako. Nisamehe kwa kukusaliti na kutembe na mwanamke mwingine, nisamehe kwa kila kitu Aglipina.
Naamini tutaonana badaye. Inshallah...” Hussein alipaza sauti kunieleza.
Nibubujikwa na machozi mdomo wangu ukiendelea kuzibwa kwa tambala gumu.
Walimvalisha soksi nyeusi usoni wakamwongoza kumpandisha kwenye jukwaa la kunyongea. Askari wawili walimvisha kitanzi cha kamba ngumu shingoni na kuhakikisha wamekaza vizuri kisha wakashuka chini wakimwacha peke yake kwenye jukwaa.
Niliendelea kulia nikimwomba Mungu kimoyomoyo afanye mujiza wake kubadilisha kile kilichokuwa kikiendelea wasaa ule, lakini haikuwa hivyo. Askari aliyehusika na kubonyeza swichi ya kupandisha kamba juu alikuwa akingojea amri kutoka kwa kamanda mkuu.
“Kill him.”
Amri ya kunyonga ilitoka.
Mnyongaji alibonyeza swichi, kamba ikaanza kujiviringisha taratibu kwenda juu. Ilivyokuwa ikijivingirisha ndivyo ikawa inamnyanyua Hussein taratibu na hapo ikawa inamkaba shingoni kwa nguvu.
Sekunde kumi badaye Hussein alikuwa akining’inia juu na kutapatapa huku na kule. Miguu yake ilikuwa ikirukaruka huku kiwiliwili chake kikitetemeka kama anapigwa na shoti ya umeme. Hussein alijikojolea na wakati mkojo huo unapita sekunde tano zilizofuata Hussein alitulia tuli.
Tayari alikuwa MAITI!!!!!.
Bila kutegemea nilijkuta na mimi nikijikojolea kwa mara ya pili, nilikuwa na woga usiyo mithilika, niliona mwili wa Hussein ukiendelea kubembea kwenye kamba. Maisha ya Hussein hapa duniani yaliashia hapo. Kilichokuwa kimebaki kwakwe ni kushushwa kupelekwa mochwari kisha kuzikwa.
“Anayefuata kunyongwa ni wewe,”
Sauti ya kamanda ilisikika nyuma yangu. Tumbo likinichafuka nikahisi kutapika, bila kutarajia nikajisaidia haja kubwa na ndogo kwa pamoja.
Nilifunguliwa kile kitambaa mdomoni na kusogezwa eneo lilitandika zuria dogo kando kukiwa na maji kwenye ndoo ambayo nilitakiwa kunawa kabla ya kusali sala zangu za mwisho kisha kunyongwa kama ilivyokuwa kwa mpenzi wangu Hussein Jabal.
“Niacheni nirudi nyumbani, sitaki kufa mimi...sitaki.” nilisema kwa hamaniko kubwa huku nikilia. Hakuna aliyenijali, wote walinitaka nijinawishe kwa maji kisha waninyonge.
Niliendele a kuwasihi waniachie nirudi nyumbani kwetu Tanzania, lakini nao waliendela kunisihi nisali sala zangu za mwisho kwani muda wa mimi kufa utakapo wadia hawatakuwa na cha kusubiri zaidi ya kunitundika kweye kamba na kuninyonga.
Muda wa kunyongwa ulifika. Walinikamata askari wawili waliokuwa na nguvu na kunisukumiza kwenye jukwaa tayari kwa kunivisha kitanzi na kunyongwa.
“Mungu uko wapi wewe Mungu...Fanya kitu kwa ajili yangu baba, fanya sasa hivi Mungu wangu, nisaidie.” nilitamka maneno hayo kwa nguvu nikiwa nimechanganyikiwa vibaya sana.
Hata hivyo, fikra hizo zilibakia kuwa kichwani mwangu tu. Nilivishwa kitambaa cheusi kisha kitanzi, kamba ikakazwa shingoni mwangu na askari anayebonyeza swichi inayoruhusu kamba kunivuta kwa juu aliiendea swichi na kuibonyeza.

UKITAKA KUSOMA HADITHI YOTE NJOO WHATSAPP NA ELFU MBILI, NAMBA NI 0687750295
 
Huu sio mkasa wa kweli usipotoshe ni mkasa wa kutunga. Katika hadithi yako umetaja Deira, Deira haipo Oman, ipo Dubai. Halafu polisi hawawezi kunyonga bila idhini ya mahakama huu ni uongo ulio wazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom